Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa
mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa
akihojiwa na makachero.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za
kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa
fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.
Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za
simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia
marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.
Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa
nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo
aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.
Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa
siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni
mazuri. lakini hakitatajwa jina lake.