Anachechemea huku mkono wa kushoto akiwa ameufumbata kwapani, uso umekumbwa na maumivu yanayoshindana na tabasamu hafifu analojaribu kulitoa. |
ANAFAHAMIKA zaidi kwa jina la Mzee Small, lakini jina lake halisi ni Small Wangamba.
Ana
sifa nyingi, lakini iliyo kubwa ni ucheshi, uchangamfu, ukarimu na kila
aina ya bashasha. Hata hivyo kwa sasa hali yake ni tofauti, mambo mengi
yamebadilika.
Sipati
shida kumpata pale nilipokusudia kumfikia na hata ninapofika nyumbani
kwake katika banda la vyumba viwili ambavyo vimemalizwa kujengwa hivi
karibuni, napokewa na msichana anayenikaribisha katika kiti nje ya
kibanda hicho.
Ujumbe
unapelekwa ndani kwa Mzee Small kuwa ana mgeni na dakika 20 baadaye
mlango unafunguliwa, anachomoza mtu ambaye sipati taabu kumfahamu kuwa
ni Mzee Small, mwigizaji nguli ambaye maradhi yamemkalisha kitako.
Anachechemea
huku mkono wa kushoto akiwa ameufumbata kwapani, uso umekumbwa na
maumivu yanayoshindana na tabasamu hafifu analojaribu kulitoa.
Hali
hiyo inaakisi wimbo mmoja wa Shakila Abdallah ‘Bi. Shakila’ wenye
mashairi ‘Macho yanacheka moyo unalia’. Kimsingi Mzee Small anaumwa
ingawa anajaribu kutabasamu, kinachoonekana katika paji lake la uso ni
tofauti na tabasamu hafifu analojaribu kulitoa pale macho yetu
yanapogongana na wakati wa mazungumzo anabainisha kinachomsibu.
“Sipo
vizuri, naumwa. Kwa sasa inawezekana ikaonekana kama nina nafuu kidogo,
lakini naumwa,” anasema baada ya kunikaribisha katika chumba kimoja
ambacho anakimiliki na mkewe.
Chanzo cha tatizo
Anasema
tatizo lake lilimuanza Mei mwaka jana baada ya kurudi kutoka Mwanza
alikokuwa na kazi ya kutumbuiza katika tamasha la kupambana na mauaji ya
Albino. Tamasha hilo liliratibiwa na Kituo cha Under The Same Sun .
“Nilitoka
Uwanja wa Ndege (Dar es Salaam) na kufika hapa nyumbani, nikaingia
chooni moja kwa moja. Lakini wakati natoka, nikadondoka. Nilipojitahidi
kunyanyuka haikuwezekana hivyo nikabebwa hadi chumbani,” anasema.
Anasema
akiwa chumbani alijaribu kujinyanyua akajikuta anadondoka tena, hivyo
akawahishwa hospitali moja jirani na nafuu haikupatikana.
Ikalazimika
apelekwe Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam ambako alilazwa siku
tatu kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
No comments:
Post a Comment