Mwanamuziki
staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika
anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya
madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka. Hivi karibuni, Ray C
ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika
kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka
karibu na mashabiki wake.
Kufuatia
ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na
picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na
alivyozoeleka.
UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.
Hata
hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo
inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa
aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya
unga.
AFUTUKA
Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo.
Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki.
Ray
C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa
kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza
zenyewe.
HATAKI KUTAJA ANAPOISHI
Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani.
Kwa
mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu
huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia
kimatibabu.
DAKTARI ANASEMAJE?
Daktari
mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa na gazeti hili, alibainisha kuwa
kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba kinachomnenepesha ni dozi ya
kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.
Aliongeza
kuwa kunenepa kunachangiwa na vitu vingi kama kupata maisha mazuri
yasiyohusisha msongo wa mawazo au mihangaiko ya hapa na pale hivyo
anachofanya ni kula, kulala na kustarehe tu.
No comments:
Post a Comment