Monday, July 29, 2013

MDC WALALAMIKIA UCHAGUZI ZIMBABWE....!!!

zimbabwe 4a402

 
CHAMA cha waziri mkuu nchini Zimbabwe kimesema kuwa mmoja wa ofisa wake mkuu wa chama hicho amekamatwa baada ya kuwasilisha ushahidi wa udanganyifu mbele ya tume ya uchaguzi nchini humo.
  Morgen Komichi aliifahamisha mamlaka baada ya kugundua makaratasi ya kupiga kura yalikuwa yamewekwa katika kituo cha kupiga kura mjini Harare ambapo maafisa wa jeshi walipiga kura za mapema katika uchaguzi huo. (HM)

Alisema masanduku yote ya kura yaliyokuwa na kura za chama cha Movement For Democratic Change (MDC) yalitupwa.

MDC kinachoongozwa na waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, kimekuwa katika serikali ya umoja wa kitaifa na rais Robert Mugabe wa ZANU PF , Umoja ambao umekuwa na mashaka ndani yake.
Uchaguzi nchini Zimbabwe umefanyika mapema Jumatano iliyopita.
Chanzo: bbcswahili

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...