Saturday, June 01, 2013

SERIKALI YAOMBELEZA KIFO CHA MANGWEA

untitled25 a7fc8
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA
BW. ALBERT MANGWEA, (Man Ngwair)
1/06/2013.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne tarehe 28 Mei, 2013.Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya "Free Style" alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi.
Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.
Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.
Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
"Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangwea mahala pema peponi."
Imetolewa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...