Friday, May 31, 2013

TANGAZO MUHIMU KWA UMMA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA

 
 Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo
na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html

Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais. 


Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyotemwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulip a ada ya shilingi 37,000/=.BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.


Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
 

IMETOLEWA NA
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...