Friday, June 24, 2016

MAOMBI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU 2016/2017

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kutoa taarifa kwa Umma na wadau wake wote kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya Mikopo kwa mwaka wa masomo 2016 /2017 kuanzia tarehe 27 Juni 2016 hadi tarehe 31 2016.

Katika kipindi hicho waombaji wa mikopo watarajiwa wanapaswa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku (GUIDELINES AND CRITERIA FOR ISSUANCE OF STUDENTS’ LOANS AND GRANTS FOR THE 2016/2017 ACADEMIC YEAR) uliopo kwenye tovuti hii ya Bodi ili kufahamu sifa za mwombaji na taratibu kufuata kabla ya kuomba mikopo kwa njia ya mtandao.

Utoaji wa Mikopo unaongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Na. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) hususani vifungu vyake vya 16 na 17.
Kwa taarifa hii, waombaji wote wa mikopo wanatakiwa kusoma mwongozo huo kabla ya kujaza maombi ya mikopo na wazingatie kuwa tarehe ya mwisho ya kuomba mikopo ni Julai 31, 2016.

Wednesday, June 22, 2016

MMILIKI WA TP MAZEMBE AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA

Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise Katumbi amehukumiwa kwenda jela, Katumbi ambaye ni boss wa TP Mazembe amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.
Katumbi amehukumiwa miaka mitatu sambamba na kutozwa faini ya dola milioni 6 kwa kosa la kujimilikisha eneo, Katumbi pia alikuwa anatajwa kugombea nafasi ya Urais wa Kongo mwishoni mwa mwaka 2016 kupitia chama cha upinzania kushinda na Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila.
rts7qug-e1462504316478
Hata hivyo wakati wa kutolewa hukumu hiyo Moise Katumbi hakuwepo Kongo, siku moja kabla ya hukumu alikuwa kasafiri kwenda Afrika Kusini kupata matibabu, makosa mengina anayotuhumiwa nayo Katumbi ni pamoja na kutajwa kuajiri wa geni kutoka nje ya Kongo kwa ajili ya kuandaa njama za kumuondoa Rais Kabila.
Moise Katumbi ndio Rais wa klabu ya TP Mazembe aliyoingoza kucheza hadi hatua ya fainali ya klabu Bingwa ya dunia dhidi ya Inter Milan December 18 2016, rekodi ambayo hakuna klabu ya Afrika imewahi kuifikia, TP Mazembe ndio ya kwanza, TP Mazembe wanakuja Tanzania June 28 kucheza mchezo wao wa pili wa nane bora dhidi ya Yanga.

Monday, June 20, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 20, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

IMG_20160620_060923 IMG_20160620_060948 IMG_20160620_061043 
Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

YANGA YASHINDWA KUTAMBA KWA WAARABU YAPIGWA 1-0

 Mabingwa wa soka la Tanzania bara Yanga SC wameanza vibaya kampeni zao za kuwania kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya MO Bejaia ukiwa ni chezo wa Kundi A.

Yassin Sahli alifunga bao pekee kwenye mchezo huo na kuipa pointi tatu MO Bejaia iliyokuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani Stade de I’Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.
Matokeo hayo yanaiacha Yanga katika nafasi ya tatu huku TP Mazembe wakiwa ndiyo vinara wa Kundi baada ya kushinda mchezo wao kwa magoli 3-0 dhidi ya Medeama ambayo inaburuza mkia.

Mazembe na MO Bejaia zinapointi sawa (pointi tatu) lakini TP Mazembe anaongoza kundi kwa tofauti ya magoli wakati Yanga na Medeama zikiwa hazina pointi lakini Yanga inakaa nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli. Medeama imefungwa magoli matatu wakati Yanga wameruhusu bao moja pekee.
Mchezo ujao wa Yanga utakuwa nyumbani (Dar es Salaam) June 28 itakapowaalika TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...