Thursday, April 24, 2014

KOCHA MPYA WA TAIFA STARS KUWASILI JUMAMOSI APRIL 26.

KOCHA

Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.
Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mart Nooij ni raia wa Uholanzi, na ameshawahi kufanya kazi katika nchi ya Mozambique kama kocha mkuu wa timu ya taifa, Burkina Faso U20, na pia ameifundisha timu ya Santos ya Afrika ya Kusini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI KUBWA NA YA KISASA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea nchini Mhe Chung IL wakiwa mbele ya mchoro wa mfano wa Hospitali ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na msanii Mrisho Mpoto baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL na viongozi wengine  wakikata utepe kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, April 24, 2014. (PICHA NA IKULU)
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Sunday, April 20, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA PASAKA APRIL 20, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.




.Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

HII KALI.. WAUMINI WASAFISHA BARABARA YA LAMI KWA SABUNI...!!!

Screen Shot 2014-04-20 at 1.08.01 AM
Wakazi wa jiji la Eldoret wamemfanya kila alieiona hii kuvutiwa na pengine kujua imekuaje wakafanya hivi kwa mara ya kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.
Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya jana na siku ya Jumatatu kuadhimisha Pasaka na kumshukuru Jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013.
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni yalikotolewa na Wakenya kuhusu ishu hii, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha waumini hao wa kanisa la Jesus is Lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima kupita kiasi.
Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya Kass Fm inayotangaza kwa lugha ya Kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la Eldoret Julius Lamaon, amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria mkutano huu’ Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na Millard Ayo

Thursday, April 17, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRIL 17, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.



.


.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

ANGALIA UKAWA WALIVYOLISUSA BUNGE MAALUM LA KATIBA JANA

Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao


Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...