Friday, March 04, 2016

"ARSENAL HATUJIAMINI" SANCHEZ

Alexi Sanchez 
Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa Arsenal haina imani kwamba itashinda ligi ya Uingereza baada ya kushindwa mara mbili mfululizo na Manchester United na Swansea. The Gunners walipoteza 3-2 katika uwanja wa Old Trafford na 2-1 nyumbani dhidi ya Swansea na hivyobasi kuwa pointi sita nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.

''Mara nyingine tunakosa motisha kwamba tayari tumeshinda 1-0 tunapoelekea uwanjani'',aliiambia Directiv Sport kabla ya mechi dhidi ya United.''Tunakosa ile ari kwamba tunaweza kuwa mabingwa''. Sanchez aliongea: Iwapo tutaingia katika uwanja na ari ya kuwa mabingwa ,kushinda ligi ama hata kombe la vilabu bingwa Ulaya,tunaweza kuafikia hilo.

''Ninakumbuka mechi dhidi ya Manchester United mwaka uliopita.Wachezaji walikuwa na motisha ya kushinda taji tulipoingia uwanjani.Tuliwashinda katika dakika 20 na kupata 3-0.Tulikuwa na ari na kujiamini siku hiyo''. Arsenal imeshinda mara tatu pekee kutoka mechi 11 katika mashindano yote na wako katika nafasi ya tatu katika ligi.

Tuesday, March 01, 2016

DAKTARI ASIMAMISHWA KAZI KISA LAKI MOJA

Baada ya kufichua uozo katika bandari tatu kubwa hapa nchini, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehamia katika afya baada ya kumsimamisha kazi daktari wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Ligula, Fortunatus Namahala kwa madai ya kumuomba mgonjwa rushwa ya Sh100,000.

Waziri Mkuu alichukua hatua hiyo jana alipotembelea hospitali hiyo ya mkoa na kukabiliwa na Tatu Abdallah ambaye alidai kwamba alilazimika kuuza shamba lake la ekari 2.5 ili apate Sh100,000 kwa ajili ya upasuaji wa baba yake.

“Februari Mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunue dawa za Sh85,000 hapo nje kwenye duka la dawa pia uzi wa kushonea kwa Sh25,000. Lakini pia daktari akasema anataka Sh100,000 ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji,” alidai.

'SERIKALI YA AWAMU YA NNE ILIJAA KULEANA' JANUARY MAKAMBA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba amesema uwajibikaji katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne haukuwa wa kuridhisha kwa sababu kulikuwa na utamaduni wa kuoneana haya, kujuana, kusitiriana na kutoogopa.

Amesema hayo yalikuwa yakitokea kwa kuwa waliokuwa wakifanya makosa hawakuwa wakichukuliwa hatua na hivyo kujengeka utamaduni wa watu kutoogopa, lakini sasa utawala mpya umeonyesha kuchukua hatua dhidi bila ya woga.

Makamba, ambaye aliingia tano bora ya mbio za urais ndani ya CCM kabla ya kuangushwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu, alitoa kauli hiyo juzi katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam juzi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...