Thursday, January 07, 2016

MTOTO WA KARUME ASHAURI SHEIN KUKAA PEMBENI

Mwanasheria wa kujitegemea nchini, Fatma ofisinakizungumzaini Dar es Salaam jana. Picha na Florence Majani

Dar es Salaam: Mwanasheria wa kujitegemea nchini, Fatma Karume amemshauri Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein kuachia madaraka.

“Dk Shein lazima aondoke kwa sababu kuendelea kubaki madarakani ni kuwanyang’anya Wazanzibari haki yao ya msingi,” alisema Fatma ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Fatma alisema kuwa mzozo wa Zanzibar umesababishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kutangaza kufutwa matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu visiwani humo wakati hana mamlaka kisheria kufanya hivyo.

JANUZAJ KUREJEA MAN U

Manchester United imemwita nyumbani Adnan Januzaj kutoka Borussia Dortmund ambako amekuwa kwa mkopo wa msimu mmoja.

United wamemtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji arejee Old Trafford kwa sababu ya kukosa kuchezeshwa Ujerumani.

Januzaj, mwenye umri wa miaka 20, amecheza mechi 12 pekee katika klabu hiyo ya Bundesliga, sana akiingia kama nguvu mpya.

Tuesday, January 05, 2016

PROF. JAY KUHAMISHIA STUDIO YAKE MIKUMI

MSANII na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, amesema ana mpango wa kuihamishia studio ya Mwanalizombe kwenye jimbo lake ili aweze kutekeleza ahadi ya kuinua sanaa. Profesa Jay alisema kuwa moja ya ahadi alizowaahidi

wakazi wa Mikumi kwenye kampeni zake ni kuibua vipaji vipya ndiyo maana ameamua kuihamishia studio hiyo huko ili aweze kutekeleza ahadi hiyo.

“Mikumi kuna vipaji vingi vya muziki lakini hakuna aliyeweza kuviibua kwa miaka mingi, ila mimi nikiwa kama Mbunge wao nitatekeleza ahadi hii kwa kuihamishia studio yangu Mikumi ili wasanii chipukizi waweze kufanya kazi zao,” alisema Profesa Jay.

Mwanalizombe ni studio inayomilikiwa na msanii huyo ipo maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es salaam na imeshatoa nyimbo kali kama Makamanda wimbo wa Sugu, Tatu Chafu na Kipi Sijasikia chini ya mtayarishaji Villy.

BENITEZ ATUPWA NJE REAL MADRID, ZIDANE ACHUKUA NAFASI

Uongozi wa klabu ya Real Madrid umemtimua kocha wake Rafael Benitez ambaye ana Miezi 7 tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu.

Sasa nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mkongwe mfaransa Zinedine Zidane ambaye awali alikuwa Kocha wa Kikosi B cha Real Madrid .

Hii inatokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka Sare 2-2 na Valencia, katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.

Tangu atue Madrid, Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona, pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...