Friday, October 03, 2014

KURA MBILI ZAPITISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

http://jambotz8.blogspot.com/

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Deo Sanga akisakata muziki katikati ya Ukumbi wa Bunge hilo baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura zilizopigwa kupitisha Rasimu ya Mwisho ya Katiba inayopendekezwa mjini Dodoma jana.


Dodoma/Dar. Licha ya upinzani kutoka makundi kadhaa ya wananchi, Bunge la Katiba jana lilihitimisha kazi yake kwa kupitisha Katiba inayopendekezwa baada ya kupata theluthi mbili za wajumbe wa kila upande wa Muungano.

Matokeo hayo yaliyohitimisha mchakato huo, yalifanikishwa kwa tofauti ya kura mbili za wajumbe katika baadhi ya ibara na nyingine kwa kura moja tu, ikimaanisha kuwa iwapo kura hizo mbili zingekosekana hadithi ingekuwa tofauti.

 Kutangazwa kwa matokeo hayo kuliwafanya wajumbe walioshiriki mchakato hadi hatua ya mwisho baada ya wenzao wa kundi la Ukawa kususia, kulipuka kwa furaha, nyimbo, tambo, vijembe na vigelegele huku wakijimwaga ukumbini kusakata dansi.

Akitangaza matokeo hayo, Naibu Katibu wa Bunge hilo, Dk Thomas Kashililah alisema hali ya upigaji kura ilikuwa ni nzuri na kila kura za kila upande zilitosheleza na kutoa uhalali wa Katiba inayopendekezwa kupelekwa kwa wananchi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PINDA: "KATIBA IPATIKANE KABLA YA RAIS MPYA"


Bunge Maalumu la Katiba, kabla ya kuahirishwa kwake 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema atafurahi kuona mchakato mzima wa Katiba ukikamilika kabla rais mpya hajapatikana katika Uchaguzi Mkuu ujao, pendekezo ambalo ni kinyume na makubaliano baina ya Rais Jakaya Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuwa upigaji wa kura ya maoni ufanyike baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Akizungumza Bungeni baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta kutoa shukrani, Pinda alipendekeza kura ya maoni ipigwe sambamba na Rais ili kiongozi ajaye afanye kazi ya kutekeleza matakwa ya Katiba hiyo.

Alisema rais ajaye anaweza kuwa na ajenda zake, hivyo ni muhimu kumaliza kazi yote na kumkabidhi Katiba ambayo imekamilika ili aitekeleze.

“Nampongeza sana mwenyekiti kwa kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana kwa wakati na kwa kuzingatia maoni ya wananchi,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Alichojifunza

Pinda alieleza kuwa katika mchakato huo wa Mabadiliko ya Katiba, amejifunza mambo makuu manne, kubwa likiwa ni kutii sauti ya wengi, kwani ni sauti ya Mungu. Alisema wingi wao bungeni ni kiashiria cha uwepo wa sauti ya Mungu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAFUNZI 40 MEXICO WAPOTEA

http://jambotz8.blogspot.com/
Mamia ya wanafunzi nchini Mexico katika jimbo la Guerrero wameandamana katika mji mkuu wa jimbo la Chilpancingo kulalamikia kutoweka kwa zaidi ya wanafunzi wenzao arobaini wiki iliyyopita.
Wanafunzi hao wanasemekana kuwa mwisho walionekana kusombwa katika magari ya polisi kufuatia maandamano walioshiriki wakilalamikia ubaguzi katika ajira ya walimu wa maeneo ya vijijini.
Polisi walifyatua rissasi kwenye basi na kwa waandamaji na kuua watu sita na wengine 17 kujeruhiwa.
Maafisa ishirini na wawili wa polisi wanashikiliwa na kwa kutuhuma za kufyatua risasi.
Ndugu ya waliouawa wanaosaidiwa na polisi waliingia mlango kwa mlango katika eneo la Iguala wakiwa wameshikilia picha za wapendwa wao na kutafuta eneo ambalo miili ya ndugu zao ilipofichwa. Serikali ya jimbo hilo imetoa dola 75,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa kueleza wanafunzi hao walipo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAFUNZI WA HONG KONG KUKUTANA NA SERAKALI

http://jambotz8.blogspot.com/
 
Viongozi wa wanafunzi huko Hong Kong wamekubali kukutana na upande wa serikali kujadili malalamiko yao siku tano baada ya maandamano makubwa ya kupigania demokrasia.
Hiyo inafuatia mwaliko kutoka kwa mkuu wa utawala wa Hong Kong CY Leung. Alitoa taarifa hiyo muda mfupi kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao waliotishia kuvamia majengo ya serikali iwapo mkuu huyo hatajiuzulu.
Muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao umemalizika salama.
Bwana Leung amesema atabakia madarakani na kuwaonya waandamanaji kuwa watapata matatizo iwapo watavamia majengo ya serikali.
Kumekuwa na makabiliano makali katika eneo la majengo ya serikali ambapo waandamanaji wamekuwa wakiendelea kudai uchaguzi wa haki mwaka 2017. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 03, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MIAKA 15 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWL. J. K. NYERERE

Kutoka kushoto ni Marehemu Habib Halala, Mzee Paul Soizgwa, JK Nyerere, Brig. Hashim Mbita, Mzee Benjamin Mkapa, siku kumi kabla ya JK kustaafu uraisi 1985.  Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Thursday, October 02, 2014

HAWA NDIO WAKE WA MARAIS WA AFRIKA WANAOTIKISA...!!!

 
Ana Paula Dos Santos.
alizaliwa1964, ni mke wa Rais wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, Paula ni mwanamitindo wa zamani, anasifika kwa uzuri na kujua kuvaa.
Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, alizaliwa 1963, anatajwa kuwa katika orodha ya wake wazuri wa marais wa Afrika, anasifika kwa mavazi yake ya kitenge.
Margaret Wanjiku Kenyatta.
Ni mke wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, anatajwa kuwa na tabasamu zuri ingawa nywele zake zenye rangi ya kijivu ni kivutio kikubwa. Kazaliwa Mwaka 1963.
 
Hinda Deby Itno.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TAARIFA TOKA BUNGE LA KATIBA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR


Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NAFASI ZA AJIRA WIZARA YA MAMBO YA NDANI {UHAMIAJI}

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anatangaza nafasi za kazi zifuatazo katika Idara ya Uhamiaji kwa Raia wote wa Tanzania wenye sifa. 

1. KOPLO WA UHAMIAJI Nafasi 114 - (Nafasi 100 kwa ajili ya Tanzania 
Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu) 
A. SIFA ZA MWOMBAJI: 
(i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 25 hadi 30. 
(ii) Awe amehitimu kidato cha sita na kufaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili, Historia, Jiografia, Kifaransa, Hisabati ambapo masomo mawili kati ya hayo yawe katika kiwango cha “Principal”. 
(iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo:
• Cheti cha Sheria; 
• Cheti cha Kompyuta; 
• Cheti cha Ufundi (FTC) kwenye fani ya umeme na mitambo 
(iv) Waombaji wenye ujuzi wa mojawapo ya lugha zifuatazo (Kifaransa, Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza. 
(v) Aidha, Mwombaji aliyepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa atapewa kipaumbele. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA CHAMA CHA ACT-TANZANIA KUHUSU ZITTO KABWE

 Zitto Kabwe
--
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPERANCY. 
--
Ndugu wanahabari kumekuwa na utaratibu wa habari zinazoupotosha umma wa watanzania kuhusu chama chetu cha ACT-Tanzania.

Katika gazeti la mwanahabari toleo na 117 la tarehe 29/09/2014 katika ukurasa wake wa mbele iliandikwa "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA CHA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".

Act-Tanzania tunaeleza kuwa ni chama cha watanzania wote kisichokuwa na mmilki wake na tunaunganishwa na misingi kumi ya chama pamoja na Itikadi yetu ya Demokrasia jamii.

Act-Tanzania tunatambua uwezo na mchango wa kisiasa na ujenzi wa demokrasia ya vyama vyingi nchini uliotolewa na Mheshimiwa Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KAJALA AMSHTAKI MAMA WEMA...!!!

KIMENUKA! Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja.
Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa Wema, Kajala Masanja.
KUNASWA KWA SAUTI NA PICHA
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.
 
Wema Sepetu akiwa na mama yake.
KAJALA AAMUA ZITO
Katika kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

GARDNER ATAKA JIDE AELEZE UKWELI JUU YA NDOA YAO


Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha mtangazaji mwenye jina kubwa wa Kipindi cha Maskani cha Redio Times FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’ kutaka mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ndiye aeleze ukweli juu ya ndoa yao.
 
Mtangazaji wa Redio Times FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’
Akizungumza kwenye Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia Televisheni ya EATV chini ya ‘hosti’ wake, Salama Jabir, Jumanne iliyopita, Gardner alikataa kuzungumzia ndoa yake inayodaiwa kuvunjika.
Pamoja na mambo mengine ambayo aliyajibu kwa ufasaha, Gardner alipoulizwa juu ya habari zinazozungumzwa mtaani kuhusu kuvunjika uhusiano wake na Jide au Lady Jaydee, aligoma kulizungumzia kwa kigezo kwamba kipindi hicho kilimhusu yeye tu.
 
Mwanamuziki wa Bongo fleva kitambo, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’
Mtangazaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia Salama kwamba amwite Jaydee kwenye kipindi hicho ili alielezee jambo hilo kwa undani.Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakielea.
Kupitia kipindi chake cha Diary of Lady Jaydee kilichokuwa kikisimamiwa na Gardner ambacho sasa kinaongozwa na ndugu wa msanii huyo aitwaye Wakazi, Jumapili iliyopita Jide alionekana kwenye harusi ya ndugu yake aitwaye Lameck Mbibo ‘Dabo’ ambaye pia ni msanii wa Dance Hall akiwa mpweke bila mumewe kama ilivyozoeleka. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na GPL

RAILA ODINGA ATANDIKWA BAKORA HADHARANI...!!!

Mzee Mdzombo anasemekana kutokuwa timamu kiakili
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amemsamehe mzee aliyempiga bakora katika mkutano wa hadhara wa kisiasa katika jimbo la Kwale Pwani ya Kenya,
Mwanamume huyo, Lengo Mdzombo, anayefanya kibarua katika shamba moja Kwale, alikamatwa Jumanne na kufikishwa mahakamani.
Alishitakiwa kwa kosa la kumshambulia kiongozi huyo pamoja na gavana wa Kwale.
Hali ya taharuki ilitanda katika mkutano wa hadhara Jumatatu wiki hii baada ya Mdzombo kwenda ukumbini na kuanza kumtandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Raila alikuwa ameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga
Mzee huyo alimpiga bakora Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani kwa nini mwanamume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wanasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

ARSENAL YAUA 4-1, WELBECK APIGA HAT-TRICK


Mshambuliaji Danny Welbeck akishangilia baada ya kupiga 'hat-trick'.

Alexis Sanchez akiifungia Arsenal bao la tatu dhidi ya Galatasaray.

Welbeck akitupia bao la nne. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametimiza miaka 18 akiwa meneja wa klabu hiyo leo.
KLABU ya Arsenal imetoa kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London usiku huu.
Mshambuliaji Danny Welbeck ametupia kambani mabao matatu 'hat-trick' huku bao la nne likiwekwa kimianai na Alexis Sanchez. Katika mtanange huo, kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Galatasaray, Burak Yilmaz.
Ushindi wa leo wa Arsenal umeongeza furaha kwa Meneja wa timu hiyo, Arsene Wenger aliyetimiza miaka 18 akiwa kocha wa klabu hiyo leo.
VIKOSI: 
Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Cazorla, Ozil (Wilshere 77), Sanchez (Ospina 62), Oxlade-Chamberlain (Rosicky 68), Welbeck.
Waliokuwa benchi: Coquelin, Bellerin, Campbell, Podolski.
Galatasaray: Muslera, Chedjou, Felipe Melo, Semih Kaya, Veysel (Bulut 68), Yekta (Altintop 46), Dzemaili, Telles, Sneijder, Pandev (Bruma 68), Burak Yılmaz.
Waliokuwa benchi: Bolat, Balta, Adin, Camdal. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 02, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...