Thursday, October 02, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 02, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MKUU WA USALAMA MAREKANI JIUZULU

Julia Pierson mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Marekani
Mkuu wa Idara ya Usalama nchini Marekani, aliyekuwa na jukumu la kumlinda Rais Barack Obama, amejiuzulu kufuatia matukio yenye kuhatarisha usalama wa taifa yaliyotokea.
Mkuu huyo wa usalama Julia Pierson alikabidhi barua ya kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Jumatano.
Siku moja kabla, alikabiliana na maswali ya wajumbe wenye hasira kutoka Baraza la Congress juu ya udhaifu mkubwa wa usalama wa Ikulu ya Marekani
Habari za tukio lingine likimhusisha mtu mwenye silaha kuruhusiwa kuingia katika lifti moja na Bwana Obama kulizidisha kutolewa wito wa kumtaka mkuu wa usalama kujiuzulu.
"Leo, Julia Pierson, mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Marekani, amenikabidhi barua ya kujiuzulu, na nimeikubali," Waziri wa Usalama wa Taifa Jeh Johnson aliandika katika taarifa.
"Nampongeza kwa utumishi wake wa miaka 30 katika idara ya usalama na taifa." Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

CHINA YAONYA MGOGORO WA HONG KONG

 Waandamanaji Hong Kong
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ametoa onyo kali dhidi ya maandamano "yasiyo halali" Hong Kong.
Akiwa katika ziara nchini Marekani, Bwana Wang pia alionya kuwa suala la Hong Kong linahusu "mambo ya ndani" ya China
Waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ameitaka Hong Kong kujizuia na matumizi ya nguvu wakati wa kushughulikia maandamano hayo.
Mapema, waandamanaji wanafunzi waliokasirishwa na China kuwateua wagombea wa uchaguzi wa mwaka 2017 waliapa kuendelea na maandamano iwapo kiongozi wa Hong kong, CY Leung hatajiuzulu.
Wamesema waandamanaji wataanza kukalia majengo ya serikali kama Bwana Leung hatajiuzulu ifikapo Alhamisi.
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na John Kerry wa Marekani
Waandamanaji walikusanyika usiku kucha nje ya ofisi ya Bwana Leung, huku polisi 200 wakiwa katika eneo hilo.
Bwana Wang, afisa mwandamizi wa China wa ngazi ya juu akizungumzia waziwazi suala hili, alisema: "Masuala ya Hong Kong ni masuala ya ndani ya China. Nchi zote lazima ziheshimu uhuru wa China kujiamulia mambo yake yenyewe. Kwa nchi yoyote, kwa jamii yoyote, hakuna atakayeruhusu vitendo vilivyo kinyume cha sheria vinavyokuika utulivu wa umma."
Hata hivyo, alisema: "Tunaamini kuwa Utawala maalum wa serikali ya jimbo la Hong Kong ina uwezo wa kushughulikia hali hii kwa mujibu wa sheria."
Bwana Kerry amesema Marekani inaunga mkono madhila ya jumla huko Hong Kong, akisema: "Tuna matumaini makubwa kwamba mamlaka ya Hong Kong itajizuia kutumia nguvu na kuheshimu haki ya waandamanaji kueleza mawazo yao kwa amani." Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Wednesday, October 01, 2014

BUNGE LA KATIBA: WALIOPIGA KURA YA HAPANA WATISHIWA MAISHA


Wahudumu  wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa wamebeba masanduku ya kura za wajumbe waliopiga kura za siri kwa Sura ya 11 hadi 19 ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, mjini Dodoma jana.

Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba waliopiga kura za hapana wamelazimika kuondoka Dodoma na kurudi Zanzibar kwa madai ya vitisho walivyopata kutoka kwa wenzao.

Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana jioni kuwa yeye na wajumbe wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu kura hiyo na kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao wameamua kuondoka Dodoma.

Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya Sitta kuunda Kamati ya Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na wajumbe saba zinazoweka njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya kupitisha Katiba inayopendekezwa.

Wajumbe waliopiga kura za wazi za hapana kwa ibara zote ni Adil Mohamed Adil, Dk Alley Soud Nassor, Fatma Mohamed Hassan, Jamila Ameir Saleh, Salma Hamoud Said, Mwanaidi Othman Twahir na Ali Omary Juma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WALIODHURIKA KWA TOGWA SONGEA WAFIKIA 340...!!!


 

Idadi ya watu waliolazwa hospitalini kwa kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Litapwasi, Kata ya Mpitimbi mkoani Ruvuma imeongezeka kutoka 270 hadi 340.

Tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya watu kushiriki sherehe ya Kipaimara ambako walikula, kunywa pombe na togwa na baadaye wale waliokunywa togwa walianza kuumwa matumbo, kuhara na kutapika.

Hadi jana, watu 102 walikuwa bado wamelazwa katika Zahanati ya Lyangweni, Hospitali ya St. Joseph Peramiho na Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.

Tayari watu watano wanashikiliwa na Polisi kwa upelelezi kuhusiana na tukio hilo, akiwamo Baba Mzazi wa mtoto Dickson aliyepata kipaimara, Enes Nungu (47). Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...