Thursday, February 13, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS FEBRUARI 13, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS



Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TOYOTA YATOA AGIZO LA KUREJESHA MAGARI KIWANDANI...!!!

prius22_b3ff7.jpg
Kampuni ya kutengeza magari ya Toyota nchini Japan, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni 1.9 aina ya Prius katika kiwanda cha magari hayo nchini Japan.
Hii ni kutokana na hitilafu ya kimitambo ambayo inaweza kusababisha gari hilo kukwama.
Gari la Prius ni moja ya magari yenye muundo unaonyesha ubunifu wa hali ya juu wa kampuni ya Toyota.
Gari hilo linaweza kutumia petroli na betri huku likitoa kiwango kidogo sana cha moshi kuliko magari ya kaiwada.
Sasa kampuni hiyo imetambua hitilafu ya programu ya gari hilo ambayo inaweza kusababisha vifaa vya elektroniki vya gari hilo kukwama.
Magari mengi yenye hitilafu hiyo yako nchini Japan na Amerika ya Kaskazini na Toyota inasema kuwa haijapokea taarifa zozote za ajali au majeraha kutokana na hitilafu hiyo. CHANZO BBC
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

KAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU MADAI YA WAFANYABIASHARA NA TRA...!!!

Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema Zitto Kabwe muda mfupi uliopita kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ametoa yake ya moyoni kwa hili seke seke linaloendelea nchini juu Wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania[TRA]kuhusu mashine za kutolea risiti za EFD.
Zitto alianza kwa kuandika>>’EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni’
‘Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000′
‘Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika’
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

GHASIA ZAONGEZEKA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

dede_d2268.jpg

Takriban wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na 6,000 wa Umoja wa Afrika wamo nchini humo kujaribu kulinda raia wakati ghasia zenye maafa zikiendelea kati ya Wakristo na Waislam.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa anasema lazima tahadhari zichukuliwe ili Jamhuri ya Afrika ya Kati isigawanyike. Onyo hilo limetolewa huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakionya kuwa mauaji ya kikabila yanaendelea katika taifa hilo lililokumbwa na mgogoro wa kisiasa.
Waziri huyo Jean Yves Le Drian alifanya mazungumzo mjini Bangui na maafisa wa ngazi ya juu ya jeshi la Ufaransa pamoja na kaimu rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba- Panza aliyeungana naye wakati wa ziara yake kusini magharibi mwa nchi.
Hii ni mara ya tatu kwa waziri Le Drian katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, tangu Ufaransa ilipozindua operesheni ya kijeshi mwishoni mwa mwaka jana. Onyo lake limetolewa huku makundi mawili ya kutetea haki za binadamu Amnesty International na Human Rights Watch yakionya juu ya mauaji ya kikabila katika baadhi ya maeneo ya nchi yanayolenga waislam walio wachache.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Wednesday, February 05, 2014

MTIBWA SUGAR KUWAKARIBISHA SIMBA UWANJA WA JAMHURI LEO MOROGORO

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16 leo (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi tano huku Mtibwa Sugar ikiikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kiingilio katika mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 tangu uanze mzunguko wa pili wa VPL kitakuwa sh. 5,000. Jonisia Rukyaa kutoka Bukoba ndiye atakayechezesha mechi hiyo.
Mechi nyingine za ligi hiyo ni Tanzania Prisons vs Coastal Union (Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na JKT Ruvu vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TANZANIA YAKAMATA DAWA ZA KULEVYA ZAIDI YA KILO 200

http://jambotz8.blogspot.com/
Polisi nchini Tanzania wamekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 201 katika eneo la bahari kati ya Dar es Salaam na Zanzibar nchini humo.
Kamanda wa kikosi maalum cha kuzuia dawa za kulevya Godfrey Nzowa ameiambia BBC kuwa Watu 12 wanashikiliwa kuhusiana na shehena hiyo.
Kamanda Nzowa amesema dawa hizo za kulevya zimekamatwa na Polisi wa doria baharini muda wa saa sita usiku wa kuamkia Jumanne zikisafirishwa katika Jahazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa Shehena hiyo ilikuwa ikitoka nchini Iran kuelekea nchi au eneo ambalo mpaka sasa bado halijafahamika.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kukamata dawa za kulevya aina mbalimbali kupitia viwanja vya ndege,nchi kavu na baharini, ambapo mwaka jana kiasi kikubwa cha dawa za kulevya zilizokamatwa ziliteketezwa.
CHANZO:BBC
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 


MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 05, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

NEC KUTANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA

malaba1 38164
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema wiki hii itatangaza tarehe ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga, lililopo wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wake, Dk William Mgimwa (CCM) kufariki dunia Januari Mosi mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Licha ya Kalenga, tume hiyo imesema uchaguzi mdogo pia utafanyika Jimbo la Chalinze baada ya Mbunge wake, Said Bwanamdogo (CCM) kufariki dunia Januari 22 mwaka huu.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema uchaguzi mdogo hauwezi kufanyika kama jimbo litakuwa wazi miezi 12 kabla ya Uchaguzi Mkuu.
"Wabunge hawa wamefariki dunia ikiwa imebaki miezi zaidi ya 12 kabla ya Uchaguzi Mkuu na kuvunjwa kwa Bunge, hilo
linamaanisha chaguzi zitafanyika na wiki hii NEC itatangaza tarehe ya uchaguzi jwa Kalenga," alisema Malaba.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

LIBYA YAHARIBU SILAHA ZA SUMU

libya1_43539.jpg
Libya imekamilisha uharibifu wa silaha za kemikali katika mpango ulioanza miaka tisa iliyopita chini ya uongozi wa aliyekuwa rais, Muammar Ghaddafi.
Tangazo hilo lilipitishwa katika mkutano wa wanahabari uliofanyika Jijini Tripoli na kuhudhuriwa na wajumbe wa kimataifa .
Ikisaidiwa na Marekani, Ujerumani, na Canada, Libya imeharibu shehena ya sumu ya mvuke pamoja na silaha nyengine zenye sumu.
Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Shirika la Silaha za kemikali zilizopigwa marufuku amepongeza Libya kwa kuchukua hatua hiyo muhimu.
Amesema kwamba hatua hiyo ni mfano mwema wa ushirikiano wa kimataifa ambao unaigwa na taifa la Syria kwa kiwango kikubwa.
Kwenye mkutano huo waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya ameeleza kwamba hatua hiyo ni ya kihistoria na ni mafanikio kutokana na ushirkiano na washirika wa kimataifa.
Mnamo mwaka wa 2004,Libya ilikuwa na takriban tani 13 za sumu ya mvuke.
Mrundiko huo wa kemikali hatari kwa sasa umeharibiwa.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Saturday, February 01, 2014

MWILI WA MTOTO ALBINO WAZIKWA NDANI YA NYUMBA SUMBAWANGA

Kamanda Jacob  Mwaruanda.
Mwili  wa mtoto wa kike  mwenye umri wa miaka minne mwenye ulemavu wa  ngozi (albinism)  umezikwa  ndani ya nyumba ya babu yake  mjini Sumbawanga katika mkoa wa Rukwa  badala  ya kuzikwa katika  shamba la wafu  la  Wakatoliki.Tukio  hilo la  maziko  ya  mtoto  huyo  licha  ya  kuwa  gumzo mjini hapa, pia  lilihudhuriwa  na  umati mkubwa  wa waombolezaji.  
Uamuzi  huo  unasadikiwa  na  wengi   kuwa ni  hofu  kuwa  endapo  mwili wake  ungezikwa  katika  shamba la wafu  upo uwezekano mabaki yake kufukuliwa na kunyofolewa  viungo  vyake na watu  wenye  imani za kishirikina.
Mwaka jana watu wawili wenye ulemavu  wa ngozi walishambuliwa na kunyofolewa mikono yao na  watu  wenye imani  za kishirikiana  ambao  wanadaiwa kuamini kuwa  viungo vya binadamu hao    vina  uwezo  mkubwa  wa kumtajirisha  mtu  kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa Kamanda  wa Polisi mkoani hapa, Jacob  Mwaruanda watuhumiwa  katika  visa  vyote viwili  walikamatwa na  mashauri yao yako  katika  hatua  mbalimbali  za kusikilizwa   mahakamani.
Baadhi  ya waombolezaji  walioshuhudia  maziko ya mtoto  huyo yaliyofanyika juzi saa kumi na moja jioni  walisikika  wakisema; "Tumefarijika  mwili  wa marehemu kusitiriwa  ndani ya  nyumba ya  babu yake  tulikuwa na hofu sana maana  kama  angezikwa  makaburini   baada ya  waombolezaji  kuupa  kisogo  shamba hilo la wafu  hakika ungefukuliwa."
Akizungumza na  mwandishi  wa habari hizi  hapo  msibani, mjomba  wa marehemu  aitwaye  God  Mwangamila ' Kizibo'  ambaye alikuwa akiishi na mtoto  huyo  kuwa  aliaga dunia  Januari 29,  nyumbani kwake mjini hapa kutokana na ugonjwa wa malaria.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 01, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

UWANJA WA AZAM COMPLEX WARUHUSIWA KUCHEZEWA MECHI ZA KIMATAIFA

chamazi_2
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindanoya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanzaunaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki  kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana Khaled Nassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote vinavyohitajika na CAF kuchezewa mashindano ya kimataifa hivyo kuanzia tarehe ya leo, uwanja huu unaruhusiwa “kuchezewa mechi za CAF
Bwana Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguziwake toka nchini Zimbabwe Bwana Wilfried Mukuna kuja kukagua uwanja huu. Bwana Mukuna aliwasilisha ripoti CAF iliyopelekea shirikisho hilo kutoa kibali kwa Azam FC na TFF kuruhusiwa kuutumia uwanja huu kwa mechi zinazoandaliwa na CAF
Uongozi wa Azam FC umetoa shukrani kwa mkaguzi wa CAF Bwana Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya Rais Jamal Malinzi, na uongozi wa CAF Cairo Misri hasa Bwana Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa uwazi na uweledi wa hali ya juu uliopelekea uwanja wetu kupata kibali cha kutumika kwenye michezo ya kimataifa.
Azam FC sasa imewatangazi wapenzi wake kuwa kuanzia msimu huu mechi zake za  CAF zitachezwa Azam Complex Chamazi.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...