Friday, December 06, 2013

HII NDIO SENTENSI YA KISWAHILI ALIYOIANDIKA NICK MINAJ INSTAGRAM KUHUSU KIFO CHA MZEE MANDELA


Kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kimewasikitisha watu wengi wakiwemo watu wa maarufu duniani kama rapper Nicki Minaj mwenye wafuasi zaidi ya milioni tatu na nusu kwenye instagram amevunja rekodi ya kuwa staa pekee wa dunia ambae ameandika yake ya moyoni na kuongezea maneno ya lugha ya Kiswahili.
1
2

HISTORIA YA KUSISIMUA YA NELSON MANDELA


JINA KAMILI: Nelson Rolihlahla Mandela
A.K.A: Mandela
MAJINA YA UTANI: Madiba, Black Pimpernel
MAHALI ALIKOZALIWA: Mveso, Transkei, South Africa
KAZI: Mwanaharakati, Kiongozi wa dunia
TAREHE YA KUZALIWA: Julai 18, 1918
TAREHE YA KUFA: DESEMBA 05, 2013
MAHALI ALIKOFIA: Johannesburg, South Africa
ELIMU: Taasisi ya Clarkebury, Chuo cha Wesleyan, Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg.
ASILI YAKE
Nelson Mandela, Mwanasiasa maarufu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi nchini mwake, ni mtoto wa Chifu wa kabila la Tembu, Chifu Henry Mandela. Mandela alizaliwa katika mji mdogo wa Transkei.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 6, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.

MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA, TANZANIA KUOMBOLEZA SIKU TATU

Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.


Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!




Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"


Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.


Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.


Alikuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.

Thursday, December 05, 2013

PAPA FRANCIS ADAIWA KUTOROKA VATICAN USIKU....!!!


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.

Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedha toka kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.


Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.


Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.


“Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda kufanya kazi hiyo,” alisema Padri Krajewski.

MECHI YA NANI MTANI JEMBE KUCHEZWA DESEMBA 21

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala na Mkurugezi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba wakioshela alama ya dole baada ya kutangaza Simba na Yanga kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe itakayochezwa Desemba 21 jijini Dar es salaam (Executive Solutions)

 Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba 21, 2013 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza MECHI YA NANI MTANI JEMBE (NANI MTANI JEMBE MATCH). 
Pambano hili  ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 05, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.



Wednesday, December 04, 2013

MAMBO YANAYOCHANGIA MUME KUTEMBEA NA HAUSIGELI...!!!


http://jambotz8.blogspot.com/
Ndugu zangu, malalamiko ya baadhi ya mabinti wanaofanya kazi za ndani ‘mahausigeli’ kuwazidi kete baadhi ya wanawake kwa kuwachukulia waume zao yamekuwa yakiripotiwa kila mara.
Si ajabu hata wewe unayesoma makala hii aidha umeshawahi kumsikia rafiki kama siyo jirani yako akikorofishana na hausigeli wake au kushuhudia hausigeli akifumaniwa na bosi wake.
Hakika ni matukio ya aibu sana. Inafika wakati unajiuliza inakuwaje mume anamtongoza na hatimaye kutembea na hausigeli wake? Ameshawishiwa na kitu gani au amekosa nini kwa mkewe mpaka anafikia uamuzi huo?
Kimsingi linapotokea tukio kama hili, wengi hujiuliza maswali mengi sana na majibu yake huwa ni magumu kupatikana. Hii ni kwa sababu ni jambo lisilotarajiwa kufanywa na mtu aliyestaarabika. Hata hivyo, tuna kila sababu ya kujua chanzo cha tatizo hili.
Nitajaribu kuzungumzia kipengele kimoja baada ya kingine kuhusiana na yapi yanayotajwa kuwasukuma baadhi ya wanaume kutembea na mahausigeli wao.
Wanawake wanajitakia
Ni jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na baadhi ya watu kuwa, inakuwaje hausigeli anapewa majukumu ya kumhudumia mume wakati mke yupo?

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 4, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
.

UN: KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI DRC

131123051035_china_stealth_drone_304x171_itcjdbynet_nocredit_9697c.jpg
Majeshi ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yameanza kutumia ndege zisizo na rubani kuchunguza harakati za waasi katika mipaka na Rwanda na Uganda.
Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa kutumia ndege za aina hiyo.
Ndege mbili za kwanza zilirushwa kutoka mji wa mashariki wa Goma ambao mwaka jana ulikaliwa kwa muda mfupi na waaasi wa kundi la M23.
Ndege mbili za kwanza zinaundwa na shirika la Italia la Selex ES.
Jeshi la Umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ndio kubwa kupita yote duniani na lilichangia kwa kiasi kikubwa mwezi uliopita ushindi dhidi ya waasi wa kundi la M23;lakini bado kuna makundi mengine kadhaa ya wanamgambo nchini humo.
Kikosi kipya kilichoimarishwa nguvu cha Umoja wa Mataifa kilitumia ndege za helikopta kulisaidia jeshi la Congo dhidi ya waasi hao wa M23.
Eneo tajiri la madini la mashariki mwa Congo limekumbwa na vita kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita lakini kushindwa kwa M23 kumeleta matumaini fulani ya kupatikana utulivu zaidi kwa eneo hilo.

DK MIGIRO APONGEZWA NA WENGI KWA KUTEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE

 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,

Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
 Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
 Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Tuesday, December 03, 2013

MBOWE, DK SLAA WAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA ARDHI YA MWANZA ...!!!




Mwanza, Tanzania. Gazeti la RAI leo katika ukurasa wake wa kwanza limeandika kwamba Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa amepigwa marufuku kukanyaga jijini Mwanza ambako chama hicho kimepanga kwenda kuwahutubia wananchi.

Mbali na kupigwa marufuku, viongozi wa Chadema wamepewa masharti ya kufanya kila linalowezekana kumrejesha madarakani aliekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka.



Viongozi wa Chadema wametakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku nne kuanzia jana.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari. 

WAATHIRIKA WA VVU MAKETE WASUSA KUNYWA DAWA ZA ARV


Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika kata ya Mbalatse wilaya ya Makete 
 Wakazi wa Mbalatse wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Makete akitoa hotuba yake

BOKO HARAM WASHAMBULIA NGOME YA JESHI

Wapiganaji wa Boko Haram

Wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia ngome ya Jeshi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa serikali wamesema.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mamia ya wapiganaji wameshambulia maeneo kadhaa katika mji wa Maiduguri kuanzia mapema asubuhi siku ya jumatatu.

Amri ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri. Na uwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.

Mwandishi wa habari wa BBC anasema shambulio hilo lililopangwa ni shambulio kubwa ambalo limerudisha nyumba juhudi za Jeshi la Nigeria.

Maelfu ya watu wameuwawa nchini Nigeria na wapiganaji hao tangu mwaka 2009 wakati Boko Haram walipoanza mashambulizi ya kutaka kusimika utawala unaoegemea sharia ya kiislamu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 03, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...