Wednesday, September 25, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 25, 2013

DSC 0027 aa995
DSC 0028 f54fc

KENYA YAOMBOLEZA KWA SIKU 3

zzzzzkenyatta_maombi_640x360_bbc_nocredit_06884.jpg
Kenya inaanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi.
Watu 67 wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa wanaungana na wale wa Kenya kujaribu kuondoa mili ambayo imenaswa kwenye vifusi vya jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka jana. Nia ni kujaribu pia kutambua uraia wa washambulizi hao.
Baraza la usalama wa kitaifa linatarajiwa kukutana leo kudadisi yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kigaidi.
Magaidi watato waliuawa katika shambulizi hilo lililodumu siku nne na kuwa washukiwa wengine 11 walikamatwa wakijaribu kuondoka nchini.
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatano , Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa alihisi uchungu mkubwa na kuwa Kenya imejeruhiwa vibaya,lakini alielezea matumaini kwa kuwa shambulizi limeisha na kusema kwamba waliohusika watakiona cha mtemakuni.

AL SHABAAB NI NANI...???

00 a9dd3
ULIMWENGU umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi. Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka 1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika mwezi wa Septemba.
La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa vikali na wapenda amani wote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya tafsiri ya vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).
Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia. Kwamba Al Shabaab inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi,
hata raia wake. Kunahitajika jitihada za pamoja kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea Nairobi kitadhibitiwa kwa njia zote, kisitokee tena.
Na hakika, aina hii ya ugaidi ni ngumu sana kudhibitika hatakama nchi ina jeshi kubwa na lenye vifaa vya kisasa. Inahitaji ushiriki wa raia wema katika kutoa taarifa za wahalifu hata kabla hawajafanya matendo yao maovu. Inahitaji pia maandalizi makini, ya kuwa na vikosi vilivyo tayari wakati wote kukabiliana na matukio kama haya.
Ni dhahiri, kuwa mbinu inazotumika kikundi cha kigaidi cha Al Shaabab ambacho maana hasa ya jina hilo ni ' Vijana', ni moja ya changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.

MANJI: YANGA SHWARI, HAKUNA MGAWANYIKO

Manji 21 55726
MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji amesema hakuna mgawanyiko ndani ya klabu hiyo na habari kwamba Seif Ahmed 'Magari' ametengwa ni uzushi, lakini habari za ndani kutoka kwenye klabu hiyo zinasema uongozi unaamini unahujumiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).



Kumekuwa na habari kwamba Seif Magari ameondolewa katika sehemu ya uongozi wa klabu na kwa sababu hiyo, hata swahiba wake, Abdallah Ahmed Bin Kleb ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, naye amejitoa pia.

"Hakuna mgawanyiko, hayo ni maneno tu, Seif yupo na Majjid (Suleiman) wote tupo nao. Na hatuna wasiwasi na ligi, Simba SC inaongoza inatuzidi pointi tano tu.
Tumefungwa na Azam FC kwa bahati mbaya, sisi ndio tulicheza mpira mzuri na kila mtu ameona,"alisema Manji.

Tuesday, September 24, 2013

BREAKING NEWZZZZZZZZZ....!!! MKUU WA WILAYA YA URAMBO BI. ANNA MAGOHA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Urambo Marehemu Bi.Anna Magoha enzi za uhai wake akiwajibika kazini 
****
Serikali ya rais Jakaya Kikwete imepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Urambo Bi. Anna Magoha kufariki dunia  akiwa Chang'ombe jijini Dar kufuatia maradhi yaliyokuwa yakimsibu.
Mkuu huyo wa wilaya Bi. Anna Magoha amefariki jioni ya leo akiwa njiani kukimbiza Hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Marehemu Anna Magoha ambaye alishawahi kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya na Rais Jakaya Kikwete mnamo mwaka 2006.

Marehemu alikuwa ni mkazi wa wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa.

VIKOSI VYA KENYA 'VIMEDHIBITI' WESTAGE

westgate 5472a
Hatimaye vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema vimelidhibiti jengo zima la Westgate mjini Nairobi, ikiwa ni zaidi ya siku tatu baada ya jengo hilo kuvamiwa na wanamgambo. (HM)


Milipuko ikifuatiwa na milio ya risasi imesikika kutoka ndani ya jengo hilo asubuhi ya leo huku duru zikisema kuwa vikosi vya usalama vinaelekea kukamilisha operesheni hiyo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, magaidi sita waliokuwa wamesalia wameuawa huku wengine watatu wakiuawa hapo jana.
Serikali imesema zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa katika shambulio hilo ambalo Al shabaab imekiri kulitekeleza.
Wizara ya mambo ya ndani imesema wanajeshi wanaendelea kulisaka jengo zima la Westgate kutoka orofa moja hadi nyengine kuhakikisha kwamba hakuna mateka aliyesalia
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje amesema kuwa wawili kati ya wanamgambo watatu waliofanya shambulii hilo ni raia wa Marekani pamoja na mwanamke muingereza.

OBAMA AIPONGEZA TANZANIA...!!!


Rais wa Marekani Barack Obama ametoa pongezi na sifa kwa Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi chache duniani ambazo zimetia saini mkataba wa Ushirikiano wa Serikali Zinazoendeshwa kwa Uwazi ambao unalenga kujenga na kuendeleza nafasi ya taasisi zisizokuwa za Kiserikali katika utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa Serikali.
Rais Obama ametoa pongezi hizo kwa Tanzania leo, Jumatatu, Septemba 23, 2013, wakati akizungumza katika mkutano maalum aliouandaa mwenyewe Rais Obama kuzungumzia nafasi za Serikali katika kuunga mkono na kuendeleza asasi na taasisi zisizokuwa za Kiserikali na kuzishirikisha zaidi katika kuboresha shughuli za utawala bora uliofanyika kwenye Hoteli ya Hilton, mjini New York, Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wachache duniani walioalikwa kushiriki mkutano huo maalum ambao pia ulishirikisha wawakilishi wa asasi zisizokuwa za Kiserikali 300.
Baadhi ya nchi nyingine za Afrika zilizoalikwa na kushiriki katika mkutano huo ni pamoja na Liberia, Ghana, Benin, Libya, Tunisia, Senegal, Afrika Kusini na Botswana.
Shabaha kuu ya mkutano huo wa saa moja ilikuwa ni kutafuta namna ya kuongeza kiwango cha kuungwa mkono kwa taasisi na asasi hizo na jinsi gani ya kuzilinda ili kuziwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Aidha, mkutano huo ulilenga kuzitaka Serikali ambazo zinaweka vikwazo kwenye utendaji wa asasi hizo kuondoa vikwazo hivyo haraka ambavyo vinahujumu utendaji kazi na mchango wa asasi hizo katika uendeshaji wa utawala bora.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 24, 2013

DSC 0016 5b08d
DSC 0017 4b107

WANAFUNZI 300 ELIMU YA JUU KUKOSA MIKOPO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa
Zaidi ya wanafunzi 300 wa elimu ya juu wa vyuo mbalimbali watakosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kutokana na kushindwa kujaza fomu za kuomba mikopo katika kipindi kilichowekwa.
Watakaokosa mikopo hiyo kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014 ni kuanzia mwaka wa pili na kuendelea, ambao hawakujaza fomu za kuonyesha taarifa zao mpya kwa bodi.
Wanafunzi hao walitakiwa kuwasilisha maombi ya kupewa mikopo kati ya Mei hadi Julai 30, mwaka huu.
Mkugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HELSB, Cosmas Mwaisobwa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi kuhusu utendaji wa kazi wa bodi hiyo.
Mwaisobwa alisema kwa kuwa wanafunzi hao hawakujaza fomu za kuomba mikopo, mwaka huu hawatapata fursa hiyo na kwamba kwa mujibu wa utaratibu wao, kila mwaka lazima mwanafunzi aombe.

SIMU ZA WATU MILIONI NANE KUFUNGIWA MWISHO WA MWEZI HUU


WATUMIAJI wa simu wapatao milioni nane wapo hatarini kufungiwa simu zao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, Tanzania Daima limebaini.
Tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeziandikia kampuni za simu waraka wa kuzitaka zianze kukata kodi mpya ya laini (simu card) mara moja kuanzia Julai 30, 2013.
Hatua hiyo inatokana na serikali kushindwa kufuta kodi hiyo ya sh 1,000 iliyopitishwa na Bunge kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete baada ya kukutana na wadau wa sekta ya mawasiliano.
Kwa maana hiyo kila anayemiliki laini moja ya simu atakatwa sh 3,000; anayemiliki laini mbili sh 6,000 na anayemiliki laini tatu sh 12,000, lengo ni kuhakikisha serikali inakusanya sh bilioni 178 zitakazopelekwa kwenye bajeti kuu ya serikali.
Watumiaji wa simu sasa watalazimika kulipia kodi hiyo ya miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba kwa wakati mmoja.
Bunge kupitia Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) lilitaka kuwapo kwa kodi hiyo ili kusaidia shughuli za bajeti ya Serikali Kuu.

MTANZANIA MMOJA AJERUHIWA KWENYE SHAMBULIO LA AL-SHABAAB JIJINI NAIROBI

 
UBALOZI wa Tanzania, nchini Kenya umesema raia wake moja alijeruhiwa juzi wakati wapiganaji wa Kikundi cha Al Shababu walipoteka jengo la Westgate mjini Nairobi. Taarifa iliyotumwa na Ubalozi wa Tanzania jana, ilimtaja raia huyo kuwa ni Vedastus Nsanzugwanko ambaye ni Meneja katika Taasisi ya Kimataifa ya Child Protection, inayofadhiliwa na Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni, (UNICEF).

Taarifa hiyo,ilisema Nsanzugwanko amejeruhiwa kwa risasi na magruneit katika miguu yake yote miwili na amelazwa hospitali ya Aga Khan.

“Anaendelea kupatiwa matibabu, huku hali yake inaendelea vizuri, hata hivyo ubalozi unaendelea kufuatilia kwa lengo la kupata taarifa zaidi endapo kutakuwapo na Watanzania wengine katika tukio hilo,

Majeruhi huyu bado yuko hospitali na hatujaweza kumpiga picha,” ilisema taarifa hiyo,”ilisema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Watanzania wanaoishi Kenya (TWA), umeandaa utaratibu maalumu utakaowezesha Watanzania waishio Kenya kujitokeza kwa ajili ya kutoa damu.

Wakati huo huo, Umoja wa Mabalozi wa Nchi za Afrika ulikutana na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa wakuu wa nchi zao. Taarifa zinasema wajumbe hao walikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kutoa

Monday, September 23, 2013

HUYU NDIYE MWANAMKE RAIA WA UINGEREZA ANAYETUHUMIWA KUIONGOZA AL-SHABAAB KUUA WATU NAIROBI

Mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi ya 175.

Tayari mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi hao walioshambulia Westgate.

Nayo akaunti ya Twitter ya American Jihad Watch ‏@watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on mall camera at Westgate Centre Shopping mall earlier yesterday may be infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.


Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo

Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.

Kwa mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.

ALIYEMJERUHI AUNT EZEKIEL KWA CHUPA ASOTESHWA KORTINI


Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.

Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya.

Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo.

Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.
Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.

Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.

P SQUARE WANATISHA AFRIKA

SQUARE1 89dc2
KUNA jambo moja ambalo mashabiki wa timu ya soka ya Arsenal wa Bongo wanajivunia kwa sasa. Unajua hao mashabiki wamefanya nini? Wamegeuza kibwagizo cha wimbo maarufu wa 'Personally' unaotamba kwa sasa wakaupa jina la 'Arsenally'.


Wimbo huo ni wa wakali wa muziki wa Afrika kwa sasa ambao ni Peter na Paul Okoye wa Nigeria. Kimuziki wakali hao wanajulikana kwa jina la P-Square.
Kwa sasa wamevunja rekodi ya kuwa wasanii ambao nyimbo zao hazijawahi kuachwa kupigwa kwenye majumba ya starehe tangu mwaka 2003 mpaka dakika hii unaposoma ukurasa huu.
Mwaka huo ndipo walipozindua albamu yao ya kwanza 'Last Night' ambayo ilitengenezwa na Timbuk Music Label.
Wasikilizaji wazuri wa muziki, watakumbuka kwamba tangu kutolewa kwa ngoma yao ya kwanza, kila mwaka wakali hao wanadondosha nyingine na mpaka sasa hawajawahi kupotea kwenye ramani.
Unaposoma makala haya, wimbo wao bora wa 'Alingo' unatesa na huku 'Personally' ukiendelea kupasua anga vilevile.

"NIKIRUDI TANAZANIA SITAKI MAPOKEZI KWASABABU WATANZANIA NI WANAFIKI"... AGNESS MASOGANGE

  Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.

Lakini hata hivyo kwa mujibu chanzo chetu toka kwa mtu wa karibu na familia yake,  Masogange  amesema  hatohitaji mapokezi yoyote pindi atakapowasili nchini kwa vile hao wanaopanga mapokezi ndio wanafiki wakubwa ambao walikuwa wanashangilia alipokuwa jela.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...