Saturday, September 14, 2013

IRENE UWOYA ATIWA MBARONI KWA WIZI WA SIMU ( AINA YA iPhone 5)

MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
 
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo  ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
 
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.

Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya.

MULUGO AMEAHIDI KITITA CHA SH. MILIONI MBILI IWAPO TIMU YA MBEYA CITY ITAISHINDA TIMU YA YANGA LEO JIJINI MBEYA

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya ameahidi kitita cha sh. milioni mbili iwapo timu ya Mbeya City itaishinda timu ya Yanga ya Jijini Dar es salaam.


Waziri Mulugo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya amesema atahakikisha kuwa kila timu itakayotia mguu mbeya inaondoka na kipigo cha magoli

WAMAREKANI WADAI KUGUNDUA CHANJO INAYOANGAMIZA UGONGWA WA UKIMWI

Washington. Wanasayansi nchini Marekani wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu.

Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limechapisha kwenye tovuti yake kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.

Likinukuu taarifa iliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa; Nature, lilimnukuu Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi vyote kwenye mwili wa nyani.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 14, 2013

DSC 0020 3186e
DSC 0021 4ba64

SAMAKI HATARI WAINGIZWA NCHINI....!!!

samaki_df55c.jpg
Afya za Watanzania ziko shakani kutokana na kuwapo kwa biashara ya kuingiza samaki kutoka nje ya nchi, wanaodaiwa kuharibika na kuuzwa katika la Soko la Feri jijini Dar es Salaam.
Samaki hao kutoka Yemen, Dubai, China na Japan, wanaoingizwa nchini wakiwa wameganda kwenye barafu, wengi huharibika muda mfupi baada ya barafu kuyeyuka au baada ya kununuliwa.
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa samaki hao huletwa nchini kutafutiwa soko baada ya kukaa kwenye majokofu kwa muda mrefu huko wanakotoka, kiasi cha kuelekea kuharibika.
Ili wasiharibike, samaki hao aina ya Marckerel hukaangwa hadi wakauke. Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanunuzi wake wakuu ni wafanyabiashara wa chakula wakiwamo wamiliki wa migahawa na Mama Lishe wanaofanya shughuli zao katika miji ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma.
Samaki hao wanauzwa kwa bei ya chini ambayo ni Sh38,000 kwa boksi lenye uzito wa kilo 15, ikilinganishwa na wanaovuliwa hapa nchini ambao bei yake ni Sh60,000, kwa uzito huohuo.
Inaelezwa kuwa samaki hao baadhi yake ni waleambao wamekwisha muda wake wa kutumika katika nchi hizo, hivyo kuingizwa nchini kutafutiwa soko.
Gazeti hili lilifika katika soko hilo kwa siku mbili na kushuhudia samaki hao wakiuzwa kwa wingi, huku wauzaji wakihimizwa wateja wao kuwahi kuwakaanga au kuwaweka kwenye jokofu.

YANGA WAPEWA SIKU 14 KUWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA 15.5m

nsajigwa faa6e
Yanga imepewa siku 14 kuanzia (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya sh. milioni 15.5.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.

Fedha hizo ni ada ya usajili ambayo klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao wakati ikiwasainisha mikataba. Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha walizokubaliana na kiasi hicho ndicho bado hakijalipwa. Nsajigwa anadai sh. milioni 9 wakati Mwasika ni sh. milioni 6.5. Chanzo: shaffihdauda

MUME AMSAMEHE MKEWE ALIYEPANGA KUMUUA....!!!


mke_3e033.jpg
Mwanamke mmoja mfanyabiashara mjini Nairobi, Kenya, ambaye alikiri kosa la kupanga njama ya kumuua mumewe, ameachiliwa na mahakama
Bi Faith Wairimu Maina, aliachiliwa huru baada ya mumewe kuitaka mahakama kufuta kesi yake kwani amemsamehe.
Bi Faith alikiri kuwa aliwakodi mamluki kumuangamiza mumewe. "Nataka kumsamehe kwa sababu ya watoto na familia yetu," mumewe Faith aliambia mahakama.

Mwanamke huyo alikiri makosa ya kupanga njama ya kutaka kumuua mumewe baada ya kukamatwa ingawa baadaye alibadili msimamo wake na kukanusha madai hayo na alitarajiwa kushtakiwa.

Polisi walitibua njama ya mwanamke huyo baada ya majasusi waliokuwa wanajidai kuwa mamluki kupokea malipo ya shilingi 40,000 kuitekeleza njama hiyo.

PADRI AMWAGIWA TINDIKALI ZANZABAR

padri_2e446.png
Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo Mwang'amba, alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia mtandao mjini Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu wasichana wawili wa kiingereza kushambuliwa.


Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.  Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

MAMA MANGWEA AJITOSA KUMTETEA MWANA FA.

Mama wa MwanaHip Hop aliyewahi kuaminika kuwa bingwa wa mitindo huru, Albert Mangwea aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, Denisia Costantine Mangwea ameibuka na kumtetea mwanamuziki wa kizazi kipya Hamis Mwin’juma ambaye anatuhumiwa kuahidi pesa kwa mama huyo na kuingia mitini.
Sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, linatokana na kitendo cha mwanamuziki huyo (MwanaFA) ambaye aliwahi kuahirisha onesho lake, baada ya kifo cha msanii mwenzake (Albert Mangwea), kutokuweka hadharani hitimisho la ahadi aliyoitoa kwa familia ya marehemu.
Tarehe 31 ya mwaka huu ilikuwa ni tarehe ya onesho la The Finest ambalo MwanaFA alikuwa akitimiza miaka 13 ya muziki wake, akawa na lengo pia na kuugeuza muziki wa Hip Hop uwe na sura ya kistaarabu na kibiashara pia ili kuuongezea aina ya mashabiki.
Siku moja kabla ya onesho, msiba wa Albert Mangwea ukatokea, na hapo ikamlazimu mwanamuziki huyo kuahirisha onesho lake, na kulisogeza wiki mbili mbele huku akiahidi asilimia 15 ya faida atakayopata, angeipeleka kwa familia ya Albert Mangwea.

Friday, September 13, 2013

VATICAN SASA KUJADILI KUHUSU UWEZEKANO WA MAPADRI WAKATOLIKI KUOA....!!!

Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin

. Suala la mapadri wa Kanisa Katoliki kuoa au la, limeibuka upya na tayari limeanza kuzua mijadala mikali duniani.

Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea.

Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.

ETO'O: 'NISHAWAHI KUAPA KUTOCHEZA KWENYE TIMU INAYOFUNDISHWA NA MOURINHO

josemourinhoandsamueletoo 275x1551 78310
Samuel Eto'o amefunguka na kusema kwamba aliwahi kuapa kutokuja kucheza chini ya kocha Jose Mourinho.
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alisema alikuwa na mahusiano yasiyoridhisha na na kocha wa kireno kabla ya hawajafanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan, mahala ambapo walishinda vikombe vitatu kwa msimu mmoja.
Eto'o ameungana tena na Mourinho wakati alipojiunga na Chelsea hivi karibuni akitokea klabu ya Anzhi Makhachkala kwa mkataba wa mwaka mmpja utaoisha wakati ujao wa kiangazi.  Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Huu ulikuwa uhamisho ambao Eto'o mwanzoni asingeweza kukubaliana nao.
"Kabla hatujakutana kule Inter, Jose na mimi hatukujuana vizuri kwa ukaribu, hivyo mahusiano yetu hayakuwa yakieleweka," alikaririwa Eto'o alipohojiwa na gazeti la The Sun.
"Nadhani nilisema huko nyuma kwamba nisingekuja kuichezea klabu inayofundishwa na Jose.
"Lakini mungu anajua zaidi. Alitaka kunionyesha sikuwa sahihi na leo hii Jose ni rafiki yangu mkubwa, pia ni kocha wangu kwa mara nyingine tena." Chanzo: Shaffihdauda

IPIGIE KURA BLOG YAKO YA JAMBO TZ ILI IWEZE KUSHINDA KATIKA TANZANIA BLOGS AWARDS

 
Upigaji kura umeanza (7/09/2013), blog hii imeshiriki kipengele cha The Best Newcomer Blog

Jinsi ya kuPiga kura, gonga/bofya/ click hayo maandishi yaliyoandikwa piga kura yako hapa, kisha chagua jambotz8.blogspot.com malizia na vote now.

 PIGA kura yako hapa..........!!! Jambo Tz

Ahsante Kwa Kutupigia Kura.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 13, 2013

DSC 0011 60970
DSC 0012 ebf41

RAIS KIKWETE AONGEZA VIONGOZI WANAOTAKIWA KUTANGAZA MALI ZAO

1_0ddb0.png
Waziri Mkuchika akizungumza kwenye katika Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari semina hiyo.
2_cd971.png
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akizungumza na washiriki wa Semina (hawao pichani).Kushoto kwake ni Waziri Mkuchika na Mwenyekiti wa Baraza la Sekretarieti Balozi Jaji Mstaafu Hamisi Msumi.

JWTZ LAKANUSHA TAARIFA ZILIZOENEA MITANDAONI KUHUSU WANAJESHI WAKE

 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepata habari kupitia mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji  na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini  na waliokuwa  likizo wameitwa kurudi kazini.
Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga mbele.

JWTZ  linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote.  Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake. 

Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye mitandao ya  ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na  ‘Twitter‘  (Twitter/ JWTZ).

Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji  na zisizo sahihi.  Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.

Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu utoaji wa taarifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...