Tuesday, September 03, 2013

WIMBO MPYA WA DIAMOND - NUMBER ONE


MWANAMKE ANASWA NA SARE ZA JWTZ....!!!


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Saida Mohamed (30), mkazi wa Mwasonga Kigamboni, akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 31, mwaka huu, katika eneo la Mwasonga, Kigamboni.

Alisema Saida alikamatwa na suruali saba, mashati saba ya kombati, kofia 10, shati mbili nyepesi, fulana mbili na kofia moja aina ya bareti, vyote vikiwa mali ya JWTZ.

Alisema mtuhumiwa huyo, alikuwa na begi moja la kuwekea nguo za jeshi, cheo kimoja cha Koplo na mikanda miwili ya kijeshi.

Alisema uchunguzi unaendelea juu ya mwanamke huyo ili kubaini sababu za kumiliki sare za jeshi, kabla ya kufikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, polisi wamemkamata Husein Mkondoa (25), mkazi wa Gongolamboto Mzambarauni, akiwa anaendesha pikipiki huku akiwa amevaa nguo za kiraia na kofia ngumu ya kijani yenye nembo ya Polisi.

VIDEO MPYA YA GK - BARAKA AU LAANA


MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 3, 2013

DSC 0008 e4878
DSC 0009 047f4

RWANDA YAONGEZA USHURU KWA MIZIGO IPITAYO BADARI YA DAR TU

paul kagame 2d247
NI dhahiri sasa biashara ya kupitisha mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, imekuwa moto, baada ya Serikali ya Rwanda kupandisha tozo ya ushuru kutoka dola za Marekani 152 hadi 500 ambazo ni sawa na Sh 800, 000 za Tanzania.
Hali hii inawezekana kwa namna moja au nyingine, imetokana na mzozo kati ya Rais Jakaya Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambao umepelekea wafanyabiashara wa Rwanda na Uganda kutishia kuacha kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam.


Itakumbukwa mzozo huo, umekuja baada ya Rais Kikwete kumshauri Rais Kagame akubali kukutana na waasi wanaoendelea na vita mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini ushauri huo unaonekana kupokelewa tofauti na Rais Kagame.
Siri ya kupandishwa kwa gharama hizo, imefichuka jana baada ya malori mengi ya wafanyabiashara wa Tanzania kukwama katika mpaka wa Rusumo mkoani Kagera.

Monday, September 02, 2013

FAMILIA: AFRIKA KUSINI YAKATALIA RIPOTI KIFO CHA NGWEA.....!!!


TAKRIBANI miezi miwili tangu alipofariki dunia mfalme wa freestyle wa Hiphop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ bado familia inalalama kuwa haijapokea ripoti ya kifo cha kijana wao.


Mama mzazi wa Ngwea, Denisia Mangweha (kulia) akiwa na aliyekuwa mchumba wa mwanaye aitwaye Misheily.
Habari za kiuchunguzi kutoka ndani ya familia zimeeleza kuwa ukiachilia mbali cheti cha kifo cha Ngwea walichopewa siku kadhaa baada ya mazishi ya mtoto wao, hawajawahi kuelezwa kwa kina juu ya kile kilichomsababishia mauti au hata mwenendo wa kesi au uchunguzi wa tukio hilo.
Ilidaiwa kuwa mara kadhaa familia hiyo ilikutana katika vikao vya ndani na kukubaliana kulifuatilia suala hilo katika Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar. Huko walikumbana na vizingiti kwa maelezo imekataliwa kutolewa nchini humo.
Ilisemekana kuwa ndugu hao walipokwenda mara ya mwisho ubalozini hapo waliambiwa waandike barua ya kuomba kujua kinachoendelea ikiwa ni pamoja na ishu ya kama kuna kesi katika tukio hilo.


Habari nyingine zilidai kuwa huenda ripoti hiyo ilikwama sehemu au uchunguzi haujakamilika.

GEORGE BUSH ATANGAZA KIFO CHA MANDELA....!!!


Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amejikuta ‘akiingia chaka’ kwa kutangaza ‘kifo’ cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ambaye bado yuko hai.
 
Kosa hilo limetokea jana asubuhi (September 1) kwa bahati mbaya baada ya msemaji wa rais huyo wa 41 wa Marekani kujichanganya kwa kutosoma vizuri habari inayomhusu Mandela kupitia Washington Post hivyo kumfanya Bush aandike ujumbe huu,

“Barbara and I mourn the passing of one of the greatest believers in freedom we have had the privilege to know. As President, I watched in wonder as Nelson Mandela had the remarkable capacity to forgive his jailers following 26 years of wrongful imprisonment — setting a powerful example of redemption and grace for us all. 
He was a man of tremendous moral courage, who changed the course of history in his country. Barbara and I had great respect for President Mandela, and send our condolences to his family and countrymen.”

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 2, 2013

DSC 0522 e0f47
DSC 0523 52ecd
DSC 0524 0ca06

NIMEPEWA MAJINA YA WABUNGE WAUZA DAWA ZA KULEVYA: WAMO CCM, CHADEMA

Khamisi_Kigwangala_e74fd.jpg
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, amesema amepokea majina ya wabunge, viongozi wa serikali na wafanyabiashara maarufu nchini ambao ni mapapa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Hata hivyo, Dk. Kigwangallah ambaye amepania kuwataja bungeni watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, amesema baada ya kukabidhiwa majina hayo kutoka kwa wananchi, anafanya uchunguzi na kupata ushahidi ili kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuwataja. Miongoni mwa majina ya wabunge aliyopewa wamo kutoka CCM na Chadema, na wafanyabiashara maarufu wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam.

"Nawashukru wananchi wamenipa ushirikiano hadi jana wamenikabidhi majina ya watu saba ambao ni wabunge wawili, kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali na wafanyabiashara wanne, ambao wote ni mapapa wauza unga na siyo madagaa," alisema Dk. Kingwangallah. 

Alisema katika kuhakikisha anatekeleza alichoahidi amemwandikia barua Spika wa Bunge kumuomba atoe maelezo kwa kuwataja majina vigogo wanaojihusisha na dawa za kulevya na kwamba bado anasubiri kujibiwa. Dk. Kigwangallah amekabidhiwa majina hayo siku chache tu baada Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), William Lukuvi, kulieleza Bunge kuwa kama serikali itaamua kutaja wanaojihusisha na biashara hiyo hakuna atakayesalimika ndani ya bunge kwa sababu pia wamo wabunge wanaotajwa.

MZEE MANDELA ATOKA HOSPITALI


nelson-mandela ba73e
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95), jana aliondolewa hospitali na kurejeshwa nyumbani ambako ataendelea na matibabu ya maradhi ya mapafu. Hata hivyo, taarifa ya Serikali ya Afrika Kusini imesema uamuzi huo hauna maana kwamba Mandela amepata nafuu kwa vile hali yake bado ni mbaya na wakati mwingine hudorora zaidi.
 

Taarifa hiyo imeongeza timu ya madaktari wa Mandela inaamini ataendelea kupata matibabu katika makazi yake mjini Houghton kwa kiwango sawa na anayopata akiwa hospitalini mjini Pretoria.

Tangazo hilo limekuja siku moja tu baada ya maofisa wa serikali kukanusha ripoti kuwa shujaa huyo wa taifa hilo, alisharuhusiwa.
Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel aliyekuwa amelazwa hospitali tangu Juni 8, mwaka huu anaheshimiwa duniani kwa kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa kibaguzi wa wazungu wachache na kuhubiri upatanisho na maridhiano na jamii za weupe pamoja na kufungwa miaka 27 jela.

"Timu ya madaktari imetuhakikishia kuwa Mandela atapokea matibabu kwa sawa na anachopata hospitalini mjini Pretoria atakapokuwa katika makazi yake ya Houghton," taarifa ya Ofisi ya Rais ilisema.
"Lakini ikibidi, atarejeshwa hospitali," taarifa hiyo ilisema na kuongeza kwamba inamtakia Mandela afya njema.

DAUDI MWANGOSI ATIMIZA MWAKA MMOJA TANGU KUUWAWA KWAKE MKOANI IRINGA.


Ndugu zangu,

HUWEZI kutawala miili ya watu ukaacha mioyo yao. Ndiyo, mjumbe hauawi, ni kauli ya hekima ya tangu enzi za wahenga wetu.

Leo ni mwaka mmoja tangu mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa,Daud Mwangosi kuawa.

Ilikuwa ni Jumapili ya Septemba 2, 2012. Hakika, siku ile  itabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mamilioni. Ni kwa kufikiwa na taarifa za kutisha za mauaji ya mwandishi wa habari. Haya yanaingia katika historia kuwa ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi wa habari kufanyika hadharani tangu nchi hii ipate Uhuru. Wengi watakuja kukumbuka walikuwa wapi na walifanya nini siku walipopata taarifa hizo za kutisha. Binafsi, taarifa ile ya mauaji ya Daud Mwangosi siku ile ya Jumapili ya huzuni kwa Taifa ilinikuta nikiwa Iringa Mjini. N umbali wa mwendo wa saa moja  kwa gari kufika eneo la tukio, Nyololo, Mufindi.


Jioni ile nilikuwa nikifundisha soka ya watoto. Mara baada ya kupata taarifa zile kwa simu,  nilisitisha mazoezi yale ya watoto. Nikawapa taarifa zile.  Nilipowaambia kuwa nimepata taarifa sasa hivi kuwa mwandishi wa habari ameuawa Mafinga, mtoto mmoja akaniangalia na kuniuliza; “ Kwanini?”

Ndiyo, swali la mtoto yule ndilo umma wa Watanzania unapaswa uendelee kujiuliza hata leo; KWA NINI?


Mwandishi wa habari ni mjumbe katika jamii. Anapokuwa akifanya kazi yake hapaswi kuwa na hofu ya kudhuriwa kwa kukusudia na waliopata mafunzo ya  kutumia silaha.  Ndivyo ilivyo kwa watumishi wa Msalaba Mwekundu, wanapokuwa kazini kwenye maeneo hata ya vita.

Sunday, September 01, 2013

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA,DIAMOND APOKONYWA PASSPORT...MASANJA MKANDAMIZAJI NAE ATAJWA.....!!!


Ni mwendelezo wa Sakata la unga ambalo sasa ni janga kwa taifa letu. Orodha zinaendelea kutoka na kuwekwa wazi huku bunge likivutana kuhusu sakata hlo. 
 
Tetesi za kutoka ndani zinasema msanii wa muziki Naseeb Abdul au Diamond ambaye alijitapa wazi mbele ya kamera za habari kuwa anamiliki ukwasi zaidi ya bilioni moja kwenye akaunti yake, nyumba 5 za thamani Kijitonyama na Mikocheni na anatumia simu 6 za thamani ambazo zipo hewani muda wote tayari amenyang'anywa hati yake ya kusafiria na baadhi ya simu zake katika mwendelezo wa uchunguzi juu yake unaofanywa na vyombo vya dola.
Msanii pia wa maigizo Masanja Mkandamizaji ambaye anadaiwa kumiliki mkwanja mrefu na nyumba za thamani kubwa mpaka magari naye tayari ametajwa kuhusika na sembe.

Episode inaendelea,tuungane katka vita hii.

SOURCE: JF

MCHUNGAJI ATOA SIRI ALIVYOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA....!!!

 Mchungaji Donald Mwakisambwe wa kanisa la Kipendekoste la Kiinjili Tanzania, kwenye ofisi za gazeti hili wakati akitoa ushuhuda wa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Kinara wa kimataifa wa kuuza madawa ya kulevya aliyezunguka sehemu mbalimbali duniani kuuza mihadarati, ameacha biashara hiyo na sasa anahubiri Injili kupiga vita dawa hizo. Kigogo huyo Mtanzania na mzaliwa wa Mbeya, ambaye sasa anajiita kiumbe kipya katika Kristo, ni Mchungaji Macdonald Mwakisambwe wa Kanisa la Kipentekoste la Kiinjili jijini Dar es Salaam. 
 
Akizungumza katika mahojiano maalumu na NIPASHE Jumamosi jana, Mwakisambwe alisema alianza biashara ya unga mwaka 1990 na kuifanya kwa miaka 10, akisafirisha dawa kwa maelfu ya wateja walioko Afrika, Asia, Ulaya na Amerika. Alisema katika kutimiza azma hiyo, alitumia pasi za kusafiria za mataifa mbalimbali zenye majina tofauti, zikimuonyesha kuwa ni raia wa Msumbiji, Tanzania, Kenya, Namibia, Afrika Kusini na Namibia.

MANDELA HAKUTOLEWA HOSPITALI....!!!

Serikali ya afrika Kusini imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba aliyekuwa kiongozi wa afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye amelazwa hospitali tangu mwezi wa Juni, kwamba alirejeshwa nyumbani Johannesburg Ijumaa usiku.

Taarifa ya serikali imesema kuwa Bwana Mandela bado yuko hospitali mjini Pretoria na kwamba bado mahtuti, lakini hali yake imetulia.

Kulazwa kwa muda mrefu kwa kiongozi huyo kumewatia wasiwasi raia wa taifa hilo na ulimwengu kwa jumla.

Mandela ambaye ana umri wa miaka 95, alikuwa Muafrika wa kwanza kuwa rais wa taifa la Afrika Kusini, na anaheshimiwa na wengi kama baba wa taifa.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 01, 2013

DSC 0522 a7487
DSC 0523 38a54
DSC 0524 3c0ac

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...