Monday, August 26, 2013

WANAUME WAWILI WAAMUA KUOA MWANAMKE MMOJA ILI KUEPUSHA UGOMVI WA KUMGOMBEA


Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda Wamesaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.


Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao anayeanza kwa kueleza kwa nini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.

Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na
mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.

Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.

Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wakotayari kumtolea mahari

MBWA AZIKWA NA MAELFU YA WATU......! APEWA HESHIMA ZOTE


dog hero

 
Unacho kiona katika picha hapo chini ni mazishi shujaa ambayo yalitolewa kwa mbwa. Jina la mbwa alikuwa akiitwa Zanjeer na yeye kuokoa maelfu ya maisha ya watu wakati wa milipuko Mumbai Serial Machi 1993. Yeye alikua na  kilo zaidi ya 3329 ya RDX kulipuka, detonatorer 600, mabomu 249 mkononi na raundi ya 6406 ya risasi kuishika kusudi watu wasilipuke.
Kusema kwaheri kwa Zanjeer baada ya yeye kupita, alizikwa kwa heshima kamili.

ANGALIA VIDEO YA MWANAFUNZI ALIYESHITAKIWA KWA KUIBA SADAKA....!!!


 
Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.

MSICHANA AMEJIKUTA AKIZOMEWA NA KUCHAPWA VIBOKO BAADA YA KUVAA NGUO FUPI...!!!


Msichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na   kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu wasamariawema kuingilia kati  na kutumia nguvu kubwa ili  kumwokoa na kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.

 Mwandishi wetu Halfani Lihundi  kutoka arusha alikuwapo katika sakata hilo na ametuma taarifa hii iliyosema,  watu walio shuhudia tukio hilo wamesema wamechukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.

Kwa upande wao wanawake waliyo msitili msichana huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.
Source ITV

AHUBIRI ZAIDI YA MASAA MATATU BILA WAUMINI...!!!

Mhubiri wa injili akitoa neno pembeni ni viti kwa ajili ya waumini japo hakuna aliyejitokeza.
...Akizidi kumwaga injili.
 ...Akielezea umuhimu wa kumtukuza bwana.

CHAZ BABA AFUNGA NDOA, ATINGA UKUMBI WA ‘TWANGA’ KUJINAFASI AKIWA PEKE YAKE


 Rehema akikubali kuolewa na Chaz.

 
Chaz akimvisha pete mkewe.

CCM KWAWAKA MOTO MMOJA ATIMULIWA UANACHAMA


Nape Moses Nnauye,

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-
1.   Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2.   Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3.   Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013

Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.

DILLISH TOKA NAMIBIA AIBUKA MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA 2013

 
Fainali za Big Brother zimefikia  tamati  usiku  huu  zikiwa  na  washiriki  watano  ambao  ni  Beverly, Melvin, Cleo, Elikem  na  Dillish.

Mshiriki  wa  kwanza  kutolewa  alikuwa  ni  Beverly  akifuatiwa  na  Melvin  huku  Elikem  akiwa  ni  mshiriki  wa  tatu  kutolewa..

Mchujo  huo  uliwafanya  Cleo  na  Dillish  waingie  katika  masaa  ya  fainali za  mwisho  ambapo  Cleo  alielemewa  na  kutolewa  huku  akimwacha  Dillish  akichekelea  $300,000  za  ushindi  wa  shindano  hilo....

Agalia  jinsi  kura  zilivyopigwa:
 Angola: Dillish
Botswana: Cleo
Ghana: Elikem
Kenya: Dillish
Ethiopia: Beverly
Malawi: Cleo
Namibia: Dillish
Nigeria: Melvin
South Africa: Cleo
Sierra Leone: Elikem
Tanzania: Dillish
Uganda: Dillish
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Elikem
Rest of Africa: Melvin
Total

Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.
 
Hongera sana Dillish

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AUGUST 26, 2013 YA UDAKU, MICHEZ0 NA HARD NEWS

DSC 0063 d67d6
DSC 0064 188c0

TANGAZO LA USAILI NAFASI ZA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA



TANGAZO                            TANGAZO                            TANGAZO                   TANGAZO
 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI – ACP ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE YA KUWA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 NA CHA SITA MWAKA 2013 NA KUCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI INAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA POLISI www.policeforce.go.tz.
MUHIMU.                                                                                                          
       i.            MWOMBAJI ANARUHUSIWA KUFANYA USAILI KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA USAILI KILICHO KARIBU NAE KULINGANA NA TAREHE ZINAVYOONYESHA KWENYE TANGAZO LA USAILI.
     ii.            KWA MKOA WA MBEYA NA IRINGA KITUO CHAO NI MBEYA NA USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 16/09/2013 HADI 19/9/2013 SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI KATIKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
  iii.            MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI AJE NA VYETI VYOTE VYA MASOMO(ACADEMIC CERTIFICATES),RESULTS SLIP(S) NA LEAVING CERTIFICATE(S), NAKALA HALISI YA CHETI CHA KUZALIWA(ORIGINAL BIRTH CERTIFICATE). HATI YA KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
  iv.            MWOMBAJI AWE NA NANMBA YA SIMU AMBAYO ITAMJULISHA ENDAPO ATAKUBALIWA.
     v.            KILA MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATAJIGHARAMIA USAFIRI, CHAKULA, NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
  NI MUHIMU SANA KILA MWOMBAJI KUZINGATIA MUDA WA KUANZA USAILI.

Saturday, August 24, 2013

KUWA WAKWANZA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD WIMBO WA MSANII MPYA WA HIP HOP CHATTA RYMES KUTOKA SHY TOWN

Ujio mpya katika mziki wa kizazi kipya katika miondoko ya hiphop.. Anaitwa ISSA ALLY  a.k.a CHATTA RYMES  ni kijana mdogo mwenye uwezo wa kushangaza katika mziki Anakuja na wimbo wake mpya  aliofanya na KING DIZZO unaitwa SEMA NAO ameufanyia katika Studio  za SHY TOWN REC pande za SHINYANGA Tz


Kwa muonekano ni mdogo lakini kiuandishi ni hatari sana na anaplan ndefu ya kuhakikisha mziki unaweza kumlipa na kumfanya aendeshe maisha yake kupitia mziki na hatimae kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi.


SUPORT YAKO NDIO ANAYOIHITAJI 



                   ARTIST: Chatta Rymes Ft King Dizzo

                   TRACK:Sema nao

                   STUDIO:Shy Town Recs

                   PRODUCER:Hance Q

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AUGUST 24, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

CHANZO CHA MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA HIKI HAPA


 Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka alipo wasili Msibani.



Mc wa Shughuli ya Mazishi alikua ni JB.



Friday, August 23, 2013

MADAM RITA: "NAY WA MITEGO HANA PESA ZA KUNILIPA HATA NIKIMFUNGULIA KESI"


                                        Madam Rita

 Mratibu wa shindano la Epic Bongo Star Search(EBSS) Rita Paulsen (Madam Rita ) ameshangazwa na taarifa zilizoenea katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ,kuhusiana na yeye kutaka kumfungulia mashtaka msanii Nay Wa Mitego ambaye anadaiwa kumchafua (defamation) katika wimbo wake mpya unaotamba sasa (Salamu Zao). Amesema hana mpango
wa kumfungulia mashitaka kwa kuwa hatakuwa na pesa za kumlipa kwa maana itakuwa kesi ya kumchafua na inaweza kumgharimu pesa nyingi.
.
Madam Rita ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha burudani cha The Strengo Saturday kinachorushwa na Radio Victoria fm kupitia 90.6 kilichopo Musoma, Mara. Ambapo mtangazaji wa kipindi hicho Patrick Derrick Mwankale alitaka kujua sababu kubwa ya EBSS kuhamishiwa katika kituo cha televisheni cha TBC1 ikitokea ITV na vipi kuhusiana na habari zilizopo za yeye (Madam Rita) kutaka kumfungulia Nay Wa Mitego kesi ya kumchafua .

JK AAPISHA MAKATIBU WAKUU NA NAIBU MAKATIBU WAKUU IKULU DAR ES SALAAM LEO

 Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi ya Sekretariate ya Baraza la Mawaziri ambako watumishi wake wawili wameteuliwa kuwa manaibu Makatibu wakuu, ambao ni Injinia Angelina Madete (kulia kwa Rais) na Mhe. Consolata Mgimba (kushoto kwa Rais) mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu hao na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...