Sunday, May 26, 2013

MULUGO NA WANAFUNZI WANAOMILIKI SIMU


NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema atafanya ziara katika shule zote za msingi na sekondari ili kuwabaini wanafunzi wanaotumia simu za mkononi shuleni.
Mulugo alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizindua mpango mkakati wa elimu ya haki za binadamu na kuongeza ataanzia Mkoa wa Dodoma na atakaowabaini atawanyang’anya na kuzichoma moto.
Alisema suala la utandawazi limechangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuharibika na kuwa na nidhamu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuwadharau walimu na wazazi.


Mulugo alisema kitendo cha wanafunzi kwenda na simu shuleni kimesababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili, ambapo pia kimechangiwa na baadhi ya wazazi kujifanya wanawapenda watoto wao: “Hivi sasa limekuwa ni jambo la kawaida kuwakuta wanafunzi wa ngazi zote wakiwa na simu shuleni. Mimi sikubaliani nalo, nimeamua nitafanya 
ziara shule moja baada ya nyingine nikimkagua mwanafunzi mmoja baada ya mwingine nikianzia na Mkoa wa Dodoma katika kipindi hiki cha Bunge. Ole wake mwanafunzi nitakayemkuta na simu nitamnyang’anya na kuichoma moto maana walimu wanawalea sana… halafu na mimi mniimbie ‘tunataka haki zetu’,” alisema Mulugo.

RAIS NKURUNZIZA WA BURUNDI AJA KUHUBIRI INJILI TANZANIA

Rais Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, anatarajiwa kuja nchini Agosti, kuhubiri Injili katika mkutano mkubwa wa Injili unaoandaliwa na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini (PCT), imefahamika.
Kwa mujibu wa Askofu Samson Mlawi aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki, tayari  Kamati ya  Maandalizi imefanya vikao kadhaa ambavyo pamoja na mambo mengine, kamati ndogo zimeundwa ili kurahisisha ujio wa Rais huyo.
Alisema, kwa kutambua umuhimu na uzito wa ujio huo katika shughuli hiyo ya kiroho, kamati imeweka mtandao wa mawasiliano kuhakikisha waumini wa madhehebu hayo kutoka mikoa mbalimbali wanahudhuria mkutano huo ambao bado unatafutiwa uwanja.
Askofu huyo alisema Rais Nkurunziza pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kuleta ujumbe wa amani na uvumilivu wa kidini hususan katika kipindi hiki cha mpito baina ya madhehebu ya Kikristo na Waislamu nchini.
“Mimi na wanakamati wenzangu, tunaamini Mungu atafanya kazi yake kupitia Rais kuhubiri Habari Njema kwa Watanzania kama ambavyo angehubiri mtu mwingine yeyote, lakini kutokana na nafasi yake ni matumaini yetu kwamba ujumbe huo utachukuliwa kwa uzito wa kipekee,” alisema.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Askofu, mwezi huo huo wa Agosti, Mwinjilisti wa Kimataifa wa Huduma ya Christ For All Nations (CFaN), Reinhard Bonkke anatarajiwa kuwasili nchini kwa ujumbe maalumu kwa waumini wa madhehebu ya Kikristo na  Taifa kwa ujumla.
 
Alisema, ujio wa wageni hao mashuhuri nchini, utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza shaka na wasiwasi kwa baadhi ya Wakristo ambao wako njia panda kuhusu masuala muhimu ya kiimani, ikiwa ni pamoja na suala la kuchinja.

WANASHERIA WAAPA KUWASHITAKI WASANII WA KUNDI LA ZE KOMEDY KWA KUPIGA PICHA ZA UTUPU...!!


Zile picha za kundi la Ze Komedy la linalorusha kipindi chake kupitia televisheni ya East Africa TV zinazowaonesha wasanii hao wakiwa na mabint ufukweni zimechukua sura mpya baada ya wanasheria  kuahidi kuzisaidia familia za wazaza wa mabint hao.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema" Nimeziona picha hizo kupitia mtandao wenu kweli imeniuma kama mzazi kwani huo ni unyanyasaji ambao haukubariki hata kidogo naziomba familia za mabint hao kuchukuwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kushtaki ili iwe fundisho kwa wasanii wengine wanaopenda kudhalilisha watu wengine kwa masrahi yao binafsi" Alisema Fortunatus Kasomfi ambae ni mtanzania anaeishi nchini Afrika Kusini

Aidha nae Hawamu Juma ambae ni mkazi wa Arusha maeneo ya Unga Limited ambae ni Mwanasheria maarufu Mkoani humo alioneshwa kusikitishwa sana na tukio na kuwashauri wazazi wa wasichana hao kumtafuta kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka wasanii hao
 
" Napenda kuwashauri wazazi wa wabinti hao kama wanahitaji msaada wa kisheria wanitafute kupitia  simu namba 0713-146416 nitawapa mawazo ya kitaalam ya kisheria ili wasanii hao wafikishwe mahakamani" Alisema Mwanasheria huyo.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 26, 2013

1 a2e01
8 67be7
4 30be2

MAPACHA WATANO WALIOZALIWA WAKATI MMOJA WAFARIKI DUNIA

 Mwalimu Sofia Mgaya akiwa amelala na watoto wake wote watano  kitandani baada ya kujifungua
...............................................................................
Na Nathan Mtega,Songea

 WATOTO watano waliozaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kwa wakati mmoja kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma wamefariki dunia baada ya kuishi hai kwa muda wa masaa kumi.
 Akizungumza kwa njia  ya simu mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Dkt Benedict Ngaiza alisema kuwa watoto hao watano ambao walizaliwa kwa njia ya upasuaji wakiwa na umri wa miezi nane tofauti na inavyotakiwa  umri wa mtoto kuzaliwa kuwa ni miezi tisa.

DIAMOND ATOA SIRI YA MUZIKI WAKE....!!!


Mengi yamekuwa yakisemwa juu ya msanii ambae inaaminika ndiye mfalme wa muziki wa bongo fleva Wapo wanaosema anatumia nguvu za giza ikiwemo ushirikina na wapo wanaosema yuko powered na Imani ya Free mason ingawa TEENTZ tunaamini juhudi na kujituma ndiyo njia pekee ya mafanikio kwa chochote TEENTZ ilipiga story na Diamond na kueleza moja ya sababu kubwa why yuko juu na  na kila siku ananendelea kuwa juu tofauti na baadhi ya wanamzki wengine


1-"Mungu ndio kila kitu kwa maisha ya binadamu,so napenda kumtanguliza Mungu kwa kila nikifanyacho"
2-"Sipendi starehe,kutumia pesa vibaya,naiheshimu sana pesa yangu,matumizi yake makubwa ni chakula,pengine mafuta kwa ajili ya gari matumizi mengine ya mhimu kwa binadamu na zaidi naitumia pesa yangu kufanya kitu kitakachoendelea kumantain muziki wangu"

3"-Sibani pesa kwenye swala la kujijenga kimziki,niko tayali nitumie milioni kadhaa kufanya kitu kitakachojenga status yangu vizuri,mfano kugharamikia mavazi ya shows n.k"

VIKONGWE WATATU WACHINJWA KAMA KUKU NA KUCHOMWA MOTO

Matukio kama haya ya watu kujichukulia sheria mikononi na kuwauwa wenzao kwa kuwachoma moto yamekithiri katika jamii na ndiyo yaliyosababisha ajuza watatu kuuwawa kikatili usiku wa kuamkia leo huko Bunda, Mara

MAUAJI ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja kama Kuku kisha kuwachoma moto ajuza watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha na vitendo vya kishirikina.
Pia watu hao mbali na kuwaua kikatili vibibi hivyo kwa tuhuma kwamba walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa wakiwafuga na kuatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa, tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua kijana huyo hivi karibuni.

Saturday, May 25, 2013

LADY JAY DEE NAYE AMSHANGAA MWANA FA. KUTOKANA NAYE KUANDAA SHOW TAREHE MOJA NA KUAMUA KUMCHUKUA LINNAH.

Kutokana na JIDE kuwa na show yake kubwa mnamo tarehe 31 mwezi huu pale nyumbani lounge ,Sasa rafikiye wa karibu sana MwanaFA inaonyesha naye ameanda show yake siku hiyohiyo  ya Tarehe 31,Zaidi ya yote mwana FA akawachukua  wasanii walio jitoa katika show ya JIDE kama Linnah  sa kutokana na sitofahamu hiyo mtandao huu wa thechoicetz uliweza kumtafuta JIDE kupitia twitter na kumuu liza juu ya hili swala naye aliweza kutoa yake anayo yafikiria,pia mtandao huu wa thechoicetz ulimtafuta  MwanaFA lakini mwanaFA hakuweza kutujibu swali tulilo muuliza hadi muda huu
 

Hivi ndivyo jide ALIVYO TUJIBU


MUONEKANO MPYA WA WEMA SEPETU HUU HAPA.....!!!


  
Huu ndio muonekano mpya wa bidada Wema, Vipi mzuri au mbaya? Comment

"MWANAMKE MCHAWI ADONDOKEA KANISANI AKIWA NA BIBLIA MKONONI, WAUMINI WAHAHA, YEYE MWENYEWE ANENA MAZITO "...!!

Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.


Tukio hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.

Baada ya Mahakama Kumruhusu Dr. Slaa Kuoa, Ridhiwani Kikwete Amponda Facebook







What is your Take ? Je ni kweli ni discussion ya Kidini ama ?

Picha za mwanasheria aliyebambwa akifanya ukahaba. Ashitaki mawakili kwa kusambaza picha zake za uchi


Mwanasheria mmoja wa Illinois ambaye alipatikana na hatia ya kufanya ngono na mwanaume mmoja kwa malipo ya Dola za Marekani 100 anamshitaki aliyekuwa wakili wake wa utetezi na mawakili wengine wawili kwa madai ya kusambaza picha zake za utupu.

Reema Bajaj, mwenye miaka 27, anasema wakili wake wa zamani Timothy Johnson, mwendesha mashitaka wa zamani Calvin Campbell, na mwanasheria aliyeorodheshwa kwenye hati ya mashitaka kama ‘John Doe’ walitoa hadharani picha zake za siri sambamba na taarifa kumhusu yeye.

Huyu Ndio Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania kwenye BBA “The Chase”

 
 

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye mitandao mbalimbali nchini Tanzania, mrembo huyu, mwanamuziki Feza Kessy, ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2013 (BBA “The Chase.” Well, hizi ni baadhi ya picha zake. Get familiar

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 25, 2013 HARD NEWS, UDAKU ,MICHEZO NA BURUDANI

.
.
.

MTOTO ALIYEZALIWA JELA AREJEA NA KUMTOA MAMA YAKE GEREZANI...!!!


 
Kanhaiya Kumari (kushoto) akiwa na mama yake, Vijaya mara baada ya kuachiwa huyu.

Mtoto mdogo wa kiume wa mwanamke ambaye amedhoofika  jela kwa takribani miaka 20 nchini India kwa upungufu wa Pauni za Uingereza 119 katika pesa za dhamana hatimaye amehakikisha kuachiliwa huru kwa mama yake. 


Kanhaiya Kumari, mwenye umri wa miaka 19, alizaliwa ndani ya gereza na Vijaya, mwenye miaka 48, ambaye alikamatwa mwaka 1993 kwa kuhusiana na kesi inayohusisha mauaji ya mmoja wa majirani zake katika wilaya ya Aligarh nchini India.


Alipatiwa dhamana mwaka 1994 lakini - ilitupwa na mumewe - hakuwa na uwezo wa kulipa Rupia 10,000 iliyokuwa ikihitajika kuhakikisha uhuru wake. Sasa ameungana tena na mtoto wake wa kiume, baada ya mtoto huyo kuwa amefanya kazi kupata pesa hizo za dhamana na kuishawishi Mahakama Kuu kwa ajili ya kuachiliwa mama yake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...