Wednesday, May 08, 2013

AUNTY LULU...... "NIMEAMUA KUACHA BIASHARA YA KUJIUZA.....NATAKA KUWA MJASIRIAMALI"



Siku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kunaswa kwenye mtego wa kujiuza, sasa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na mwingine mpya.

Katika ‘exclusive interview’ na paparazi wetu jijini Dar, juzikati, Aunty Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.
Alisema kuwa anawashukuru waandishi wa habari wa magazeti ya Global Publishers kwani wamebadilisha maisha yake, kama siyo wao angefikia hatua mbaya lakini kwa sasa ametulia na anafanya mambo ya maendeleo tofauti na zamani ambapo alikuwa hajielewi anafanya nini.

“Yaani kutokana na mtego wa kujiuza nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila siku lakini nikawa naukataa.
Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani.
Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la vipodozi na ni wakala wa kutoa na kuweka fedha kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi maeneo ya Kinondoni Kanisani, Dar ambapo ndipo anashinda kwa sasa na kwa mujibu wake  ameachana kabisa na kujiachia kwenye sehemu za starehe na kufanya mambo yasiyotakiwa katika jamii.

SIR ALEX FERGASON KUSTAFU MWISHO WA MSIMU HUU


Taarifa rasmi zinasema Kocha wa timu ya Manchester United Sir Alex Fergason Ameamua kustafu Mwisho wa Msimu, Tayari bodi ya timu hiyo imepokea taarifa toka kwa kocha huyo tayari kwa majadiliano ya kumtafuta mrithi wa kocha huyo aliyewapa mafanikio makubwa timu ya Manchester united kwa kipindi cha muda mrefu aliyokaa katika timu hiyo..

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 71 ataondoka mwisho wa msimu huu na mechi yake ya mwisho ataiongoza Manchester United Dhidi ya West Bromwich Albion tarehe 19 Mei .
Akiwa kocha wa Manchester united Sir Alex Fergason Ameipa timu hiyo jumla ya makombe 38 toka ameanza kuifundisha timu hiyo mwaka 1986.

KINANA AJIBU TUHUMA ZA MCHUNGAJI MSIGWA


Dodoma. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema anaamini chanzo cha kuchafuliwa kwake na wapinzani ni wadhifa wake.
Akizungumza na mwandishi wetu Dodoma jana, Kinana alisema anaamini kuwa kama asingekuwa na wadhifa huo, asingesakamwa kwa tuhuma alizoziita za uzushi.
Aprili 29, mwaka huu, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alimtuhumu Kinana kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na kudai kuwa meli iliyokuwa chini ya uwakala wa Kampuni Sharaf Shipping inayomilikiwa na Kinana ilikamatwa huko Vietnam na nyara hizo za Serikali.

“Hivi vitu havinisumbui. Hapa tatizo ni kuwa Katibu Mkuu wa CCM. ‘I am a senior officer’ (Ofisa Mwandamizi) sasa katika chama changu kama ningekuwa nimekaa nyumbani nafanya biashara zangu yasingetokea haya.
“Nataka kuwaambia tu, waelewe kuwa hawawezi kunitoa katika ajenda yangu ya msingi. Hii ni sawa na mwanajeshi anayekwenda kupigana vita na adui halafu akawa na vikundi vidogo vinakushambulia kutoka kila upande kukutoa katika lengo la msingi... ni lazima mtu ukomae na ili ufanikiwe,” alisema Kinana.

KADINAL PENGO ASISITIZA TENA KUWA ALIYERUSHA BOMU SI MUISLAMU.......KIKWETE AWATAKA WATU WAENDELEE KUSALI

Kadinali Pengo

“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:

“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.

MUSWADA WA KUZUIA MAANDAMANO NCHINI WAANDALIWA


Katika hali ya kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi aliliambia bunge jana  jioni  kwamba serikali  imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Waziri Nchimbi alisema kuwa  hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa....

Alisema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo. 

Huenda  azimio hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. 

Ikumbukwe ni hapo juzi  tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali  wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kudhibiti wapinzani kuiimarisha CCM.

HILI NDO NENO LA P-FUNK MAJANI KWA LADY JAYDEE KUHUSU BIFU LA JIDE NA CLOUDS

Producer mwenye historia kubwa na ya kipekee katika muziki wa Bongo Fleva P-Funk Majani ameonesha kumuunga mkono Lady JayDee na kwamba anadhani ni muda sasa wengine wakafuata nyayo zake, yeye mwenyewe majani amemhakikishia Jide kuwa yuko nae “Count Me in”.
Ameongeza kuwa endapo wasanii na watayarishaji wa muziki wakiungana hakuna kitakachowazua isipokuwa Mungu.

Hizi ni Tweet za P-Funk Majani za May 4:

@JideJaydee I think its really high time others follow in ur Footsteps!! Count Me in!

HIKI NDICHO ALICHOSEMA JACKLINE WOLPER BAADA YA MAGAZETI KUANDIKA KUWA AMETUPIWA ZAGA ZAKE NJE YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI


JESHI LA TANZANIA LIMESHATUA CONGO..... WAASI WA M23 WAANZA KUHAHA KWA KUJIKOSHA KWA WANANCHI


Kwa mujibu wa mwandishi aliye na waasi  wa  m23, Diana Katabarwa kwenye Blog yake  anamnukuu kiongozi wa kisiasa wa M23  Mr. Bisimwa akiwambia wakazi wa North Kivu kuwa majeshi ya Tanzania na South Africa nimajeshi dhalimu yaliyo jaa rushwa na hayawezi kuibadili Congo.... 

Bisimwa anadai  kwamba  majeshi  ya  Tanzania  yamekuja kuiba mali na kumsaidia KABILA awatawale   hali  itakayosababisha   jeshi lake la FDLR na waasi wa MAI MAI wapewa nafasi ya kuwa pora mali zao na kuwabaka wake zao na watoto....

Mbali  na  hayo,  bwana Busimwa anadai kinyume na taarifa zilivyo , kikosi cha jeshi la Tanzania kikiwa na askari 450 kimesha ingia mashariki ya CONGO kwenye mji wa UVIRA SOUTH KIVU huku Kamanda wao (TPDF) akiwa mjini Goma.  

Kikosi cha jeshi la SOUTH AFRICA kiko mita 20 kutoka waasi walipo kwenye mji wa MUNGI nje kidogo ya GOMA.  

Pia aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna makomandoo 30 wa jeshi la Ufaransa ambao wako mjini GOMA na  wamefikia Linda Hotel... 


BUSIMWA alidai wafaransa ndio walisimamia mauaji ya kimbari ya Rwanda ,kwa hiyo kuwepo kwao ni ishara mbaya kwa wakazi wa mashariki ya CONGO ambao wengi ni watusi

HUYU NDIO MUIGIZAJI ANGA'NGANIA WATOTO WA MICHAEL JACKSON, HUU NDO USHAHIDI ALIOTOA




MUIGIZAJI nyota kutoka nchini Uingereza, Mark Lester amesema anaendelea na taratibu za kuthibitisha kuwa watoto wa Michael Jackson ni wake.
Nyota huyo amesema anaendelea na taratibu za kupima vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kwamba Prince, Prince II, na Paris pia ni watoto wake.Hayo yalibainishwa katika gazeti la Mirror nchini Uingereza.
“Siwezi kufanya vipimo vya vinasaba kama sijapata kibali kutoka kwa watoto pindi watakapokuwa kiumri na si muda mrefu wataamua mimi kufanya hivyo, nami nitafanya," alisema Nyota huyo.

Lester, ambaye aling'ara katika wimbo wa Oliver alikuwa rafiki wa muda mrefu wa Michael Jackson kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Pia nyota huyo alisema, mwanadada Paris amefanana kwa kila kitu na binti yake, Olivia.

Tangu Lester aanze kutoa malalamiko yake hayo kwa mujibu wa Mirror, alisema familia ya Jackson imekata mawasiliano yote na yeye.

Kwa mujibu wa Mirror, Lester halizuiliwa kuwaona watoto tangu kifo cha Michael Jackson mwaka 2009.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL 8, 2013

1 c281d

2 108fd

Tuesday, May 07, 2013

SALAMA JABIR "AKINYONYWA ULIMI" NA NJEMBA HADHARANI......!!



Mambo  vipi jamani....

Katika  pitapita   zangu nimefanikiwa  kumnasa  live  Salama Jabir  akinyonyana  ndimi  bila  chenga  na  mwenzake...!!

Nashindwa  kuthibitisha  huyo  wa  pili  ni  nani  na  ni  jinsia  gani....nikimwangalia  haraka  haraka  naona  kama  ni  mwanaume  na  namfananisha  na  mdogo  wake    Wema   Sepetu  aitwaye  Bill Sepetu.....

Nikijaribu  kukaza  macho  kwa  kwa  makini,  huyo  wa  pili  namuona  kama  ni  mwanamke  kutokana  na vazi  lake.Hicho  cha  mabegani  nakifananisha   na  sidiria  za  akina  dada....!!

Yaani  nimeumiza  macho  mpaka  yanauma...Nashindwa  kuyaamini  macho  yangu  kuhusu  Salama Jabir. Sikutegemea..!!
Chanzo Gumzo la Jiji

KIKOSI CHA MIZINGA WAFUNIKA DAR CHID BENZI ADUNDWA NA PINA

 Mc mwenye VVU 
Nash Mc


 alifanya poa Usiku wa kikosi na mizinga 21


 Kala Pina



FBI WAFIKA ARUSHA KUCHUNGUZA TUKIO LA KIGAIDI LA KANISA KUPIGWA BOMU



MAJASUSI wa shirikisho la ujasusi la nchini Marekani wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini Tanzania katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa Vatican nchini siku ya jumapili.
Magesa alitoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipozuru eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali na kuwapa pole.

Wakati maafisa hao wakifika jijini humo tayari vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao wakiwemo watu wanne kutoka Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja kabla ya tukio.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa watu hao walikamatwa muda mfupi wakiondokanchini kupitia mpaka wa Namanga kuelekea nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi zitatolewa kadri muda na wakati utakavyoruhusu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 7, 2013

DSC 0007 83e8a

DSC 0006 a102d

FAHAMU KUHUSU DIAMOND PLATNUM KUBORONGA HUKO LONDON...... ADAM NDITI ANAYECHEZEA CHELSEA AMBWATUKA


Mtanzania ambaye kwa sasa ni raia wa Uingereza na anayechezea klabu ya Chelsea, Adam Nditi ameiponda show ya Diamond mjini Reading nchini humo na kudai ilikuwa ni aibu tupu.

adam na diamond 
“Diamond jana manyago aibu tupu waswahili lazima tubadilike it’s embarrassing,” ametweet.
  
“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa very unprofessional kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1 asubuhi.”
 
“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni alikuwa haimbi.”

Kwa sasa Diamond yupo ziarani nchini Uingereza.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...