Monday, May 06, 2013

SIRI NZITO YAFICHUKA NA YA YULE MFANYA BIASHARA ALIYE JIRUSHA GHOROFANI KARIAKOO!

NYUMA ya habari ya mfanyabiashara tajiri wa Kariakoo jijini, Costa Shirima (47), anayedaiwa kujirusha kutoka ghorofa ya tisa katika Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Mtaa wa Mchikichini, Dar es Salaam na kufariki dunia, kuna siri ambayo Ijumaa Wikienda limeelezwa.
Wananchi wakiwa eneo alipodondoka marehemu Costa Shirima.

Habari za kina kutoka hotelini hapo zilieleza kuwa Shirima alikuwa asafiri kwa ndege ya saa 10:00 jioni, Ijumaa iliyopita kuelekea nchini China kufuata bidhaa za maduka yake.

ALIMILIKI MADUKA KADHAA
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ulibaini kwamba Shirima ambaye alithibitishwa kufariki dunia baada ya kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar, alikuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na hoteli hiyo ya Concord.
Taarifa zaidi zilidai kuwa marehemu mara kwa mara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya hoteli hiyo kupunga upepo.
Ilidaiwa kuwa jamaa zake walipomhoji kulikoni kwenda kupunga upepo mchana wote huo, Shirima alisema kuwa alihisi hewa nzito mahali alipokuwa.

Mwili wa Costa Shirima baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya tisa katika Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Mtaa wa Mchikichini, jijini Dar.

MHUDUMU AFICHUA MANENO YA MWISHO
Madai zaidi yalishushwa na mhudumu mmoja wa hoteli hiyo aliyeomba hifadhi ya jina kuwa jamaa huyo alipoingia mahali hapo, alitaka kupatiwa chumba cha kupumzika lakini alipopelekwa kwenye vyumba vya ghorofa ya kwanza alikataa hadi alipofika ya tisa na kuanza kupunga upepo.

Mhudumu huyo alidai kuwa alikuwa akimsikia Shirima akiongea peke yake akisema “Haiwezekani… haiwezekani kabisa…” na baadaye alipokea simu ya kiganjani ambayo alisikika akibishana na mtu wa upande wa pili.

CHID BENZ AMBATIZA JINA JIPYA NEY WA MITEGO.... ASEMA SASA ATAITWA "NEEMA WA MITEGO"...!!

 
Ugomvi  wa  chini chini kati   ya Chid benz  na  Ney wa  mitego  sasa  umefikia  pabaya.....
Juzi  Ney wa mitego  alionja  kichapo  toka  kwa  mashabiki  katika  show  yake  mbagala....Inadaiwa  kwamba Varangati hilo   lilitokana  na  madai  yake  kwamba   Chid  benz  ni  shoga  na  ametoboa  pua  kama  dem.... 
Mapema mchana huu Chidi Benz amefunguka kupitia ukurasa wake ya Facebook   na  kumtaka  NEEMA  WA  MITEGO(Neema ni jina la  kike aache  kumtukana  wala  kumwandika  message  zozote.....Vinginevyo  ataendelea  kuambulia  kichapo
Hii ni post yake

JANUARY MAKAMBA NAYE AWAPONDA CLOUDS FM KWA KUGOMA KUPIGA "BONGO FLEVA " LEO....!


Huenda mjadala kuhusu uamuzi wa kituo cha radio cha Clouds FM, leo kutopiga Bongo Flava siku nzima haujalikuna sikio la naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Kupitia Twitter, Makamba ameandika kuwa Tanzania ina matatizo matatizo mengi ya kujadili kuliko nyimbo za kuchagua kucheza redioni. “We’ve got much bigger problems than radio playlists, ” ametweet.

Katika mahojiano maalum leo kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alidai kuwa ametoa amri leo kituo chake kisicheze Bongo Flava.

Uamuzi huo leo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Rais Kikwete akatiza ziara nchini Kuwait kurejea nyumbani kuwafariji waathirika wa mlipuko wa Bomu Arusha.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amelazimika kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika  eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Mei, 2013

RAY ‘ASINGIZIWA’ MTOTO WA BATULI.


 
KATIKA hali ya kushangaza, mashabiki wameibuka na kumsingizia mtoto wa mwigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ kuwa ni wa Vincent Kigosi ‘Ray’.
 
 
Vincent Kigosi ‘Ray’.
Ishu hiyo imetokea juzikati katika mtandao wa Facebook ambapo awali, Batuli aliposti picha inayomuonesha akiwa na mwanaye, ndipo shabiki mmoja alipozua mada kuwa mtoto ni wa Ray.
“Manga Msabaha nitake radhi mwanangu anafanana na Vincent Kigosi jamani? Hunitakii mema wewe…jamani sijazaa na Vincent Kigosi pls wadau huyo siyo mtoto wa Ray mshindwe,” aliandika Batuli.
Chanzo ni Global Publishers

MSANII MWINGINE AMUUNGA MKONO LADY JAYDEE KWENYE SAKATA LAKE LA RUGE NA KUSAGA

 
Mkali wa miondoko ya bongo fleva anatamba na ngoma yake kali aliyomshirikisha OMMY DIMPOZI  chukua tyme SUMA MNAZALETI ameyasema maneno hayo leo kwa njia ya masseji Alisema'' ebana nadhani unajua nini kinaendelea kuhusu lady jaydee! nachukua nafasi hii we kaka yangu ambaye umenisaidia sana kwa mda mrefu kukujulisha kuwa mdogo wako,Nitakuwa msanii miongoni mwa wasanii wanao support maneno ya lady jay dee Nakwambia haya kwasababu najua umenisaidia sana,but kama baada ya haya utaamua kuona sifai  sio tatizo pia! no interview 4 NOW  Nilikuwa nakupa habari  kama ndugu yangu wa karibu. lakini kama hili unaliunga mkono sio mbaya ukinijulisha kwamba hakuna tatizo na unaendelea kusaport kazi zangu. alimaliza kwakuandika jina lake suma mnazaleti.

Mwandishi wetu alinyanyua simu kutaka kujua zaidi juu ya sakata hili

mzazi kwanini umeamua kuchukua maamuzi hayo mazito?

Suma alisema ana sababu nyingi sana ambazo zimemfanya amuunge mkono lady jaydee kwenye mambo yake yanayomsibu sasa hivi na kubwa zaidi pia alizungumzia jinsi watu walivyomkatili kwenye tuzo za kili ambako kwenye academi alionekana kupata nafasi zaidi ya 3 kuwa nominies ikiwemo ya wimbo bora wakushirikiana lakini mwisho wa siku hakuingia hata sehemu moja, pili alilalamika kwakutopata airtime ya nyimbo zake kabisa katika kituo ambacho lady jaydee anarushiana nacho maneno na mengine mengi suma mnazaleti alifunguka.

LADY JAYDEE ASEMA''ILE ILIKUWA TRAILER MOVIE NDIO LINAANZA SASA"" TAREHE 15 AU 17 ATAFUNGUKA YA MOYONI

https://sphotos-a.xx.fbcdn.net/hphotos-prn1/p206x206/557919_10151342477575025_1251237535_n.jpg


CUF: SPIKA MAKINDA HAIFAI.

WADAI ANA UWEZO MDOGO WA KUONGOZA.
Mwenyekiti wa TAIFA wa Chama Cha Wananchi –CUF Profesa Ibrahim Lipumba.
Spika wa Bunge,Anne Makinda.

MWENYEKITI wa taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema Spika wa Bunge, Anna Makinda, ameshindwa kukiongoza chombo hicho kwa maslahi ya taifa, badala yake amegeuka kuwa kinara wa upendeleo kwa chama na serikali ya CCM.

Profesa Lipumba amemtaka Makinda atafakari na apime uwezo wake wa kiuongozi katika Bunge na afanye maamuzi magumu ya kubadilika kifikra kwa kuacha upendeleo anaoufanya kwa sasa.


Kauli hiyo aliitoa juzi jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujadili na kuchangia mawazo juu ya maendeleo kwa wote mkoa wa Mwanza, uliofanyika katika Hoteli ya JB Belmont.


Alisema Spika amejionyesha uwezo wake mdogo wa kuongoza Bunge na akubali kushau

riwa au kubadilika kifikra ili alinusuru Bunge lisiendelee kudharaulika ndani na nje ya nchi.

JACQUILINE WOLPER ATUPIWA VIRAGO VYAKE NJE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA.....!!

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kutupiwa nje na baadaye kuzuiliwa vyombo vyake kwenye ile nyumba ya kifahari ya kupanga aliyokuwa akiishi Mbezi Beach, Dar es salaam.

Madai hayo yalitua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu hiyo ilijiri maeneo hayo baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa kulipa kodi ya pango ya mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh. milioni 2.4 za madafu).
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyekuwepo eneo la tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake kwenda kuchukua vyombo hivyo lakini walipofika mama mwenye nyumba (jina tunalo), aliwazuia na kumpigia simu staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa kulipa fedha kabla ya kuchukua vitu vyake.



 

“Wolper alipopigiwa simu alikuja juu na kumwambia mama mwenye nyumba kuwa kama anamfuatilia eti atamfunga kama mume wa mama huyo alivyofungwa na kumwambia kuwa atampelekea polisi wakamkamate,” alidai mtu huyo.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kuona soo limekuwa la kutishana, mama huyo alikwenda kumfuata mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina moja la Musa na kumueleza kisha kumuomba asimamie zoezi hilo.
Baada ya kujazwa data hizo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumsaka Wolper na alipopatikana alisema kuwa hajawahi kudaiwa na huyo mama na anayesema hivyo huenda alimuona wakati anahamisha vitu vyake kwani kwa sasa amehama kwenye nyumba hiyo.
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja la Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba suala hilo lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya kufanya usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia.
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Musa alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia sakata hilo alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper.
Alisema kuwa msanii huyo alikuwa hajamaliza kulipa fedha, akawatuma ndugu zake wakachukue vitu vyake lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba aliwazuia mpaka alipwe chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu vyake.

BIFU LA JAYDEE NA CLOUDS SASA LAFIKIA PABAYA, RUGE AAMURU CLOUDS KUTOPIGWA NYIMBO YOYOTE YA BONGOFLEVA.......


 
Akizungumza kupitia kipindi cha Power Breakfast, Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameelezea yafuatayo kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na msanii Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ wiki iliyopita:
Asema vita ya Lady Jaydee ameielekeza sehemu isiyo sahii kama tatizo ni Bendi ya SkyLight basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine.
Awaasa wasanii kukubali kupokezana vijiti na kujiandaa kwa maisha yajayo
Aelezea Clouds ilipomtoa Jaydee mpaka sasa alipo. Aaamua siku ya leo kutopigwa muziki wa Bongo Flava
Asema kuwa Clouds ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria
Asema siyo vizuri watu kuchafuana katika mitandao ya kijamii, kama kuna tatizo ni vyema kuonana na muhusika ili kumaliza tatizo
Awaasa wasanii kukabiliana na changamoto na si kuziona kuwa ni tatizo

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 6, 2013


DSC 0001 62cc9
DSC 0002 e243a
DSC 0006 1d3df
DSC 0007 aa6d3

ANGALIA PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA

DSCN2227Hali ya eneo mlipuko ulipotokea

DSCN2220Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea

DSCN2228Ulinzi umeimarishwa

DSCN2252Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

DSCN2246Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio

Sunday, May 05, 2013

RPC ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU....WATU 3 WANAHALI MBAYA, 50 WAMEJERUHIWA...!!

Mkuu wa Mkoa Mulongo naye  amefika  eneo  la  tukio  na  kuwafariji  wahanga  wa  tukio  la  bomu....

RPC  wa  mkoa  wa  Arusha  naye  aliambatana  na  mkuu  wa  mkoa  na  muda  huu  alikuwa  anatoa  nasaha  zake  kwa  wananchi....

 
RPC  amesema  tukio  hili  ni  la kigaidi. Amesema kuwa  aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu. ...
Amesema kuwa Polisi wanawasaka waliohusika  na  unyama  huu  na  ameomba yeyote  mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..

Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida  na 3 wako  mahututi

Mpaka sasa  mtu mmoja anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaidi

"WAZIRI WA ELIMU AKAMATWE NA ASHITAKIWE"... MBATIA


Baada ya Serikali kutoa kauli kuhusu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka jana, Mbunge James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ametaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, awajibike na ikiwezekana akamatwe na kushitakiwa. 
Kauli hiyo aliitoa jana kwa waandishi wa habari akisema kuvurugika kwa utaratibu kutokana na kuanzisha utaratibu mpya wa usahihishaji na kutoa alama bila kushirikisha wadau, unamgusa Waziri ambaye ndiye mwenye dhamana. 
Alisema watu wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)  hawawezi kufanya uamuzi bila kujulikana na watu wengine wa juu akiwamo Waziri na kusababisha wanafunzi wengi kufeli mitihani ya kidato cha nne mwaka jana.
Aidha, Mbatia alisema kwa mantiki na falsafa ya utendaji haiwezekani utaratibu huo ukakosa baraka za Waziri wa Elimu.“Si kujiuzulu tu kuna watu wanatakiwa wakamatwe na kushitakiwa kwa kosa hili, kwa kuwa limefanyika kwa makusudi…limetengenezwa, halikutokea kwa bahati mbaya,” alisema.
Mbatia ambaye alifuatana na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema Dk Kawambwa alitakiwa kwa ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, asionekane hadharani kwa sababu ni aibu kwake.

MFANYA BIASHARA ALIYEJIRUSHA TOKA GOROFA YA TISA AFARIKI DUNIA

TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.
Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.
Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.
Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.
Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika

Mfanya biashara huyu mkazi wa Dar es salaam mzaliwa wa Moshi kilimanjaro alikutwa na mauti hayo baada ya kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya hoteli hiyo ambayo alienda kwa lengo la kuuona ukumbi wa tukio hilo ambao uko gorofa ya tisa ya hoteli hiyo.
Chanzo Cha Mfanyabiashara huyu kujirusha bado hakijafahamika mpaka sasa.
Taratibu za Mazishi ya Marehemu Zinapangwa jijini dar es salaam  na tukizipata tutakuhabarisha mapema. 
Ndugu Costa shirima ameacha mke na watoto.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mahali Pema Peponi 
Amina

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...