Monday, February 18, 2013

Stay away from the ear! Mike Tyson hugs Evander Holyfield… 15 years after BITING him during infamous fight.


Friends again: Former heavyweight champion Mike Tyson fellow former champion Evander Holyfield hugged in Chicago on Saturday.
Plenty of pals: They were also joined by Henry Tillman, heavyweight gold medalist at the 1984 Los Angeles Olympics.
Condiment fans: They teamed up at a promotional event for Holyfield’s Real Deal barbecue sauce inside a Jewel-Osco grocery store.
High spirits: Tyson smiled and waves to fans.
Here for business: The 46-year-old is in the city with his one-man show.
THAT fight: Evander Holyfield (L) and Mike Tyson (R) trade punches in 1997.
Ouch! Holyfield left with a chunk taken out of his ear.

TIGO Tanzania miongoni mwa Kampuni Bora zaidi Duniani yenye mahusiano ya karibu na wateja kwenye kurasa za Facebook.

Meneja wa Tigo Bw. William Mpinga akielezea jinsi kampuni ya Tigo ilivyoshinda nafasi ya nane duniani yenye mahusiano ya karibu na wateja wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Tigo Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa makampuni bora zaidi duniani yenye mahusiano ya karibu na wateja wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la SocialBokers tarehe 7 February, 2013  ambalo lilifanya utafiti wa makampuni 10 bora zaidi duniani yenye uhusiano wa karibu na wateja kwenye mitandao ya jamii kwenye kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka 2012. Tigo Tanzania ndiyo shirika pekee la simu kutoka kanda ya Kati, Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika lililofikia viwango hivyo vilivyojumuisha makampuni yote bora duniani.
Mitandao ya kijamii inajitokeza kuwa njia rahisi zaidi kwa wateja mbali mbali kupata taarifa, kuomba misaada na kuelimishwa  kuhusu bidhaa mbalimbali, na makampuni yaliyo na uhusiano bora na wateja wao na yenye uwezo mkubwa yamechukua fursa hii kuboresha  mahusiano na kuwa karibu na wateja wao.  Mitandao hii mikubwa ya kijamii duniani kama vile Facebook, hutoa njia m-badala na iliyo bora kwa mashirika yaliyozidiwa ki-huduma na hivyo kutoa fursa kwa watu wa tamaduni mbali mbali kushirikishana kujadili na kueleweshana.
” Tigo Tanzania imeibuka kuwa namba 8 duniani kote kwenye tafiti hizi kutokana na kujikita vilivyo kwenye kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora na za kujitosheleza kwa  wateja wake.Tunathamini sana wateja wetu na tunahakikisha kuwa tuko pamoja nao wakati wote kila wanapotuhijati. Maendeleo ya kiteknolojia na dijitali yamewezesha kuwepo kwa mijadala mingi kila wakati kwenye mitandao ya kijamii. Tigo kama  Kinara wa uvumbuzi wa bidhaa za  mawasiliano inatazama changamoto hii kama fursa ya kujiweka karibu zaidi na wateja na kushirikiana nao kwa ukaribu zaidi. Kila tunachofanya Tigo ni kwa ajili ya wateja wetu, hivyo  kutambuliwa huku ki-dunia ni fahari kubwa sana kwetu” alisema  Ndg. William Mpinga Manager brand ya Tigo.
Kwa mujibu wa shirika la SocialBoker, utafiti wa  mashirika yanayojituma zaidi kijamii kwa kipindi cha mwezi Oktoba na Desemba, 2012, umeonyesha kuwa mashirika  huwajibika na kujibu hoja kutoka kwa wateja wao haraka zaidi kwenye kurasa za Facebook. Hoja iliyokuwa inajibiwa kwa wastani wa   masaa 21 miezi ya nyuma sasa makampuni yanaweza kujibu kwa kipindi cha masaa 19.5 tu kuelekea mwishoni mwa 2012. Shirika la simu la Tigo Tanzania limepata asilimia 87.30% kwa kujibu hoja ndani ya masaa 28.
“Tigo Tanzania mbali ya kujibu hoja za wateja kwenye mitandao ya kijamii inahakikisha kuwa  inafanya hivyo kwa ufanisi zaidi kila wakati. Kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kutambua hilo tumefanikiwa kupata heshima hii kubwa. Tutazidi kuongeza ubunifu  ili kuboresha huduma na bidhaa zetu, na tunatambua kwamba, ili kutoa huduma stahili, ushiriki wa wateja wetu ni  nyenzo muhimu sana. Tumepata mafanikio makubwa tuliyonayo na kufika hapa tulipo leo kwa kuupa utoaji wa huduma bora kipaumbele, na
kwa heshima hii kubwa, tunaahidi kuwa tutajikita kuhakikisha tunaendelea kutoa ufumbuzi wa mawasiliano uliobora zaidi jambo litakalomfanya kila mteja wetu kutabasamu.” alihitimisha Ndg  Diego Gutierrez, Managa wa Tigo.
Socialboker ndilo shirika linaloongoza duniani miongoni mwa mashirika yanayofanya tafiti na kutoa takwimu kuhusu mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Google+, LinkedIn na You tube. Kwa njia hii inasaidia makampuni  uwezo wa kampeni za kijamii za makampuni yao. Tafiti za hivi karibuni zinajumuisha taarifa za Desemba 2012 za ‘Global Social Media Report’ ambapo utafiti mkubwa ulifanywa ukihusisha idadi ya kurasa za Facebook na watumiaji wake kidunia katika mataifa ya Marekani, Uingereza na Brazili. Mengine ni Azerbaijan, Serbia, Mexico, Poland na El Salvador- kwa kutaja machache.

Masoud Kipanya naye anautani mbaya, hebu cheka na hii hapa kwanza…

Sunday, February 17, 2013

NAPE AUNGURUMA GOBA KATIKA MKUTANO WA HADHARA LEO

Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimefanya mkutano wake wa hadhara katika Kata ya Goba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mkutano huo ambao ulijaza umati wa watu wakiwamo wanachama wa chama hicho ulihutubiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye.




RAIS KIKWETE AZIFARIJI FAMILIA ZA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA GARI UBENA ZOMOZI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kwa ajali ya gari maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua watu wanane papohapo, wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kwa ajali ya gari maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua watu wanane papohapo, wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
 Sehemu ya mabaki ya gari hilo lililopata ajali na kuua watu wanane.
  Sehemu ya mabaki ya magari hayo yaliyopata ajali na kuua watu wanane.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kwa ajali ya gari maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua watu wanane papohapo, wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.

MANCHESTER CITY WAIBUKIA KOMBE LA FA


Manchester City 4 Leeds 0

At the double: Sergio Aguero scored twice as Manchester City 
cruised into the sixth round
At the double: Sergio Aguero scored twice as Manchester City cruised into the sixth round
Three and easy: Carlos Tevez (left) celebrates with Sergio Aguero 
and David Silva after scoring Manchester City's third goal against Leeds
 United (below)
Three and easy: Carlos Tevez (left) celebrates with Sergio Aguero and David Silva after scoring Manchester City's third goal against Leeds United (below)
Carlos Tevez scores Man City's third goal
It was just the fillip manager Roberto Mancini needed, with City 12 points behind Manchester United in the title race and amid fresh speculation over his position.
Celebration: Sergio Aguero (left) and David Silva mark the second 
goal
Celebration: Sergio Aguero (left) and David Silva mark the second goal
Spot on: Sergio Aguero scores a textbook penalty to double City's 
lead after 15 minutes
Spot on: Sergio Aguero scores a textbook penalty to double City's lead after 15 minutes
Sergio Aguero scores a penalty
Under-fire Warnock also made a goalkeeping change, replacing Paddy Kenny with Jamie Ashdown, and brought back former Liverpool man El-Hadji Diouf, Rodolph Austin and Aidan White, but to no effect.
Early lead: Yaya Toure celebrates with his teammates Sergio Aguero,
 James Milner and Carlos Tevez after giving City a 1-0 lead on five 
minutes
Early lead: Yaya Toure celebrates with his teammates Sergio Aguero, James Milner and Carlos Tevez after giving City a 1-0 lead on five minutes
Composure: Yaya Toure rounds Leeds goalkeeper Jamie Ashdown to slot
 home Manchester City's first goal after five minutes
Composure: Yaya Toure rounds Leeds goalkeeper Jamie Ashdown to slot home Manchester City's first goal after five minutes
Aerial battle: Matija Nastasic (left) challenges Aidan White in the
 air
Aerial battle: Matija Nastasic (left) challenges Aidan White in the air
He's behind you! El-Hadji Diouf tries to rob Kolo Toure of the ball
 during the first-half
He's behind you! El-Hadji Diouf tries to rob Kolo Toure of the ball during the first-half
On the turn: James Milner tries to find a route past Leeds player 
Stephen Warnock
On the turn: James Milner tries to find a route past Leeds player Stephen Warnock
Nice to
 meet you! The FA Cup mascot makes the acquaintance of Man City manager 
Roberto Mancini
Nice to meet you! The FA Cup mascot makes the acquaintance of Man City manager Roberto Mancini

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MWAMINI MALEMI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA NYUZI ZA MKONGE CHA JESHI LA MAGEREZA, KIHONDA MKOANI MOROGORO.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (wa pili kutoka kushoto) akiangalia nyuzi za mkonge ambazo zimeanikwa kwa ajili ya kukaushwa maji kabla ya kuingizwa kiwandani kwa ajili ya kuzilainisha na kuzisafisha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja.
Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha majani ya mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) akizishika nyuzi za mkonge zilizokamilika ambazo zipo tayari kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) pamoja na wageni wengine wakionyeshwa pamoja na kufafanuliwa zaidi na Msimamizi wa kiwanda hicho Fidelis Muhaya jinsi inavyofanya kazi mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguzwa ukubwa.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na wageni waliotembelea kiwanda hicho wakiangalia mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguza ukubwa kabla ya kusafirishwa. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya kuuwawa kwa Padri Evaristitus Mushi


Padri Evaristitus Mushi

Padri Evaristitus Mushi wa KANISA la katoliki,Parokia ya ST.Joseph,Shangani,Unguja ameuwawa leo mnamo saa moja asubuhi katika eneo la Beit-EL-Ras karibu na kanisa la Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mohamed Aboud imeeleza kuwa kutokana na tukeo hilo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatambua wale wote waliohuka na tukio hilo kwa ajili ya kuwachukulia hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria.

Aboud amesema kuwa wakati uchunguzi huo unaendelra, Serikali inawaomba wananachi wote kuwa watulivu na kuliachia Jeshi hilo la Polisi kutekeleza wajibu wake .

Aidha Serikali imetoa mkono wa pole kwa familia na wanafamilia wa marehemu pamoja na waumini wa kanisa hilo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA FREEMAN MBOWE AONGEA NA VIONGOZI WA CHAMA KUTOKA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI

 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Freeman Mbowe akiwa anaongea na viongozi wa chama kutoka katika mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni arusha ,kilimanjaro ,manyara pamoja na tanga kuhusiana na sera ya majimbo leo jijini Arusha
 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Freeman Mbowe akiwasili katika ukumbi wa bugaloo kwa ajili ya kuongea na viongozi wa vyama mbambali kwa jili ya kupanga mkakati wa chama chao
 mwenyekiti wa  muda wa  chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kanda ya kaskazini ambaye pia ni mbunge wa karatu akiwakaribisha viongozi mbalimbali wa kanda ya kaskazini katika kikao cha viongozi wa chama hicho kanda  kikao ambacho kinajadili seraya majimbo
 picha juu na chini wajumbe ambao ni viongozi walioudhuria mkutano huo



KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA),Freeman Mbowe amesema kuwa mauji ya Viongozi wa dini ambayo yametokea,katika mkoa wa Geita, na Zanzibar ni matokeo ya CCM,na hivyo kama wataandelea kuendesha nchi kwa msingi hiyo bado nchi itakabiliwa na mauji makubwa sana

Mboye aliyasema hayo mapema leo wakati akizindua kanda ya kaskazini
kwa chama hicho ambayo itaweza kuhudumia mikoa ya kanda ya kaskazini
katika shuguli za kichama na za kijamii

Alisema kuwa hapo awali Chadema kilishasema kuwa CCM isipuuzie
matatizo ya ubaguaji wa dini lakini chama hicho hakikusikia na badala
yake kiliendelea kujiendesha kwa misingi ya kubaguana kidini hali
ambayo sasa inanyima watu uhuru wa kuabudu na kufanya mambo yao

Alisistiza kuwa kama CCM  bado iliendelea kufanya ubaguzo wa dini kwa
misingi kuwa inakomoa Chadema lakini hawakujua na kutambua kuwa hali
hiyo inafanya mauaji ya kila siku ambayo sasa yameanza Geita lakini
Leo yameelekea Zanzibar mara baada ya Padre kuuliwa wakati akielekea
Kanisani kusalisha misa

“Leo kila mahali unasikia mauji ya dini lakini mimi nilishawaambia CCM
kuwa hiii sio hali ya kuendelea kuangalia lakini walujua  kuwa ni
siasa na wao  walifanya hivi kwa malengo ya kuwa wanatukomoa sisi
Chadema kwa kugawa Taifa katika Imani ya kidini sasa wamelikoriga
wanatakiwa kulinywa’aliongeza Mbowe

Katika hatua Nyingine Mbowe alisema kuwa wao kama Chadema wanalaani
Mauji ambayo yanatokea kila siku ndani ya Tanzania na kwa hali hiyo
hawataweza kuwagawa wananchi  katika misingi ya kidini kwa kuwa wote
wapo sawa na kama Nchi itaendeshwa hivyo ni wazi kuwa damu ambazo
hazina hatia zitamwagika kila mara.

“Chadema tunaalani kwa kweli haya mauji na kwetu Muislamu, Mkristo
wote ni wa moja na kamwe kiongozi ambaye ataonesha ubaguzi dhidi ya
wakristo na waislamu ni wazi kuwa tutamkimbia hatuwezi kuingiza
jitiada za CCM ndani ya chama chetu,na kuweka utaratibu wa kumwaga
damu ambazo hazina hatia kabisa’aliongeza Mbowe

Akiongelea suala la kanda ya kaskazini ndani ya chama hicho alisema
kuwa hiyo ni moja ya mikakati ambayo imewekwa na mbali na hilo pia
kupitia viongozi wa kanda ya kaskazini wataweza kujiwekea nafasi nzuri
sana ya kuchukua Nchi ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2015 hivyo
kufanya Nchi iwe huru zaidi kuliko  ilivyo kwa sasa

Mbowe aliongeza kuwa kanda ya kaskazini pia itaweza kuwa chachu ya
Maendeleo kwa kuwa itaweza kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo
zinawakabili kwa kuwa sasa kazi za maendeleo zitafanywa chini ya mikoa
minnne tofauti na hapo awali ambapo kila mkoa ulikuwa unajitegemea kwa
shuguli za kichama na za kichama.

TAMKO LA RAIS KIKWETE KUHUSU MAUWAJI YA PADRI ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.

Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.

Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”

“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”

Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu

TARIFA MPYA KUHUSU KIFO CHA PADRI ZANZIBAR LEO


Taarifa  imeripoti kuwa Padre Mushi aliuawa na watu walipolisimamisha gari la Padre huyo alipokuwa akielekea katika kanisa la Mtakatifu Theresia lililoko eneo la Mtoni, na alipopunguza mwendo ili awasikilize, ndipo alipopigwa risasi kichwani na kusababisha gari alilokuwamo kukosa uelekeo na kuigonga nyumba iliyokuwa jirani. Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua Padre Mushi ili kumwahisha hospitalini katika jitihada za kuokoa uhai wake, lakini alifariki dunia. Waliomwua Padre Mushi bado hawajakamatwa.
-----------------------


Akina mama wakilia kwa uchungu kuomboleza kifo cha ghafla cha kupigwa risasi Padre Evaristus Mushi kilichotokea leo asubuhi muda mfupi kabla ya kuanza Misa ya Jumapili kwenye kanisa la Kigango cha Mtoni, Zanzibar. (Picha na Martin Kabemba via Lukwangule blog)

Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Miwili huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.


Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.


Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.


Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.


Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.


Wakizungumza kuhusu hilo, raia wamesema hawana imani na Polisi wala Madaktari na hawatarajii jipya zaidi ya ripoti kuwa suala hili ni la uhalifu kwa kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea mwishoni mwa mwaka jana kwa Padre Ambrose kupigwa risasi na taarifa zilisema lilikuwa ni tukio la kihalifu na kwamba risasi hazikutumika jambo ambalo halikuwa kweli kwani Padre Ambrose alikutikana na risasi alipohamishiwa katika hospitali ya Taifa, Muhimbili.


Kwa taarifa zaidi, tafadhali fuatilia vyombo mbalimbali vya habari.

SIMBA IMESHADUNGWA MSHALE 1-0 NA LIBOLO FC YA ANGOLA,

S5Mchezaji wa timu ya Simba ya Tanzania Shomari Kapombe kulia akichuana vikali na Maieco Antonio  mchezaji wa timu ya Libolo FC kutoka nchini Angola wakati wa mchezo wa  Klabu Bingwa  Afrika ( CAF) kati ya timu hizo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Libolo FC ya Angola inaongoza goli 1-0 dhidi ya Simba ya Tanzania ni kipindi cha pili na mpira bado unaendelea.
S1Waamuzi wa mchezo huo wakiwaongoza wachezaji wa timu ya Simba na Libolo ya Angola wakati timu hizo zikiingia uwanjani tayari kwa kumenyana katika mchezo huo.
S2Wachezaji wa Simba ya Tanzania na Libolo FC ya Angola wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
S3Mashabiki kwa mbali uwanjani hapo wakishuhudia nguo kuchanika wakati timu hizo zikimenyana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
S4Hizi siyo salakasi il ni harakati za kuwania mpira wakati wa mchezao wa Simba ya Tanzania na Libolo FC ya ambapo Libolo inaongoza goli 1-0  dhidi ya Simba ya Tanzania

TAARIFA YA INSPEKTA JENERALI WA POLISI SAID A. MWEMA KWA UMMA KUHUSU TUKIO LA KUUWAWA KWA PADRE EVARISTI MUSHI ZANZIBAR TAREHE 17 FEBRUARI, 2013


IJPMkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema akitoa taarifa ya jeshi hilo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo leo mchana.
Nimelazimika nizungumze nanyi kuhusu tukio la kuuwawa kwa Padre Evaristi Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar lililotokea leo asubuhi tarehe 17 Februari, 2013 eneo la Mtoni mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo watu wasiofahamika walimpiga risasi Padre huyo alipokuwa anaenda kusalisha ibada katika kanisa la Betras. Baada ya tukio hilo kutokea alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo baadae alifariki dunia. Tukio hili ni baya na la kusikitisha.
 2 Kufuatia kutokea kwa tukio hilo na kujirudiarudia kwa vitendo vya kuwashambulia na kuwadhuru viongozi wa dini na uchomaji wa nyumba za ibada, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumeanza uchunguzi wa kina wa kuwatafuta wanaohusika na matukio hayo.
 3Hivyo, nimetuma timu ya wataalam waliobobea kwenye masuala ya upelelezi na oparesheni kutoka Makao Makuu ya Polisi, kwenda kushirikiana na timu ya wataalam iliyoko Zanzibar. Hadi sasa watu watatu wananshikiliwa kwa mahojiano.
 Jeshi la Polisi limeimarisha doria maeneo yote hapa nchini na tunafuatilia mienendo na kuakamata watu wote wanaochochea, kufadhili, kuhamasisha na kushiriki katika vitendo vya uhalifu, vurugu na fujo.
 Tukiwa katika kipindi hiki, nawaomba wananchi wote hapa nchini kuwa watulivu wakati suala hili linaposhughulikiwa kuhakikisha kwamba wahalifu hao wanakamatwa na sheria inachukua mkondo wake.
 Naomba nitumie fursa hii pia, kuwasiliana na wananchi wenzangu wenye taarifa zitakazosaidia wahalifu hao kukamatwa kutupa ushirikiano kupitia namba zetu maalum za simu zifuatazo 0754785557 au 0782417247 na namba za makamanda wa mikoa na vikosi, ili kuhakikisha kwamba amani, usalama na utulivu vinadumishwa hapa nchini.
    Nawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano. 
AHSANTENI SANA.

BAADHI YA FAMILIA ZA KOSA MAHALI PA KUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUEZULIWA NA UPEPO MKALI





                 
BAADHI ya wakazi wa maeneo ya Mafisa mkoani hapa wamekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha leo jioni,


Mbali na kuezua nyumba hizo pia upepo huo uliangusha miti mirefu,taa za barabarani  na mabango marefu ya matangazo ya makampuni ya simu ya vodacom na tigo

Miongoni mwa mabango hayo ni bango kubwa la vodacom ambalo liliwekwa eneo la stendi ya mabasi ya Msamvu katikati ya geti kuu la kutokea mabasi eneo ambalo pia madereva wa boda boda huegesha pikipiki zao chini ya bango hilo.

" Ni mungu tu ametunusulu na kifo wakati bango hili linaanguka sisi tulikuwa hapa chini tukisubiri abiria kwa bahati tuliwahi kustuka,na kukimbia mwenzetu mmoja kwenye heka heka ya kukimbia aliiacha pikipiki yake ambayo aliangukiwa na bango hili na kuhalibika vibaya"alisema mmoja wa mabareva hao wa boda boda aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Samwel

Hii ni mara ya pili kwa bango la kampuni hizo kuanguka ambapo mara ya kwanza takribani miaka miwili iliyopita bango la tigo lililowekwa katikati ya stendi ya daladala lilianguka na kuharibu daladala mbili ambazo kwa bahati zilikuwa hazina watu ingawa zenyewe zilihalibika vibaya baada ya kuanguliwa na bango hilo.

Pia upepo huo uliovuma jana kutoka upande wa kaskazini ya mji wa Morogoro uliezua nyumba za watu na kuangusha miti mirefu ambapo  hadi mtandao huu unakwenda hewani takribani nyumba 15 ziliezuliwa mapaa hali iliyosababisha wakazi wa nyumba hizo kukosa mahali pa kuishi.

BREAKING NEWZZZ!!!!! PADRI APIGWA RISASI HADI KUFA ASUBUHI HII HUKO ZANZIBAR

Taarifa zilipatika sasa hivi ni kuwa Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Mirefu Zanzibar, Evarist Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi saa 1.00 asubuhi na kufariki kabla hajafika hospitali ya Minazi Mirefu. Paroko huyu amepigwa risasi akishuka katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00 leo.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano. 

Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.
R .I.P
SOURCE WAPO RADIO

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...