Monday, February 11, 2013

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka Kuzindua Kampeni ya Okoa Mtoto wa Kike Tanzania Machi 3 -2013

WAZIRI  wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Okoa Mtoto wa Kike Tanzania itakayofanyika baadaye mwezi ujao wilayani Tarime, Mara. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group inayoratibu kampeni hiyo, Mossy Magere.Na Mpigapicha Wetu
---- 
SERIKALI imeshauriwa kuangalia upya adhabu zinazotolewa kwa watu wanaofanya vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto nchini.

Ushauri huo umetokana na kuendelea kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji huku vyombo na mamlaka husika vikishindwa kutoa adhabu kali kwa lengo la kukomesha.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, aliyasema hayo mjini hapa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya Okoa Mtoto wa Kike Tanzania.

Kwa kuanzia kampeni hiyo itazinduliwa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, na baadaye kusambaa kwenye maeneo mbalimbali nchini hasa yaliyoshamiri kwa vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto.

Gaudentia, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, alisema licha ya kuwepo kwa sheria lakini bado vitendo vya unyanyasaji vimezidi kushika kasi, jambo linaloashiria kuwa adhabu zinazotolewa bado ni ndogo.

“Unyanyasaji umekuwa kwa kiwango kikubwa mno na umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya wanawake nchini. Sheria zipo na watu wanapewa adhabu, lakini tunadhani kuna kila sababu ya kuangaliwa upya ili kukomesha kabisa vitendo hivi,” alisema Gaudentia. Alisema zaidi ya moja ya tatu ya wanawake nchini wameshakabiliana na ukatili wa kijinsia na kwamba, mgawanyo wa unyanyasaji ni mkubwa zaidi kwa wanawake hasa waliotalikiwa na wajane. 

“Hili ni tatizo kubwa kwani, utafiti unaonyesha asilimia 23 ya wasichana wenye umri kati ya 15 hadi 19 tayari wamejifungua, hivyo kushindwa kuendelea na masomo kwa ajili ya kuajiandaa na maisha yao ya baadaye,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group (NMG), Mossy Magere, alisema kampeni hiyo itazinduliwa rasmi Machi 3, mwaka huu.

Alisema wameamua kushirikiana na Gaudentia kutokana na kuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake na kwamba, tatizo hilo la unyanyasaji limekuwa kubwa mkoani Mara.

Mossy alisema kampeni hiyo itakuwa endelevu na kwamba, itakwenda sambamba na uanzishwaji wa klabu za kupinga unyanyasaji katika shule mbalimbali kwa lengo kuleta usawa.

“Unyanyasaji wa kijinsia unaumiza wanawake na watoto wengi nchini, ni lazima jamii ikubali kubadilika ili kila mtu awe na furaja katika maisha badala ya wengine kufikia hatua ya kujuta kuzaliwa,” alisema Mossy.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete Afungua Semina Maalum Kwa Ajili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mjini Dodoma


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa White House uliopo katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.Rais Kikwete amefungua na kuongoza semina kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa ambayo pamoja na mambo mengine itachagua wajumbe wa Kamati kuu.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akielekeza jambo wakati wa ufunguzi wa Semina maalum kwa ajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa iliyofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa White House makao makuu leo.Kushoto anayesikiliza kwa makini ni Makamu  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM bara Pius Msekwa.Wengine katika picha ni Rais Wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(Wapili kushoto),Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana(wanne kushoto), na kulia ni Makamu Mwenyekiti CCm Bara Ndugu Philip Mangula.
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM taifa wakihudhuria semina maalum iliyofunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa White House,Makao makuu ya CCM mjini Dodoma.Picha na Freddy Maro-IKULU

Waziri Mkuu ashiriki mjadala kuhusu juhudi za Serikali ya Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa Malaria uliofanyika Afrika Kusini


Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anahojiwa na Mtangazaji wa habari za michezo wa Televisheni ya Super Sport Bi. Carol Tshabalala  katika mjadala kuhusu Tanzania inavyo jitahidi kupamabana na ugonjwa wa Malaria mjadala huo ulifanyika kwenye kituo cha mikutano cha Sandton kilichopo jijini Johannesburg Afrika Kusini.(picha na Chris Mfinanga).
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisaini mpira ikiwa ni ishara ya kupambana na Malaria kwakupitia michezo kutoka kulia Mama Tunu Pinda, kushoto kwake Meneja wa mpango wa kudhibiti malaria nchini Dr. Ally Mohamed, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr Seif Rashid  anayefuatia ni Mwana muziki marafu nnchini Afrika kusini na Balozi wa kupambana na ugonjwa wa malaria Bibi Yvonne Chakachaka, kushoto kwa waziri mkuu ni Mh Dr. Hamisi Kigwangalla (Mb) kulia. Waziri Mkuu alikuwa amehudhuria mjadala wa kupambana na Malaria uliofanyika katika kituo cha mikutano cha Sandton kilichopo Johannesburg Afrika Kusini.(Picha na Chris Mfinanga).
Mh Mama Tunu Pinda akisaini juu ya mpira ikiwa ni ishara ya kutumia michezo kupambana na Malaria. Kulia ni Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangaliatukio hilo na katikati ni Balozi wa kupamabana na Malaria na mwanamuziki marufu nchini Afrika kusini Yvonne Chakachaka. Mama Pinda aliongozana na waziri mkuu katika mjadala wa kupamabana na Malaria uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sandton Johannesburg Afrika Kusini.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...