Wednesday, March 27, 2013

RAIS KIKWETE AKAGUA MIRADI YA UZALISHAJI JKT RUVU

8E9U3121Mwakilishi wa Wabunge waliomaliza mafunzo maalumu ya muda mfupi ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)katika kambi ya RUVU Ester Bulaya akikabidhi risala kwa niaba ya wenzake kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana.8E9U3133Wabunge waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mris8E9U3151Wabunge waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho kikwete wakati wa gwaride maalumu la kumaliza mafunzo hayo huko kambi ya RUVU leo.8E9U3177Wabunge walihudhuria mafunzo ya muda mfupi Ruvu JKT wakionesha walijifunza kwa

Tuesday, March 26, 2013

SANAMU YA KANUMBA KUWEKWA BAGAMOYO, SOMA STORY HAPA

Steven-Kanumba
Of course Steven Kanumba had so much fans kwenye hii tasnia ya filamu za Bongo and he could defenetely take ‘Bongomovie’ somewhere far na ndio maana anakumbukwa kutokana na ku-inspire wengi.
Taarifa zisizokuwa rasmi kitaani kwasasa ni kwamba kwenye maazimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha the late steven kanumba mwaka huu huenda ikatengezwa sanamu yenye sura yake na kuwekwa kwenye mji wa kihistoria wa bagamoyo Mkoani Pwani.

Muigizaji Stevene Kanumba alifariki mwezi April mwaka jana 2012 nyumbani kwake Sinza Vatkan dar es salaam akiwa na umri wa miaka 28 baada ya majibizano na mpenzi wake Elizabeth Michael ‘lulu’ ambae pia ni muigizaji.

MCHORO WA KUMUUA ASKOFU MOKIWA


MCHORO uliosanifiwa na watu ambao inaaminika walitaka kumuua Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Dk. Valentino Mokiwa ni hatari.

 
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Dk. Valentino Mokiwa.
Taarifa za kila upande, zinathibitisha kwamba mchoro huo ulisanifiwa kitaalam na kwamba kilichomwokoa Mokiwa ni Mungu.
Imebainika kuwa kingine kilichonusuru maisha ya Mokiwa ni muundo wa nyumba yake, kwani baada ya majambazi kumshambulia kwa mapanga mlinzi wake, iliwawia vigumu kuifikia nyumba ambayo kiongozi huyo wa kiroho alikuwemo.

MCHORO WENYEWE
Uchunguzi unaonesha kwamba uvamizi nyumbani kwa Mokiwa, Mbezi kwa Yusuf, Dar es Salaam, Machi 9, mwaka huu haukuwa wa bahati mbaya kwani uliandaliwa mapema.
Pikipiki ambayo namba zake hazikunakiliwa, inatajwa kuhusika na upangaji wa uvamizi huo kwani siku ya tukio ilikaribia nyumba ya Mokiwa takriban mara tatu.

WANAFUNZI 10,000 WALIOKATA RUFAA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-2012 WAMEFELI TENA

Wakati tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi, imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa, wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa, wanafunzi waliokata rufaa NECTA kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni takribani 10,000 na kwamba baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa Machi 15, mwaka huu na kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi kadhaa kukata rufaa, NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo yote na kuanza kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa umakini, kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli kimeongezeka,” alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza hilo.

ABOMOLEWA NYUMBA NA KUCHOMEWA VYOMBO VYA NDANI AKIDHANIWA MSHIRIKINA ILEMI MBEYA

Wananchi wenye hasira kali wakibomoa nyumba ya mama Atupele Kalile akidhaniwa kuwa mchawi maeneo ya ilemi Mbeya
Wengine wameshaingia ndani na kuanza kutoa vyombo nje tayari kwa kuvichoma
Mtoto wa mama Atupele akijaribu kuokoa vitu vya mama yake visichomwe moto na wanakijiji
Vyombo vinazidi kutolewa ndani ilivichomwe moto
Wamefyeka shamba lake lote la mahindi
Wengine wanapongezana kwa kazi waliofanya
Kushoto mama Atupele Kalile anaedhaniwa kuwa ni mshirikina akiwa na mtoto wake
MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Atupele Kalile (60) mkazi wa Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya amenusurika kifo baada ya wananchi wa Mtaa huo kutaka kumpiga kisha kubomoa nyumba yake wakimtuhumu kwa ushirikina.
  
Wananchi hao kumtuhumu Mwanamke huyo kuhusika na upotevu wa motto mwenye umriwa miaka mitatu(3) (Judith Chengula) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Februai 22, Mwaka huu.
  
Kwa mujibu wa wakazi hao walisema Mtoto huyo alipotea majira ya saa 11 jioni baada ya kupoteana na dada yake  Anitha Mgaya wakiwa wametokea kanisani ambapo hadi sasa mototo huyo hakuweza kupatikana licha ya juhudi kubwa za wakazi hao kumtafuta bila Jitihada. 
Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa mtaani hapo kwa ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtotolakini Mwanamke huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu miongoni mwa wakazi hao hali iliyopelekea kuhisiwa kuhusika na tukio hilo.
  
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23 Mwaka huu majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea kusisitiza kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa motto ambapo iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.
  
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na kufanya upekuzi walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo Mwanamke huyo baada ya kuulizwa alishindwa kutolea ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na hasira na kuanza kumpiga.

WABUNGE ZITTO, AZAN WAMALIZA MAFUNZO YAO YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ LEO


Mbunge wa Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani Tanga.

Pichani juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake  Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.
Aidha Zitto Kabwe amesema anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya kubwa katika maisha yake hii leo. Anapasha zaidi katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama. NA FATHER KIDEVU

UAMSHO WASOMEWA KESI UPYA

Na Salma Said Zanzibar
KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na Mihadhara imeanza kusomwa upya jana katika mahakama Kuu ya Zanzibar.

Kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahmoud na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Bw. Ramadhan Nassib, ambae aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Farid Hadi (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47)
mkaazi wa Makadara na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini mkoa wa Mjini wa Magharibi Unguja.
Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Washitakiwa wote kwa pamoja walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kuharibu mali, Uchochezi, Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la ttatu ni kula njama ya kufanya kosa huku kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan Khalid ambae anadaiwa kufanya vitendo
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Makosa yote hayo yandaiawa kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti ambapo washitakiwa hao walipotakiwa kujibu tuhuma zao walizikana.
Mara baada ya kuwasomea mashtaka yao hayo Mwenesdha Mashtaka wa Serikali Bw. Nassib alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo tayari umeshakamilika lakini hata hivyo aliiomba mahakama hiyo kufanya subra ya kuweza kuamuwa maamuzi yoyote kutokana na upande huo wa mashtaka kukata rufaa kitendo ambacho alisema kwamba iwapo mahakama hiyo  itaendelea na kesi hiyo kunaweza mahakama ya rufaa ikatoa maamuzi ambayo yataweza kuathiri maamuzi ya mahakama hiyo.
Kwa upande wa mawakili wa watetezi uliokuwa ukiongozwa na Bw. Taufik Salum uliiomba mahakama hiyo kuwapatia dhamana washitakiwa wake haohasa ikiangaliwa kuwa tayari washitakiwa hao wameshakaa ndani kwa muda mrefu.
“Mhe Jaji tumefurahi kuona kwamba kwa mara ya kwanza upande wa mashtaka unatamka kuwa upelelezi umekamilika lakini isiwe sababu ya kuendelea kubakia rumande wateja wetu kwa vile muda wa kukaa kwako umekuwa mwingi na kupelekea haki yao ya msingi ya dhamana kunyimwa”,
alisema Bw. Salum.
Hata hivyo Jaji Mahmoud alisema kuwa atayachukuwa maombi ya pande yote mbili na kuyapitia kwa umakini ili baadae aweze kutoa maamuzi yaliyosahihi kutokana na kuwa ni mgeni wa kesi hiyo na jalada lake amelipokea kwa muda mchache ambao haukpata nafasi ya kuipitia.
“Nayachukuwa maombi yote mawili nitayatafakari kwa kina na kuja kutoa maamuzi unaofaa”, alisema.
Hata hivyo Jaji huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka huu.

HABARI KUHUSU KUVUNJIKA KWA KUNDI LA P. SQUARE...!!!

P-Square1-460x396
Kumekuwa na uvumi kuhusu wasanii wanaoliunda kundi la muziki la PSquare kutengana kiasi cha mashabiki wao kubaki wameduwaa.
Hata hivyo Peter na Paul Okoye wameweka wazi kuwa huwa wanaingia kwenye mitafaruku hadi kufikia hatua ya kupigana makonde huku kila mmoja akitishia kutengana lakini wakadai kwamba kama ni kutengana ambae angeweza kuwatenganisha ni mama yao pekee.

Wawili hao wamesema kuwa mama yao aliwalea na kuwaonyesha upendo na mapenzi na kama ingetokea kuwa siku moja itatokea PSquare watatengana basi yatakuwa ni maamuzi ya wazi na kama mmoja wao ataamua kustaafu muziki basi haimaanishi kuwa wataacha kusaidiana.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...