Wednesday, January 07, 2015

MAFUTA YAZIDI KUSHUKA BEI NCHINI




Bei ya mafuta ya petroli, dizeli na ya taa nchini inazidi kushuka kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia tangu Juni mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi alisema jana kuwa bei ya rejareja ya petroli kuanzia leo imeshuka kwa Sh74, dizeli kwa Sh62 na mafuta ya taa kwa Sh54.

Bei hizo zinashuka wakati kukiwa na mjadala mkali kuwa bei zilizopo sasa hazisadifu hali halisi ya kuporomoka kwa mafuta ghafi yanayouzwa kwa Dola 50 za Marekani kwa pipa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 07, 2015

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ZIARA YA MH. RIDHWANI KIKWETE JIMBONI KWAKE CHALINZE


 Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na kuwashuru kwa kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
 Mkazi wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
 Mkazi wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo kusababisha kukosa maendeleo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UTATA WAJITOKEZA KIFO CHA MESHACK YEBEI

William Ruto 

hali tata imezidi kujitokeza juu ya kifo cha Meshack Yebei, anayetajwa kuwa shahidi katika kesi inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Shahidi huyo alitarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC dhidi ya naibu Rais wa Kenya.
Lakini mwishoni mwa wiki mwili wa Yebei ambao ulionekana kuunguzwa kiasi ,ulikutwa umetupwa kando ya mto huko Eldoret Magharibi mwa nchi hiyo.
Familia ya Yebei wanashuku kwamba chanzo cha mauaji hayo ilikuwa ni kumzuia ndugu yao asiweze kutoa ushahidi wake katika mahakama ya ICC huko The Hague. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SHELL YAKUBALI KULIPA FIDIA NIGERIA

Kampuni ya Shell nchini Nigeria 
 
Kampuni kubwa ya mafuta ya Shell imekubali kulipa dola milioni 80 kama fidia.
Kampuni hiyo ya Uholanzi imewapa fidia wakazi wa jamii ya Bodo katika eneo la Niger Delta walioathiriwa na uvujaji wa mafuta.
Mawakili wa wavuvi 15,600 wa Nigeria wamesema wateja wao watapokea dola za Kimarekani 3,300 kila mmoja kutokana na hasara iliyosababishwa na uvujaji wa mafuta hayo.
"Kiasi kilichobaki cha dola milioni 30 zitatumika kwa ajili ya shughuli za jamii ya Bodo ambayo iliathirika vibaya kutokana na matukio mawili ya kuvuja mafuta mwaka 2008 na 2009".
Mawakili hao wamesema mafuta hayo yaliharibu maelfu ya hekta za mikoko kusini mwa Nigeria.
Fidia hiyo imesemekana kuwa kuwa kubwa kuwahi kuliko zote zilizowahi kulipwa nchini Nigeria, na hivyo kumaliza mvutano wa kisheria uliodumu kwa miaka mitatu. Wanaharakati wanasema kampuni ya Shell ililazimika kukiri kosa hilo mapema zaidi.
Matukio yote mawili ya kuvuja kwa mafuta yametokea katika bomba hilo hilo la Trans Niger Pipeline, linaloendeshwa na kampuni ya Shell, ambalo linachukua mafuta kutoka visima vyake(Shell) kwenda kituo cha mwisho cha kusafirisha mafuta hayo nje kilichopo pwani ya Bonny. Bomba hilo linasafirisha mapipa 180,000 ya mafuta kwa siku. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KASEJA, YANGA GIZA NENE

kaseja
IPO misemo mingi ambayo huashiria kutokea kwa jambo liwe nzuri au baya, moja ya misemo hiyo ni ule usemao dalili ya mvua ni mawingu.
Msemo huu unaweza ukawa na na maana kubwa hivi sasa kwa golikipa wa timu ya Dar es salaam Young African, Juma Kaseja ambaye hivi sasa inaonekana hana mawasiliano mazuri na uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar  es salaam.
Mchezaji huyo mwenye heshima kubwa nchini mwishoni mwa mwaka uliopita aliachwa katika kikosi cha timu hiyo kilichoelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya mapinduzi, lakini isitoshe jina la Kaseja halijaonekana kwenye orodha ya wachezaji wa timu hiyo iliyotumwa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa ajili ya ushiriki wa kombe la shirikisho.
Matukio hayo yote yameibua maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya mlinda mlango huyo, hatua iliyotufanya tumtafute afisa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro kutaka kufahamu kinaga ubaga kinachoendelea kati ya Kaseja na Yanga..
Muro amesema Kaseja kutohusishwa katika kikosi kilichopo Zanzibar na kilichotumwa CAF ni kujitakia mwenyewe.
http://jambotz8.blogspot.com/
Jerry Muro.  
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...