Tuesday, June 03, 2014

NIGERIA YAANIKA `BUNDUKI` ZA MWISHO KOMBE LA DUNIA BRAZIL

412895_heroaKOCHA mkuu wa Nigeria, Stephen Keshi ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mabingwa hao wa soka barani Afrika wanaenda kushiriki fainaili hizo kwa mara ya tano na wamepangwa kundi moja na Argentina, Iran na Bosnia.
Wachezaji wazoefu kama Vincent Enyeama, Austin Ejide, Joseph Yobo na Elderson Echiejile waliokuwa sehemu ya kikosi cha fainali za mwaka 2010 nchini Afrika kusini wamejumuishwa katika orodha hiyo ya mwisho. Mfungaji bora wa fainali za 29 za AFCON, Emmanuel Emenike, Godfrey Oboabona, John Obi Mikel na Victor Moses wanatarajia kucheza fainali zao za kwanza za kombe la dunia. Kikosi kizima: Walinda mlango: Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie Agbim
Walinzi: Joseph Yobo, Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Efe Ambrose, Kunle Odunlami Viungo: John Mikel Obi, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Michael Uchebo, Reuben Gabriel
Washambuliaji: Osaze Odemwingie, Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIA 130, 00 WA DRC WAFUKUZWA BRAZAVLLE

wakimbizi wa Congo wahangaika
Zaidi ya wakimbizi 130,000 kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wamefukuzwa kutoka Congo Brazaville tangu mwezi Aprili. Wengi wao sasa wanaishi katika kambi za muda nchini DRC.

Serikali ya Brazzaville imesema kuwa watu hao walikuwa wahamiaji haramu lakini wengi wao wamekanusha hili wakisema kuwa wameteswa sana na polisi wa Brazaville. Umoja wa maaifa umetoa wito kwa Congo kukoma kuwafukuza watu hao. Hapo Jumatatu ujumbe kutoka pande zote mbili ulikutana mjini Kinshasa nchini DRC kujaribu kutafuta suluhisho.
Maelfu ya waliohamia kambi hizo za muda za DRC waliishi nchini Brazaville maisha yao yote na sasa wamepoteza kila kitu walichokuwa nacho. Wamedai kuwa polisi wa Brazaville waliwapiga, kuwabaka na hata kuwaua baadhi ya watu walioaminiwa kuwa raia wa DRC wakati wa msako wao.

Huu ni unyama

Upande wa DRC umelalamikia hatua hii na kusema kuwa Brazaville imekiuka haki za binadamu.
Richard Muye ni waziri wa mambo ya ndani wa DRC. Ameambia BBC, '' Mbona sasa wanawafukuza tena kwa wingi hivi bila kujali haki zao? Wanawatesa watu wote, wake waume na hata watoto.''

Brazaville yajitetea

Lakini waziri mwenzake kutoka upande wa Brazaville Raymond Zéphirin Mboulou amekanusha kuwafukuza wakongomani 130,000. Amesisitiza kuwa ni 2000 pekee waliofukuzwa kwa lazima nchini humo, na hiyo pia ni kwasababu walikuwa wahalifu.
"Walifanya uhalifu wa kuchukiza. Wizi, ubakaji ukahaba na mengine. Wameharibu mitaa yetu. Na hawakaribishwi hapa tena kwasababu hao wahamiaji ndio wanaowahangaisha raia wetu usiku na mchana."
Waziri huyo ameongeza kuwa wale wengine 128,000 walioondoka walifanya hivyo kwa hiari yao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

NIGERIA YAKOMESHA 'BRING BACK OUR GIRLS'


Polisi wazuia maandamano Nigeria
Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamepiga marufuku maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya wasichana wa shule mia mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu la Boko Haram mwezi Aprili.
Maandamano yamekuwa yakiandaliwa kila siku kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kuishinikiza serikali kutia bidii zaidi katika juhudi za kuwakomboa wasichana hao. Polisi wanasema maandamano hayo yanamepigwa marufuku kwa kuwa yanazua hatari kwa wenyeji.

Aibu kwa serikali

Kampeini ya 'Bring back our Girls, au warudisheni wasichana wetu,'' ambayo imekuwa ikifanywa nchini Nigeria na hata nje ya Nchi hiyo imeleta aibu kubwa sana kwa serikali ya Nigeria.
Waandamanaji wamekuwa wakikutana hadharani wakiishinikiza serikali hiyo kukoma kuzungumza tu katika vyombo vya habari na badala yake waongeze jitihada na kuhakikisha wasichana hao wamekombolewa.

Makosa sio ya serikali

Lakini wiki iliyopita, kundi tofauti lilianzisha kampeini sambamba, na hata kuvuruga ile ilyokuwa ikiendelea ambapo wanadai kuwa hasira zinastahili kuelekezewa hao watekaji nyara na wala sio serikali ya Nigeria.
Kundi hili linatumia nembo 'Release Our Girls Boko Haram'. Wameongeza jina Boko Haram kwa kusudi hapo mwisho. Polisi sasa wanasema kuwa maandamano haya yanatishia usalama kwa wananchi wa Abuja.
Lakini waandamanaji wanaoendesha kampeini ya 'Bring Back our Girls' sasa wanaona kama hili ni jaribio la serikali kuwanyamazisha na wamewasilisha ombi mahakamani kutaka kutolewe agizo la kuvunja amri hiyo ili waruhusiwe kufanya maandamano yao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Sunday, June 01, 2014

GHANA YATANGAZA KIKOSI CHAKE KITAKACHOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA, GYAN KUONGOZA KIKOSI

414047_heroa 
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zinazoanza kushika kasi mwezi huu nchini Brazil.  
Kikosi hicho cha Appiah kinajumuisha wachezaji 16 wanaokwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza, huku nahodha Asamoah Gyan na Sulley Muntari wakiwa wakongwe wanaokwenda kucheza fainali zao za tatu mfululizo, wakati Jonathan Mensah, Michael Essien, Kwadwo Asamoah, Andre Ayew na Kevin-Prince Boateng wanakwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya pili.  
Kocha huyo mwenye miaka 53 amewaacha majeruhi Jerry Akaminko, Jeffrey Schlupp na David Accam katika kikosi hicho kinachoelekea Miami kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ambapo kitacheza mechi ya kirafiki juni 9 dhidi ya Korea kusini Akaminko alipata majeruhi jana jumamosi katika kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Uholanzi kwenye mechi ya kirafiki na atafanyiwa upasuaji utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa miezi mitatu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

GHANA YATANGAZA KIKOSI CHAKE KITAKACHOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA, GYAN KUONGOZA KIKOSI


414047_heroa 
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zinazoanza kushika kasi mwezi huu nchini Brazil.  
Kikosi hicho cha Appiah kinajumuisha wachezaji 16 wanaokwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza, huku nahodha Asamoah Gyan na Sulley Muntari wakiwa wakongwe wanaokwenda kucheza fainali zao za tatu mfululizo, wakati Jonathan Mensah, Michael Essien, Kwadwo Asamoah, Andre Ayew na Kevin-Prince Boateng wanakwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya pili.  
Kocha huyo mwenye miaka 53 amewaacha majeruhi Jerry Akaminko, Jeffrey Schlupp na David Accam katika kikosi hicho kinachoelekea Miami kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ambapo kitacheza mechi ya kirafiki juni 9 dhidi ya Korea kusini Akaminko alipata majeruhi jana jumamosi katika kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Uholanzi kwenye mechi ya kirafiki na atafanyiwa upasuaji utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa miezi mitatu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

TAIFA STARS YALAZIMISHA SARE YA 2 - 2 NA ZIMBABWE KATIKA MECHI YA MARUDIANO

DSC_457511 
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani.
Stars leo ilikuwa inacheza Zimbwabwe kwenye mchezo wa marudiano baada ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kulazimisha sare ya 2-2.
Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 28. 
Muda mchache baadae  Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa Tanzania wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

TANZIA: MAMA MZAZI WA MBUNGE ZITTO KABWE AFARIKI DUNIA

http://jambotz8.blogspot.com/ http://jambotz8.blogspot.com/Mama Mzazi wa Zitto enzi za uhai wake.
http://jambotz8.blogspot.com/ 
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGEREZA 12 TANZANIA HAYAFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU...!!!




Mahabusu 


Wakati mamilioni ya fedha za Watanzania yakipotea kila mwaka kutokana na ufisadi na misamaha ya kodi, imebainika kuwa baadhi ya magereza nchini hayafai kutumiwa na wafungwa kutokana na kukosa sifa ukiwemo uchakavu wa majengo.

Ripoti ya utafiti uliofanywa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwenye magereza na vituo vya polisi 102 katika mikoa 12, inaeleza kuwa magereza 12 hayafai kutumiwa na binadamu.

Hali hiyo inaamanisha kwamba magereza hayo siyo tu ni hatari kwa wafungwa na mahabusu, bali pia kiwa watumishi wa Idara ya Magereza. Ripoti hiyo inaweka bayana kuwa magereza hayo yana hali mbaya kutokana na majengo yake kujengwa miaka mingi iliyopita, huku mengine yakikabiliwa na ukosefu wa mwanga wa kutosha.

Magereza yaliyotajwa kukosa sifa za kutumiwa na binadamu ni Rombo, Nzega, Geita, Ngudu, Kasungamile, Ukerewe, Mugumu, Musoma, Bunda, Ushora, Mang’ola na Bariadi.

“Hali kwenye haya magereza ni kinyume na Kanuni namba 10 ya Umoja wa Mataifa, inayozungumzia namna ya kuwahifadhi wafungwa ambayo inataka sehemu za kulala zikidhi vigezo vya kiafya, hali ya hewa, nafasi ya kutosha, joto na mwanga wa kutosha,” inasema sehemu ya ripoti hiyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

'JK VUA KOTI LA CCM, VAA LA UARAIS'




Mwenyekiti wa Kongamano la Katiba, Dk Ayub Rioba akizungumza na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mdahalo ulioandaliwa na Muungano wa Asasi za Kiraia (Azaki) uliofanyika Dar es Salaaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa utetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa na Awadhi Ally Saidi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya kukusanya maoni. Picha na Venance Nestory      

Dar es Salaam/Mwanza. Rais Jakaya Kikwete ameshauriwa kunusuru mchakato wa kupata Katiba Mpya ili usisimame kwa kuvua koti la Uenyekiti wa CCM na kubaki na Urais ili awaeleze wananchi nini cha kufanya kupata Katiba Mpya.
Ushauri huo umetolewa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na wasomi walioshiriki katika mdahalo wa Katiba uliofanyika jijini Dar es Salaam na Mwanza jana. Walisema kuwa Rais ana wajibu kuunusuru mchakato huo kwa kuwa yeye ndiye aliyeuvuruga kwa hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge Maalumu la Katiba iliyoonekana kuelemea upande wa chama chake CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete amekuwa kigeugeu juu ya Muundo wa Serikali za Muungano kama zilizopendekezwa kwenye Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba.
Alisema kuwa Rais Kikwete alionyesha wazi kukubaliana na Muundo wa Serikali tatu, kwani kabla Rasimu ya Pili ya Katiba haijapelekwa kwenye Bunge Malaumu la Katiba ili kujadiliwa, alisaini kuonyesha kuwa amekubaliana na yaliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 01, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

NDOTO ZA LUIS MONTES KUCHEZA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA ZAZIMA GHAFLA

Clash: Luis Montes came off worse than Segundo Castillo when the pair went for a 50-50 ball
Agony: It left Montes in severe pain as his team-mates urged the club doctor to come to his attention
 Mchezaji mwenzake akimuita daktari wa timu baada ya Montes kupata majeruhi kubwa
Worried: Montes' Mexican team-mates look on as their midfielder is lifted on to a stretcher
 Wasiwasi: Wachezaji wenzake wakimtazama Montes anapobebwa na machela.
NDOTO za Luis Montes kuichezea Mexico katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil zimezima ghafla kufuatia kuvunjika mguu jana usiku kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador.
Nyota huyo mwenye miaka 28 alishuhudia timu yake ikishinda mabao 3-1 na yeye akifunga bao dakika ya 33, lakini dakika mbili baadaye alipata majeruhi mbaya.
Montes alibebwa na machela kutoka nje ya uwanja baada ya kugongana na mchezaji wa Ecuador,  Segundo Castillo, na kumuacha kocha wake Miguel Herrera akikiri wazi kuwa timu umwombee mchezaji huyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

AMUUA MKEWE KWA WIVU WA MAPENZI...!!!

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwamo la mwanamke mmoja kudaiwa kuuawa na mume wake kutokana na wivu wa mapenzi.
Katika tukio la kwanza, Mkazi wa Kijiji cha Liwalanje, wilayani Mbozi, Christina Hayola (35) amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kifuani na miguuni na mtu anayedaiwa kuwa mume wake.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba chanzo cha mauaji ni wivu wa mapenzi na kwamba polisi wanamsaka mhusika.
Katika tukio la pili, Msangi alisema mkazi wa Isanga jijini hapa, Abdi Sanga aliuawa kwa vipigo baada ya kutuhumiwa kuwa wizi katika eneo la Forest.
Alisema marehemu anadaiwa alikuwa na mwenzake ambaye alitoroka baada ya kuiba vitenge vyenye thamani ya Sh70,000.
Katika tukio la tatu na la nne, alisema mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ibumila wilayani Mbarali, Fitina Mwandosya alifariki dunia baada ya kudondoka kutoka kwenye trekta dogo aina ya ‘Powertiller’ alilokuwa amepanda akitoka kuvuna mpunga.
Alisema mwanafunzi huyo alipatwa na mkasa huo juzi wakati wanarudi na wenzake waliokwenda kuvuna mpunga wa shule.
Wakati huohuo mwanafunzi mwingine wa kidato cha pili Sekondari ya Makongorosi, wilayani Chunya, Aden Ngombe(17) amefariki dunia juzi baada ya kugongwa na lori aina ya scania alipokuwa akikatisha barabara.
Msangi alisema polisi walimkamata dereva wa lori na kubainika alikuwa amelewa pombe.
Katika matukio mengine watu wanne wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma mbalimbali zikiwamo za kukutwa na bastola kinyume na sheria.
Kamanda wa polisi alisema aliyekamatwa na bastola ni mkazi wa Kijiji cha Itentula, Mbozi aliyekuwa na bastola aina ya Baby. risasi tatu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na Mwananchi

MWANAMKE ALIYEBADILI DINI NA KUPEWA ADHABU YA KIFO APATA UTETEZI

Bi.Meriam Ibrahim na mumewe
Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya maswala ya kigeni nchini Sudan amesema kuwa mwanamke aliyepewa hukumu ya kifo kwa kubadili dini yake ya kiislamu, Meriam Ibrahim atawachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo.
Abdullahi Alzareg ambaye ni katibu katika wizara hiyo amesema kuwa Sudan inatilia maanani uhuru wa kuabudu na kwamba serikali itamtetea mwananmke huyo.
Kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu hukumu aliyopewa mwanamke huyo.
Meriam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.
Ameolewa na mkristo na pia amehukumiwa kuchapwa viboko mia moja kwa kuzini kwa sababu mwanamke wa kiislamu kuolewa na mkristo ni haramu kulingana na sheria za Sudan. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na BBC

Friday, May 30, 2014

WAMILIKI WA MAGARI WATAKIWA KURUDISHA MAGARI YAO KIWANDANI, SOMA HAPA UJUE NI GARI ZA AINA GANI

Kampuni kubwa ya kutengeza magari nchini Marekani imeagiza magari milioni 1.4 yarejeshwe kutokana na hitilafu ya usukani.
Takriban magari milioni 1.1 yaliyoundwa kwa mtindo wa kispoti yaliyokuwa yameuzwa Marekani Kaskazini yametakiwa kurejeshwa kwani huenda yana hitilafu kwenye usukani.
Vilevile magari mengine 200,000 yenye muundo wa Taurus yaliyoundwa kati ya mwaka wa 2010 na 2014 huenda yakakumbwa na tatizo ya kushika kutu kwa haraka.
Matukio kama hayo yaliyofanyika majuzi huenda yakaifanya kampuni hiyo kuvunja rekodi ya kutaka magari mengi zaidi yarejeshwe katika kipindi cha mwaka mmoja.
Urejesho huo umetokea wakati sakata ya usalama inawakumba wapinzani wakuu wa kampuni ya hiyo , General Motors (GM). GM ililaumiwa kwa kutotoa ilani za kiusalama kwamba baadhi ya magari yake hata baada ya kubaini kuwa magari hayo yanazima ghafla.
Dosari hiyo imehusishwa na vifo 13, ingawa wasanifu wa Marekani wanaamini kuwa idadi hiyo itaongezeka.
Pindi tangazo hilo lilipofanywa, kampuni za kutengeneza magari hayo pamoja na wasanifu wa Marekani wameongeza juhudi za kurejesha magari ambayo yanapatikana kuwa na dosari. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 30, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MMILIKI WAMANCHESTER UNITED, MALCOM GLAZER AFARIKI NA KUIACHA TIMU KWA WATOTO WAKE


Mmiliki wa Manchester United, Malcom Glazer amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85, na kuacha umiliki wa klabu hiyo kwa watoto wake sita.
Familia ya bilionea huyo iliinunua Man United kwa gharama ya Euro 790 milioni Mei, 2005 licha ya pingamizi kali kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo. Hata hivyo, chini ya umiliki wake uliosababisha deni kubwa kwa klabu hiyo ‘’the Red Devils’’ walishinda taji la Ligi Kuu mara tano na Ligi ya Mabingwa 2008.
Watoto wa Mmarekani huyo waliozaliwa Marekani Byan, Joel, na Avram wote wamejumuishwa katika bodi ya klabu hiyo, huku Joel na Avram wakiwa wenyekiti wenza.
Kifo cha Glazer hakitarajiwi kuathiri umiliki wa Man United, kwani familia hiyo bado inamiliki asilimia 90 za hisa za klabu hiyo.
Asilimia 10 inayosalia inamilikiwa na wenye hisa katika soko la hisa la NY stock Exchange. Glazer alikuwa pia mmiliki wa Tampa Bay Buccaneers, iliyobadili sura ya kandanda ya Marekani kwa kushinda taji la Super Bowl. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Bilionea huyo ambaye hakuwahi kukanyaga uwanjani Old Trafford kutokana na hofu ya kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wanamsuta kwa kupanga njama ya kuinunua klabu hiyo kwa kutumia madeni.

AUSTRALIA YAWA TIMU YA KWANZA KUWASILI BRAZIL NA REKODI YAKE YA MABAO 31-0

Australia-National-Football-Team-3 Timu ya soka ya Taifa ya Australia, maarufu kama ‘ Soccerrose’ ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja duniani. Australia waliichapa, American Samoa magoli 31-0, April 11, 2001 katika mchezo wa kimataifa unaotambuli wa na FIFA…Soccerrose, walitua nchini, Brazil siku ya juzi  tayari kwa michuano ya kombe la dunia inayotaraji kuanza kutimua vumbi, juni 12.  Australia ipo katika kundi la pili sambamba na mabingwa watetezi, Hispania, makamu bingwa wa fainali zilizopita, Uholanzi, na Chile.

Kikosi cha kocha, Ange Postecoglou kimeshawahi kucheza michuano hiyo mara tatu na mafanikio yao makubwa ni kufika hatua ya 16 bora, mwaka 2006… Kwa mara ya kwanza, Australia, ilifuzu kwa fainali za mwaka 1974 zilizofanyika nchini Ujerumani na kuondoka patupu. 

Walipata suluhu-tasa dhidi ya Chile, kisha wakapoteza kwa waliokuwa wenyeji wa michuano, Ujerumani Mashariki, na Ujerumani Magharibi na kuondoshwa mashindanoni pasipo kufunga goli lotote. 
Ikiwategemea zaidi wachezaji wake wazoefu kama Tim Cahiil, na nahodha wa kikosi hicho, Michael Jadinak ambaye anakipiga katika kikosi cha Crystal Palece ya England ,kikosi hicho kimekuwa timu ya kwanza kuwasili, Brazil. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIS BANDA "NITAHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU"

Rais Joyce Banda wa Malawi akipungia wafuasi wake waliokusanyika huko Lilongwe wakati wa uzinduzi wa kampeni yake. Machi 29, 2014.
Rais Joyce Banda wa Malawi akipungia wafuasi wake waliokusanyika huko Lilongwe wakati wa uzinduzi wa kampeni yake.
Mahakama kuu inapanga Ijumaa kutoa maamuzi kama iwapo matokeo ya uchaguzi yatangazwe hadharani au kura zihesabiwe tena. Matokeo ya awali yamemuweka Bi. Banda nyuma ya mpinzani wake Peter Mutharika.
Bi.Banda anasema uchaguzi ulijaa ubadhirifu, ikiwemo pamoja na wizi wa kura na watu kupiga kura zaidi ya mara moja.
Ameliambia shirika la habari la reuters kwamba atakubali maamuzi ya mahakama kuu, akifahamu fika kuwa amejaribu kutetea haki za wamalawi kwa kuhakikisha kuwa kiongozi anachaguliwa kwa haki na utaratibu wa heshima. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Bi.Banda ameamuru uchaguzi mpya uitishwe katika kipindi cha siku 90 na kusema hatakuwa mgombea. Lakini mahakama kuu imebatilisha maamuzi yake pale chama kikuu cha upinzani kilipowasilisha malalamiko.
CHANZO:VOA

Thursday, May 29, 2014

MUME WA FLORA MBASHA ANATAFUTWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA SHEMEJI YAKE



JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa kwa ubakaji.

Taarifa zilizopatikana  ndani  ya  jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi  yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada  la  Uchunguzi  Na. TBT/IR/1865/2014 akidai  kufanyiwa  unyama  huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili)  wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa  kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa  alitekeleza ukatili wake huo ndani ya  gari lake  hali ambayo  ilimfanya mlalamikaji kutoa  taarifa  Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.

 
Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji.

Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu  makali  aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi  aende  Hospitali ya Amana  na  kugundulika  kuwa aliingiliwa  kimapenzi na kumsababishia michubuko  sehemu za  siri. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MWILI WA MSANII RACHEL HAULE WAAGWA LEO JIJINI DAR

Mwili wa muigizaji wa filamu nchini Rachel Haule umeagwa leo hii katika viwanja vya Leaders na baada ya hapo atazikwa katika makaburi ya Kinondoni. Wasanii wengi ndugu, jamaa na marafiki wamejawa katika simanzi kubwa huku Irene Uwoya akizimia pengine kwa mshituko wa kuondokewa na msanii mwenzao. Angalia picha zikionyesha matukio ya mwili wa Rachel tangu akitolewa Muhimbili, kupelekwa Sinza na Leaders..........
Irene Uwoya akiwa amezimia . Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

SHEIKH PONDA AGOMA KWENDA MAHAKAMANI

Sheikh-Ponda1_41fd8.jpg
Kiongozi wa Taasisi ya Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, jana aligoma kufikishwa mahakamani kutoka mahabusu ya Gereza la Mkoa wa Morogoro, akidai kuchoshwa kuhairishwa kwa kesi yake kila anapofikishwa mahakamani.



Pamoja na kuchelewa kufikishwa mahakamani, kesi yake iliahirishwa tena hadi Juni 10 baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo kusema kuwa jalada bado halijarudishwa kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Wakili wa kiongozi huyo, Bathelomeo Tarimo alilalamikia hali hiyo na kutaka haki itendeke kwa mteja wake.

Akizungumza jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza alisema kuwa kukwama kwa faili la Sheikh Ponda ni kutokana na maombi namba 25 ya mwaka 2014 yanayosubiri kusikilizwa mahakamani hadi sasa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 29, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

HALIMA MDEE AMVURUGA WAZIRI TIBAIJUKA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana alijikuta katika wakati mgumu wakati alipokuwa waziri wa kwanza kuhusishwa na tuhuma za ufisadi wa kutumia vibaya madaraka yake na lawama lukuki kuhusu kasoro za kiutendaji katika wizara anayoiongoza.


Mawaziri wengine wamekuwa wakiwekwa kitimoto kutokana na tuhuma za utendaji mbovu na udhaifu kwenye wizara zao, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati Waziri Kivuli wa Ardhi, Halima Mdee aliposoma hotuba ya kurasa 77 ya upinzani kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, huku kurasa 30 zikielekeza tuhuma kwa waziri huyo.
Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya waziri huyo ni pamoja na kujinufaisha kupitia mgogoro wa ardhi katika eneo la Chasimba na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Mdee, ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alimhusisha waziri huyo na ufisadi katika kazi ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa masuala ya ardhi, uliogharimu Sh700 milioni. Tuhuma hizo zilimchanganya Waziri Tibaijuka kiasi kwamba wakati akitoa majibu alijikuta akitoka nje ya mada na kumshambulia Mdee, huku Spika Anne Makinda akimrudisha kila mara na kumtaka ajikite kwenye hoja na kuacha kushambulia wapinzani.
Waziri Tibaijuka pia alidai hotuba ya upinzani ilijaa uongo na kumtaka Spika Makinda kumchukulia hatua Mdee. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIS GOODLUCK ATANGAZA VITA VIKALI

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameagiza kufanywa oparesheni kali zaidi ili kudhibiti alichokiita mauaji ya kiholela yanayofanywa na magaidi.
Katika hotuba kwa taifa kuadhimisha siku ya demokrasia, rais Jonathan alitaja utekaji nyara wa zaidi ya wasichana mia mbili wa shule na kundi la Boko Harama kuwa unyama usiokubalika kamwe.
Waandishi hata hivyo wanasema kuwa haijulikani rais Jonathana anazungumzia kuchukua hatua zipi au ni oparesheni gani itafanywa kwa sababu tayari eneo hilo la Kaskazini mashariki mwa Nigeria tayari limewekwa chini ya hali ya hatari.
Rais Jonathan pia ameahidi kufanya mashauriano na upatanishi na watu watakaoweka silaha chini na kukoma kujihusisha na ugaidi.
Alipongeza jamii ya kimataifa kwa kuisaidia Nigeria kukabiliana na tatizo la ugaidi na usalama kwa jumla.
Rais Jonathan ameahidi kushughulikia swala la umasikini ambalo limechochea harakati kama za Boko Haram, lakini akasisitiza hilo litafanyika tu ikiwa ugaidi unaotendwa na Boko Haram utakomeshwa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Benki ya dunia inasema kuwa zaidi ya watu milioni miamoja na kumi na tatu wanaishi kwa umaskini katika taifa hilo linalozalisha kiwango kikubwa zaidi cha mafuta Afrika.
Rais Goodluck, ametoa fursa kwa Boko Haram ikiwa wanataka kufanya mazungumzo na serikali kama njia ya kusuluhisha matatizo yao.
Maelfu ya watu wameuawa katika miaka mitano ya harakati za kundi hilo.Mwaka huu pekee watu 2,000 wameuawa huku zaidi ya wengine 750,000 wakiachwa bila makao.

MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU MALAWI KUTANGAZWA KESHO

Hatimaye tume ya uchaguzi nchini Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kesho ijumaa.
Uamuzi huo unakuja baada ya mivutano na mapingamizi kadhaa kwenye mahakama kuu nchini humo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ameeleza kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe kuwa sasa wananchi wa Malawi wameondolewa hofu ya kusubiri kwa muda mrefu matokeo ya kura za uchaguzi walioufanya juma lililopita.
Taarifa fupi iliyotolewa na tume ya uchaguzi jana usiku mjini Blantyre, imesema wameamua kutangaza matokeo hayo kwa kuzingatia sheria inayoibana kufanya hivyo ndani ya siku zisizozidi nane na ikiwa ni baada ya saa 48 tangu kumaliza hesabu ya kura.
Kwa siku mbili sasa kumekuwa na tuhuma za kuokotwa kwa baadhi ya masanduku ya kura, huku baadhi ya magari ya yakipatikana na masanduku ya kura na hata katika baadhi ya maeneo ambako ilielezwa kuwa kura zimehifadhiwa, usalama wake umesemwa kuwa mdogo.
Tangu jumatatu tume hiyo imekuwa ikisubiri uamuzi wa mahakama kuu mjini Blantyre wa kuiongeza muda wa angalau siku 30 kukamilisha jukumu ililopewa, hata hivyo mahakama yenyewe bado ina mashauri mengine iliyopokea kuhusu uchaguzi huu
Mmoja kati ya wananchi wa nchi hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Malani Nyirenda, alielezea hisia zake alipozungumza na BBC mjini Lilongwe kutokana na suala la kuchelewa kutolewa matokeo na mpango wa kuhesabu upya kura za baadhi ya maeneo.
Tume hiyo imesema hadi kufikia sasa imepokea malalamiko 275 na imekwisha yafanyia kazi malalamiko 170 tu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...