Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na waendesha bodaboda na kuahidi kushugulikia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa vikwazo vya wao kuingia katikati ya jiji.
Aidha, amewaahidi kuwapatia pikipiki kwa marejesho ya Sh25,000 kwa wiki kwa muda maalum kabla ya kuwaachia kabisa.
Kwa mantiki hiyo, Makonda amewataka kufanya usajili upya na kusajili vituo vyao ili watambulike kisheria huku akisema atawapatia mavazi maalum 'reflectors' kama utambulisho.
Awali, mmoja wa waendesha bodaboda hao, Daud Laurian alimsomea RC Makonda risala iliyoainisha matatizo yao ikiwemo zuio la ya jiji kutokana na agizo la aliyekua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick Machi 3, 2014.
Waendesha hao wamehaokikishia Makonda kuwa raia wema katika suala zima la ulinzi iwapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum litawachukulia kama ndugu zao na marafiki.