Wananchi wa Kijiji cha Nyalubanda wakiwa wamembeba Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe alipowasili katika kijiji hicho jana katika hafla
ya kukabidhi gari la wagonjwa alilotoa ahadi katika kampeni za Uchaguzi
wa mwaka 2010.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
amesema kutimuliwa uanachama na Chadema ni dhoruba inayomkumba
mwanasiasa yeyote anayefanikiwa na kwamba iko siku atashika “nafasi
kubwa ya uongozi ya kuwatumikia Watanzania”.
Zitto aliwasili mjini hapa juzi, ikiwa ni siku
chache baada ya Chadema kutangaza kumtimua uanachama kwa kosa la
kupeleka mgogoro wa ndani ya chama kwenye mahakama.
Alifungua kesi Mahakama Kuu akitaka imuamuru
katibu mkuu wa Chadema kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu
vilivyomvua madaraka yote na baadaye kukizuia chama hicho kumjadili.
Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali shauri lake na Chadema ikatangaza
mara moja kumtimua. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.