Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati) akiwasihi Mbunge wa
Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy
wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta
Escrow na kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli
kati yake na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.
Juzi, kamati hiyo ya Zitto iliwasilisha ripoti
yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo amekuwa mara kwa mara
akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba ndani ya fedha hizo
hakukuwa na fedha za umma.
Kamati hiyo ilieleza kuwa imebaini kuwa Profesa
Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Singh Sethi na
James Rugemalira tena katika ofisi ya umma na pengine hilo ndilo
lilikuwa sababu ya upotoshaji.
Akiwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo,
Profesa Muhongo alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine ingawa
katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa na wachangiaji wengine waliohoji
uhalali wa vielelezo alivyotoa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz