Wawakilishi
wa Chama cha Uhifadhi wa Wanyama cha Frankfurt (FZS), wakikabidhi
magari zaidi ya 11 kwa Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam jana, kwa
ajili ya kusaidia vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori katika hifadhi
na mbuga za taifa.Picha na Ikulu
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali
imenuia kumaliza kabisa ujangili nchini, ikiwa ni hatua ya kunusuru
wanyama walio hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.Hakusita kusisitiza kwamba, nia ya dhati ya Serikali ni kuhakikisha mkakati huo unakamilika, japokuwa kumekuwa na changamoto zinazotokana na ukubwa wa hifadhi hizo na uhaba wa vitendea kazi pamoja na askari wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa kupokea magari 11 ya kisasa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili kutoka kwa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la Ujerumani, Kikwete alisema tatizo hilo limekuwa la muda mrefu, lakini juhudi za kulikomesha zinafanyika.
Alisema, pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna tatizo la uhaba mkubwa wa wafanyakazi wanaotakiwa kudhibiti majangili, ambapo kwa sasa kuna wafanyakazi 1,155 sawa na asilimia 24 tu ya mahitaji halisi ya wafanyakazi 4,000 wanaohitajika.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz