Na Steven Kanyeph - SHINYANGA
Wazazi ambao hawajulikani makazi yao maalumu wameitelekeza familia ya
watoto wao wanne katika hoteli ya Ibanza iliyopo mjini Shinyanga kwa
takribani miezi 3 ambapo mpaka sasa wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni
tatu.
Mhasibu wa Hoteli hiyo bwana Julius Kiungu amemtaja bi Christina Peter
ambaye ni mzazi wa watoto hao kuwa alifika katika hoteli ya Ibanza Mei,
15 mwaka huu akiwa na watoto wa wanne kwa lengo la kupumzika.
Bi Chritina ambaye ni mzazi wa watoto hao alieendelea kuwepo katika
hoteli hiyo kwa takribani wiki mbili lakini baada ya hapo aliondoka bila
taarifa na kuwatelekeza watoto wake katika hoteli hiyo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Mmoja wa watoto hao aliyejitambulisha kwa jina la Teddy Masumbuko
mwenye umri wa miaka 20 amesema kuwa anashangazwa na kitendo cha mama
yao kuondoka bila kutoa taarifa huku akimuacha na wadogo zake watatu
wenye umri mdogo.
Msemaji wa hoteli hiyo bwana Julius Kiungu anawaomba ndugu, jamaa na
marafiki wa familia hiyo wafike ili kuwachukuwa watoto hao kwa ulinzi na
usalama wa watoto hao.