Orodha
mpya ya vyuo vikuu bora zaidi
duniani ya Times Higher Education, kwa kuangazia sifa za chuo kikuu
husika, imetolewa, huku vyuo vikuu kutoka bara Asia vikiimarika sana.
Mwaka huu, kuna vyuo vikuu 17 kutoka Asia vilivyomo kwenye orodha ya
vyuo 100 bora, likiwa ongezeko kutoka vyuo 10 mwaka jana.
Kwa
mara ya kwanza, kuna chuo kikuu kutoka Uchina katika 20 bora, Chuo
Kikuu cha Tsinghua University kutoka Beijing ambacho kimo nambari 18.
Vyuo vikuu vya Marekani bado vinatawala orodha hiyo, chuo kikuu cha
Harvard kikiwa ndicho kinachoongoza. Vifuatavyo ni vyuo vikuu bora 100.