Sunday, March 15, 2015
MILIPUKO YALENGA MAKANISA...!!!
Mabomu mawili yamelipuka yakilenga makanisa mawili yaliyokuwa yamejaa
watu kwenye mji wa Lahore chini Pakistan wakati watu walipokuwa
wakihudhuria misa ya jumapili.
Polisi wanasema kuwa takriban watu 6 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo yanaoyoaminika kuwa ya kujitoa mhanga yalifanyika eneo lenye waumini wengi wa kikristo la Youhanabad
Sehemu ya kundi la Taliban linalofahamika kama Jamatul Ahra limesema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SOMO KUHUSU UBAKAJI KUFUNZWA UINGEREZA
Wanafunzi
kuanzia miaka 11 nchini Uingereza watafundishwa kuhusu tofauti kati ya
ubakaji na tendo la ngono ambalo limetekelezwa kutokana na idhini ya
wapenzi wawili kama mojawapo ya mipango ya kuwawapa ujuzi kuhusu maisha
ya sasa nchini humo
Somo hilo ambalo litaanzishwa mara moja baada
ya siku kuu ya Easter litaongezwa katika mtaala wa Uingereza baada ya
wasiwasi kutolewa kwamba vijana walikuwa wakishinikizwa kushiriki katika
ngono.
Nick Morgan ambaye ni katibu wa elimu alitoa tangazo hilo siku ya kimataifa ya wanawake.
''Lazima
swala hili tulikabili kwamba mambo ambayo wasichana wetu wanapitia
hayakuwepo wakati wa ujana weyu,kwa hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha
kuwa wasichana wetu wanamaliza shule wakiwa na uwezo wa kukabiliana na
changaomoto watakazokumbana nazo wakiwa watu wazima'', aliandika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
VATICAN: NGUVU ZITUMIWE DHIDI YA IS
Makao makuu ya kanisa katoliki duniani Vatican yanasema kuwa nguvu
inaweza kutumiwa kusitisha mashambulizi yanayoendeshwa na wanamgambo wa
Islamic State dhidi ya wakristo na makundi mengine madogo .
Askofu
mkuu Silvano Tomasi ambaye ni mwakilishi mkuu wa Vatican kwenye umoja
wa mataifa mjini Geneva ameyashutumu makundi ya jihad kwa kuendesha
mauaji ya halaiki.
Akizungumza kupitia mtandao wa Vatican amesema kuwa hatua za kijeshi zitaanzishwa ikiwa suluhu ya kisiasa haitapatikana.
Lakini amesema kuwa muungano wowote dhidi ya Islamic State ni lazima ujumuishe nchi za kiislamu kutoka mashariki ya kati. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MAN UNITED KUMKOSA DI MARIA
Kilabu
ya Manchester United itamkosa Angel Di Maria,ambaye anahudumia mafuruku
ya mechi moja baada ya kupewa kadi nyekundi dhidi ya Arsenal,naye Jonny
Evans akiwa anahudumia marufuku.
Mshambuliaji nyota Robbin Van
Persie bado anauguza jeraha huku Marcos Rojo akiwa hajulikani iwapo
atachezeshwa kutokana na jeraha la paja.
Hatahivyo Ashley Young atacheza licha ya kujiumiza mguu siku ya jumatatu.
Kocha wa kilabu ya Tottenham Mauricio Pochettino ana kikosi chake kizima.
Danny Rose huenda akacheza mechi ya leo katika safu ya ulinzi wa kushoto huku Mousa Dembele pia akitarajiwa kuanza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WENGER: ARSENAL ITAIBANDUA MONACO
Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa kilabu hiyo bado ina fursa ya
kuibandua Monaco katika michuano ya kilabu bingwa barani Ulaya licha ya
kucharazwa 3-1 katika awamu ya kwanza ya mechi hizo.
Arsenal
itakabiliana na timu hiyo ya Ligi ya daraja la kwanza siku ya jumapili
huku ikiwa hakuna timu ilioweza kufanikiwa kubadilisha matokeo kama hayo
katika michuano hiyo.
Wenger:Tuna changamoto kubwa mbele yetu lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha kwamba tunafuzu kwa robo fainali.
''Wao ndio wanaopigiwa upato kufuzu lakini tunaweza kubadilisha mambo''.
''Tutahakikisha kuwa tuna hamu na imani ya kushinda''.
Arsenal italazimika kufunga bao tatu kwa bila ili kuweza kufuzu kwa robo fainali.
Tayari kilabu hiyo imepata motisha kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya kilabu ya West Ham siku ya jumamosi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Saturday, March 14, 2015
KINANA AMSIFU, AMPONDA NYARANDU...!!!
Jana ilikuwa siku ya hisia tofauti kwa watu wawili wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro cha urais, Edward Lowassa na Lazaro Nyalandu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kumsifu mmojawao na kumponda mwingine.
Akiwa Kondoa, Kinana alitumia muda mwingi kujibu
kilio cha wananchi wanaosumbuliwa na askari wa wanyamapori kwa kumponda
Waziri Nyalandu kuwa anazurura bila kushughulikia matatizo ya wananchi,
lakini saa chache baada ya kuwasili Monduli alimsifu Lowassa kuwa ni
kiongozi shupavu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
UNENE WAMKOSESHA BURUDANI
Mama
mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake wawili walizuiliwa kuingia
katika kilabu moja ya burudani kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni wanene
sana na wenye sura mbaya
Stacey Owen 33, alikuwa ametoka na
marafiki zake wawili kwa ajili ya kupata burudani wakati wa usiku siku
ya jumamosi alipokataliwa kuingia katika baa moja jijini Manchester kwa
sababu ya unene wake.
Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine wakiingia katika baa hiyo maarufu mjini humo,
Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na wamiliki wa Baa hiyo lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka kwao.
Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni mrembo sana lakini kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa wateja. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu
zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click
Neno Jambo Tz.
Friday, March 13, 2015
HUYU NDIYE MTOTO ALIYENUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA BASI YA MAJINJA PALE CHANGARAWE MUFINDI
Hapa mtoto huyo akiendelea kutibiwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi. Tupia neno moja kwa mtoto huyu ili kumtakia afya njema katika Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SERIKALI KUJENGA NYUMBA 403 MWAKATA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua
ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani
Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali
itajenga nyumba 403 ambazo zimebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha wiki
iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu
649 kukosa mahali pa kuishi.
Kauli hiyo aliitoa jana kwenye kijiji cha Mwakata
baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na mvua hiyo na kujionea maisha
duni wanayoishi watu hao.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake
Rais Kikwete alisema Serikali iko pamoja na wananchi hao na
itahakikisha makazi yao yanarejea katika hali yake ya kawaida kwa
kuwajengea nyumba hizo.
Pia,
Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Kujenga
Taifa(JKT) wajenge nyumba hizo bila kupitia mkandarasi yeyote kama vile
ulivyo ujenzi wa Serikali kwa kuwa ujenzi wa jeshi unaisha kwa muda
mfupi na hakuna uchakachuaji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu
zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click
Neno Jambo Tz.
MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MH. MBONI MHITA AUNDA KAMATI MAALUMU YA KUCHUNGUZA CHANZO CHA AJALI YA CHANGARAWE
Mh. Mboni Mhita akizungumza na moja wa majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Mufindi
Mkuu wa wilaya akiwa na wana kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo eneo la tukio
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MAASKOFU: PIGIENI KATIBA KURA YA HAPANA
Jukwaa la Wakristo Tanzania
limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu
la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa
kwa kupiga kura ya “hapana”.
Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na
kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk
Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki
Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa
la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili
za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya
Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha
mgawanyiko.
“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote
wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya
elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi
kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa
hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WATOTO WENGINE 11 WAKUTWA WAMEFICHWA
Baadhi ya watoto 18 katika tukio la kwanza walikuwa wakihifadhiwa kwenye
nyumba iliyopo Kata ya Pasua kwa lengo la kuwafundisha dini ya
Kiislamu, mkoani Kilimanjaro.
Mambo mazito zaidi yamezidi kubainika
mkoani Kilimanjaro baada ya polisi kugundua nyumba nyingine yenye watoto
kumi na mmoja waliokusanywa kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya
kufundishwa dini.
Hii ni mara ya pili katika muda usiozidi wiki moja
baada ya polisi kubaini nyumba iliyohifadhi watoto 18 kwa lengo kama
hilo Jumamosi iliyopita.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela
alisema tukio hilo linafanya wapelelezi kuumiza vichwa kwa kuwa mikoa
waliyotoka ndio ile ile waliyotoka watoto 18 waliokutwa kwenye nyumba
moja mjini Moshi.
Nyumba
hiyo imebainika wakati kukiwa na madai
kwamba baadhi ya misikiti katika maeneo ya Pasua, Njoro na Kibosho
yanaendesha mafunzo ya judo na karate. Tangaza biashara yako hapa kwa
bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa
Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Subscribe to:
Posts (Atom)