
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo, Diego Gutierrez (Kulia) na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Muhula wakitia saini ya
makubaliano jijini Dar es Salaam jana baina ya Tigo na DTBi ya kusaidia
wajasiriamali kujifunza teknolojia ya digitali na mawasiliano.
Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof
Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH), Dk Hassan Mshinda. Picha na Venance Nestory.
Kampuni za simu
za mkononi za Tigo, Airtel na Zantel zimeunganisha huduma zao za kutoa,
kutuma na kuweka fedha na sasa mteja anaweza kutuma fedha kutoka mtandao
mmoja kupitia mwingine.
Taarifa ya pamoja na kampuni hizo iliyotolewa
jana, ilisema kuwa wote wanaotumia huduma za kifedha za mitandao hiyo,
wataweza kutumiana fedha kupitia simu zao za mikononi pasi na tatizo
baada ya kampuni hizo kuunganisha huduma zao.
Huduma hiyo inayotarajiwa kuanza kutumika mwishoni
mwa mwezi huu, itawafanya wateja wa mitandao hiyo kutumiana na kupokea
fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao tofauti na ilivyokuwa awali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz