Friday, May 30, 2014

MMILIKI WAMANCHESTER UNITED, MALCOM GLAZER AFARIKI NA KUIACHA TIMU KWA WATOTO WAKE


Mmiliki wa Manchester United, Malcom Glazer amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85, na kuacha umiliki wa klabu hiyo kwa watoto wake sita.
Familia ya bilionea huyo iliinunua Man United kwa gharama ya Euro 790 milioni Mei, 2005 licha ya pingamizi kali kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo. Hata hivyo, chini ya umiliki wake uliosababisha deni kubwa kwa klabu hiyo ‘’the Red Devils’’ walishinda taji la Ligi Kuu mara tano na Ligi ya Mabingwa 2008.
Watoto wa Mmarekani huyo waliozaliwa Marekani Byan, Joel, na Avram wote wamejumuishwa katika bodi ya klabu hiyo, huku Joel na Avram wakiwa wenyekiti wenza.
Kifo cha Glazer hakitarajiwi kuathiri umiliki wa Man United, kwani familia hiyo bado inamiliki asilimia 90 za hisa za klabu hiyo.
Asilimia 10 inayosalia inamilikiwa na wenye hisa katika soko la hisa la NY stock Exchange. Glazer alikuwa pia mmiliki wa Tampa Bay Buccaneers, iliyobadili sura ya kandanda ya Marekani kwa kushinda taji la Super Bowl. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Bilionea huyo ambaye hakuwahi kukanyaga uwanjani Old Trafford kutokana na hofu ya kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wanamsuta kwa kupanga njama ya kuinunua klabu hiyo kwa kutumia madeni.

AUSTRALIA YAWA TIMU YA KWANZA KUWASILI BRAZIL NA REKODI YAKE YA MABAO 31-0

Australia-National-Football-Team-3 Timu ya soka ya Taifa ya Australia, maarufu kama ‘ Soccerrose’ ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja duniani. Australia waliichapa, American Samoa magoli 31-0, April 11, 2001 katika mchezo wa kimataifa unaotambuli wa na FIFA…Soccerrose, walitua nchini, Brazil siku ya juzi  tayari kwa michuano ya kombe la dunia inayotaraji kuanza kutimua vumbi, juni 12.  Australia ipo katika kundi la pili sambamba na mabingwa watetezi, Hispania, makamu bingwa wa fainali zilizopita, Uholanzi, na Chile.

Kikosi cha kocha, Ange Postecoglou kimeshawahi kucheza michuano hiyo mara tatu na mafanikio yao makubwa ni kufika hatua ya 16 bora, mwaka 2006… Kwa mara ya kwanza, Australia, ilifuzu kwa fainali za mwaka 1974 zilizofanyika nchini Ujerumani na kuondoka patupu. 

Walipata suluhu-tasa dhidi ya Chile, kisha wakapoteza kwa waliokuwa wenyeji wa michuano, Ujerumani Mashariki, na Ujerumani Magharibi na kuondoshwa mashindanoni pasipo kufunga goli lotote. 
Ikiwategemea zaidi wachezaji wake wazoefu kama Tim Cahiil, na nahodha wa kikosi hicho, Michael Jadinak ambaye anakipiga katika kikosi cha Crystal Palece ya England ,kikosi hicho kimekuwa timu ya kwanza kuwasili, Brazil. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIS BANDA "NITAHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU"

Rais Joyce Banda wa Malawi akipungia wafuasi wake waliokusanyika huko Lilongwe wakati wa uzinduzi wa kampeni yake. Machi 29, 2014.
Rais Joyce Banda wa Malawi akipungia wafuasi wake waliokusanyika huko Lilongwe wakati wa uzinduzi wa kampeni yake.
Mahakama kuu inapanga Ijumaa kutoa maamuzi kama iwapo matokeo ya uchaguzi yatangazwe hadharani au kura zihesabiwe tena. Matokeo ya awali yamemuweka Bi. Banda nyuma ya mpinzani wake Peter Mutharika.
Bi.Banda anasema uchaguzi ulijaa ubadhirifu, ikiwemo pamoja na wizi wa kura na watu kupiga kura zaidi ya mara moja.
Ameliambia shirika la habari la reuters kwamba atakubali maamuzi ya mahakama kuu, akifahamu fika kuwa amejaribu kutetea haki za wamalawi kwa kuhakikisha kuwa kiongozi anachaguliwa kwa haki na utaratibu wa heshima. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Bi.Banda ameamuru uchaguzi mpya uitishwe katika kipindi cha siku 90 na kusema hatakuwa mgombea. Lakini mahakama kuu imebatilisha maamuzi yake pale chama kikuu cha upinzani kilipowasilisha malalamiko.
CHANZO:VOA

Thursday, May 29, 2014

MUME WA FLORA MBASHA ANATAFUTWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA SHEMEJI YAKE



JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa kwa ubakaji.

Taarifa zilizopatikana  ndani  ya  jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi  yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada  la  Uchunguzi  Na. TBT/IR/1865/2014 akidai  kufanyiwa  unyama  huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili)  wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa  kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa  alitekeleza ukatili wake huo ndani ya  gari lake  hali ambayo  ilimfanya mlalamikaji kutoa  taarifa  Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.

 
Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji.

Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu  makali  aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi  aende  Hospitali ya Amana  na  kugundulika  kuwa aliingiliwa  kimapenzi na kumsababishia michubuko  sehemu za  siri. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MWILI WA MSANII RACHEL HAULE WAAGWA LEO JIJINI DAR

Mwili wa muigizaji wa filamu nchini Rachel Haule umeagwa leo hii katika viwanja vya Leaders na baada ya hapo atazikwa katika makaburi ya Kinondoni. Wasanii wengi ndugu, jamaa na marafiki wamejawa katika simanzi kubwa huku Irene Uwoya akizimia pengine kwa mshituko wa kuondokewa na msanii mwenzao. Angalia picha zikionyesha matukio ya mwili wa Rachel tangu akitolewa Muhimbili, kupelekwa Sinza na Leaders..........
Irene Uwoya akiwa amezimia . Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

SHEIKH PONDA AGOMA KWENDA MAHAKAMANI

Sheikh-Ponda1_41fd8.jpg
Kiongozi wa Taasisi ya Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, jana aligoma kufikishwa mahakamani kutoka mahabusu ya Gereza la Mkoa wa Morogoro, akidai kuchoshwa kuhairishwa kwa kesi yake kila anapofikishwa mahakamani.



Pamoja na kuchelewa kufikishwa mahakamani, kesi yake iliahirishwa tena hadi Juni 10 baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo kusema kuwa jalada bado halijarudishwa kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Wakili wa kiongozi huyo, Bathelomeo Tarimo alilalamikia hali hiyo na kutaka haki itendeke kwa mteja wake.

Akizungumza jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza alisema kuwa kukwama kwa faili la Sheikh Ponda ni kutokana na maombi namba 25 ya mwaka 2014 yanayosubiri kusikilizwa mahakamani hadi sasa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 29, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

HALIMA MDEE AMVURUGA WAZIRI TIBAIJUKA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana alijikuta katika wakati mgumu wakati alipokuwa waziri wa kwanza kuhusishwa na tuhuma za ufisadi wa kutumia vibaya madaraka yake na lawama lukuki kuhusu kasoro za kiutendaji katika wizara anayoiongoza.


Mawaziri wengine wamekuwa wakiwekwa kitimoto kutokana na tuhuma za utendaji mbovu na udhaifu kwenye wizara zao, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati Waziri Kivuli wa Ardhi, Halima Mdee aliposoma hotuba ya kurasa 77 ya upinzani kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, huku kurasa 30 zikielekeza tuhuma kwa waziri huyo.
Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya waziri huyo ni pamoja na kujinufaisha kupitia mgogoro wa ardhi katika eneo la Chasimba na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Mdee, ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alimhusisha waziri huyo na ufisadi katika kazi ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa masuala ya ardhi, uliogharimu Sh700 milioni. Tuhuma hizo zilimchanganya Waziri Tibaijuka kiasi kwamba wakati akitoa majibu alijikuta akitoka nje ya mada na kumshambulia Mdee, huku Spika Anne Makinda akimrudisha kila mara na kumtaka ajikite kwenye hoja na kuacha kushambulia wapinzani.
Waziri Tibaijuka pia alidai hotuba ya upinzani ilijaa uongo na kumtaka Spika Makinda kumchukulia hatua Mdee. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIS GOODLUCK ATANGAZA VITA VIKALI

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameagiza kufanywa oparesheni kali zaidi ili kudhibiti alichokiita mauaji ya kiholela yanayofanywa na magaidi.
Katika hotuba kwa taifa kuadhimisha siku ya demokrasia, rais Jonathan alitaja utekaji nyara wa zaidi ya wasichana mia mbili wa shule na kundi la Boko Harama kuwa unyama usiokubalika kamwe.
Waandishi hata hivyo wanasema kuwa haijulikani rais Jonathana anazungumzia kuchukua hatua zipi au ni oparesheni gani itafanywa kwa sababu tayari eneo hilo la Kaskazini mashariki mwa Nigeria tayari limewekwa chini ya hali ya hatari.
Rais Jonathan pia ameahidi kufanya mashauriano na upatanishi na watu watakaoweka silaha chini na kukoma kujihusisha na ugaidi.
Alipongeza jamii ya kimataifa kwa kuisaidia Nigeria kukabiliana na tatizo la ugaidi na usalama kwa jumla.
Rais Jonathan ameahidi kushughulikia swala la umasikini ambalo limechochea harakati kama za Boko Haram, lakini akasisitiza hilo litafanyika tu ikiwa ugaidi unaotendwa na Boko Haram utakomeshwa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Benki ya dunia inasema kuwa zaidi ya watu milioni miamoja na kumi na tatu wanaishi kwa umaskini katika taifa hilo linalozalisha kiwango kikubwa zaidi cha mafuta Afrika.
Rais Goodluck, ametoa fursa kwa Boko Haram ikiwa wanataka kufanya mazungumzo na serikali kama njia ya kusuluhisha matatizo yao.
Maelfu ya watu wameuawa katika miaka mitano ya harakati za kundi hilo.Mwaka huu pekee watu 2,000 wameuawa huku zaidi ya wengine 750,000 wakiachwa bila makao.

MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU MALAWI KUTANGAZWA KESHO

Hatimaye tume ya uchaguzi nchini Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kesho ijumaa.
Uamuzi huo unakuja baada ya mivutano na mapingamizi kadhaa kwenye mahakama kuu nchini humo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ameeleza kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe kuwa sasa wananchi wa Malawi wameondolewa hofu ya kusubiri kwa muda mrefu matokeo ya kura za uchaguzi walioufanya juma lililopita.
Taarifa fupi iliyotolewa na tume ya uchaguzi jana usiku mjini Blantyre, imesema wameamua kutangaza matokeo hayo kwa kuzingatia sheria inayoibana kufanya hivyo ndani ya siku zisizozidi nane na ikiwa ni baada ya saa 48 tangu kumaliza hesabu ya kura.
Kwa siku mbili sasa kumekuwa na tuhuma za kuokotwa kwa baadhi ya masanduku ya kura, huku baadhi ya magari ya yakipatikana na masanduku ya kura na hata katika baadhi ya maeneo ambako ilielezwa kuwa kura zimehifadhiwa, usalama wake umesemwa kuwa mdogo.
Tangu jumatatu tume hiyo imekuwa ikisubiri uamuzi wa mahakama kuu mjini Blantyre wa kuiongeza muda wa angalau siku 30 kukamilisha jukumu ililopewa, hata hivyo mahakama yenyewe bado ina mashauri mengine iliyopokea kuhusu uchaguzi huu
Mmoja kati ya wananchi wa nchi hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Malani Nyirenda, alielezea hisia zake alipozungumza na BBC mjini Lilongwe kutokana na suala la kuchelewa kutolewa matokeo na mpango wa kuhesabu upya kura za baadhi ya maeneo.
Tume hiyo imesema hadi kufikia sasa imepokea malalamiko 275 na imekwisha yafanyia kazi malalamiko 170 tu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

Wednesday, May 28, 2014

WANACHAMA WA SIMBA WAANDAMANA NA KUFUNGA NJIA ZA MSIMBAZI WAKITAKA WAMBURA ARUDISHWE KWENYE ORODHA YA WAGOMBEA



Mashabiki wa Timu ya Simba wakijikusanya nje ya jengo la klabu hiyo kongwe kupinga Wambura kuondolewa kwenye uchaguzi unakuja hivi karibuni.
Hapa mashabiki wakizidi kujikusanya kwa wingi mchana huu.
Wanachama wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo la klabu yao mchana huu kupinga kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu hiyo.
Wanachama wa Simba wakipiga kelele nje ya jengo la klabu yao hiyo wakitaka wapewe ufafanuzi wa kina kwanini Wambura ametolewa kwenye uchaguzi unaokuja. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MBUNGE WA NKASI NUSURA APIGWE NJE YA UKUMBI WA BUNGE...!!!




Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Mohamed Kessy (kushoto) akiwakwepa wabunge wa CUF, Kombo Khamis Kombo (kulia) na Ibrahim Mohammed Sanya (wa pili kushoto) walipokuwa wakimfokea nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana na Mbunge wa Mikumi, Abdulsalaam Amer akijalibu kuwazuia. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Na Fidelis Butahe na Sharon Sauwa, Mwananchi

Kelele, kukunjana na kunyoosheana vidole jana mchana vilitawala nje ya ukumbi wa Bunge wakati wabunge wa CUF kutoka Zanzibar walipotaka ‘kumkanya’ Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy.

Sakata hilo la aina yake lililodumu kwa takriban dakika 15 lilitokea saa 7:05 mchana baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuahirisha kikao cha Bunge.

Wabunge hao Mussa Haji Kombo (Chakechake), Kombo Khamis Kombo (Magogoni) na Muhammad Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe), walitaka ‘kumkanya’ Keissy kutokana na kile alichosema alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka 2014/15 na kusema Zanzibar haichangii katika Muungano, hivyo haina haki ya kuhoji mambo ya upande wa pili.

Kauli hiyo licha ya kulalamikiwa na wabunge wote wa CUF kutoka Zanzibar kiasi cha kufikia hatua ya kusimama na kuomba mwongozo wa Spika, Keissy alizidi kuwashambulia na kusema kuwa majimbo ya Zanzibar watu wake wanaweza kukusanywa sehemu moja kwa kupigiwa filimbi tu.

“Nyie Zanzibar idadi yenu ya watu ni asilimia 2.8 ya watu wote wa Tanzania. Sasa mnataka kupata kila kitu sawa ili iweje! Mnataka ajira asilimia 21 na Watanganyika wakafanye kazi wapi?” alisema Keissy.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho na wabunge kuanza kutoka nje, wabunge hao wa CUF walikwenda kumsubiri Keissy karibu na jengo la kantini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

DEREVA APORWA LORI LA MAFUTA AKIWA KWENYE FOLENI MIZANI


Picha na Maktaba

Watu watano wasiofahamika wanaodhaniwa ni wezi, wamemvamia dereva wa lori la mafuta, Stephano John eneo la Kibamba, Barabara Kuu ya Dar es Salaam -Morogoro alipokuwa katika foleni na kisha kumpiga, kumjeruhi sehemu kadhaa za mwili, kumfunga kamba na kumtupa mtaroni.

Ilielezwa kuwa baada ya kumfunga kamba, wahalifu hao walimdhibiti ndani ya lori na kutembea naye umbali wa kilomita moja walipofika maeneo ya Kiluvya ambako walimtupa katika mtaro na kuendelea na safari. Walifika mizani Kibaha wakapima uzito wa gari kama kawaida na kutokomea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea saa mbili usiku wakati dereva huyo akiwa kwenye foleni na lori lake aina ya Scania lililokuwa na tela pia lilikuwa na shehena ya petroli lita zaidi ya 39,000.

“Wakati dereva akiwa katika mwendo wa polepole kwenye foleni ya malori kuingia mizani, alivamiwa ghafla na watu watano waliofungua mlango na kuingia ndani.

“Wakati dereva akishangaa, walimnyanyua kwenye kiti na kumweka kiti cha nyuma na wakimtaka kukaa kimya,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

PAPA FRANCIS, WAZIRI MKUU WA ISRAEL WALUMBANA KUHUSU YESU




Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.PICHA|MAKTABA 

Malumbano makali ya maneno na hoja yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu lugha gani aliyotumia Yesu Krtisto miaka 2,000 iliyopita.

Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya siku tatu ya Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu atwae wadhifa huo. “Yesu aliishi hapa katika ardhi ya nchi hii. Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati akimweleza Papa Francis kwenye mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.

Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya mahali alikozaliwa Yesu na Ukristo. Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “Yesu alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”

“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.

Hata hivyo, mjadala huo umepokewa kwa hisia tofauti na watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia ziara ya siku tatu ya Papa Francis katika nchi takatifu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 28, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...