Dodoma. Sakata la fedha za IPTL limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wabunge kudai kurubuniwa na wenzao kwa fedha ili wakwamishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, wakidai balozi mmoja yuko nyuma ya mpango huo.
Katika sakata hilo, Sh200 bilioni zilizohifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilitolewa na kulipwa kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP), ambazo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema anachunguza akishirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto ameonya kuwa kuwaingiza
mabalozi katika sakata la ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni za IPTL ni
kuibua mgogoro wa kidiplomasia na nchi husika.
Akizungumza na gazeti hili jana, mbunge huyo alisema kuwa kiongozi yeyote atakayegundulika kufaidika na hongo hiyo, kamati yake itaweka wazi jina lake na hakuna atakayeachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Zitto alitoa kauli hiyo jana baada ya kubainika ujumbe mfupi wa maandishi (sms) unaodaiwa kusambazwa, ukifichua kile kinachodaiwa ni kuhongwa kwa baadhi ya wabunge ili wakwamishe bajeti ya wizara hiyo.
Ujumbe huo unasomeka: "Spika wa Bunge la Jamhuri, sisi wabunge waadilifu tunakiri kwamba Mhe. Mkono ametufuata na kutupatia fedha kila mmoja milioni 3 ili tukwamishe bajeti ya Nishati na Madini.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz