Sio
mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi
katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya
kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano
yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe
majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako,
hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha
yako ya mapenzi. Makala hii inaeleza
mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu,
jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.
1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:
Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa
nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza
unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha
kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza
kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala
mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili
kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz