Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba.PICHA|MAKTABA
Dar es Salaam. Kituo cha Taarifa kwa
Wananchi (TCIB), kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kubadilisha
mfumo wa uendeshaji Uchaguzi Mkuu ikiwamo kuweka kipengele
kitakachowalazimisha wagombea wa nafasi za uongozi kupima afya zao ili
kuepuka kuchaguliwa viongozi wenye maradhi yatakayowafanya washindwe
kumudu majukumu yao ya kazi.
Pia kimeitaka NEC kuweka zuio la
kufanyika kwa uchaguzi na kutoza faini kali kwa mgombea anapotangaza
kujitoa katika hatua za mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi wenyewe.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi
Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba wakati akitoa tathimini ya uchaguzi mdogo
wa udiwani uliofanyika katika Kata 27 na funzo kuelekea uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na ule wa Ubunge katika Jimbo la Kalenga mwezi ujao.
Alisema, Novemba 2012 kulifanyika
uchaguzi kujaza nafasi 29 za udiwani wakati Juni 2013 kulifanyika tena
uchaguzi katika kata 22 na mwezi huu umefanyika uchaguzi katika kata 27,
huku baadhi ya kata zikiwa tayari zimekwisharudia chaguzi zaidi ya mara
moja ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz