Rais Jakaya Kikwete ametia saini hati ya dharura (Certificate of Urgency) ili Muswada wa Fedha wa Mwaka 2013 ufanyiwe marekebisho ya
kuondoa tozo ya kodi kwa kadi za simu.
Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2012/13
lilipitisha kodi ya Sh1,000 kwa kila kadi ya simu, hatua ambayo
ilipingwa na wabunge wengi.
Ingawa wasemaji wa Ikulu hawakupatikana jana
kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete alitia saini
hati hiyo juma hili.
Ingawa wasemaji wa Ikulu hawakupatikana jana
kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete ametia saini
hati hiyo juma hili.
“Maana yake ni kuwa, muswada huo unatakiwa urudi
bungeni haraka ili uweze kufanyiwa marekebisho hayo,” alisema Makamba.
Alisema kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo, Rais alishawaagiza wadau
wanaohusika na sekta hiyo wakae na kujadili suala la kodi hizo...
“Mazungumzo hayo bado yalikuwa yanaendelea mpaka katikati ya juma hili.”