WACHUNGAJI wa makanisa mbalimbali nchini
wamemkalia kooni Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Antony Lusekelo
maarufu kama Mzee wa Upako, kwa kumtaka atoe rambirambi aliyoahidi mbele
ya umati wa watu siku ya kuaga mwili wa marehemu Askofu Moses Kulola
Temeke, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtu wa kamati iliyoratibu mazishi ya kiongozi huyo wa kanisa, viongozi wote wa dini walioahidi kutoa rambirambi hizo wametoa isipokuwa Lusekelo aliyeahidi kwa mbwembwe kutoa shilingi milioni 15.
Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Mchungaji David Mwasota alisema anamheshimu Lusekelo kwani ni mtumishi wa Mungu, lakini ni bora angetimiza ahadi yake kama walivyofanya wenzake.
“Mzee wa Upako ni mtu mwenye jina kubwa kwenye jamii na kwa Mungu, hivyo anapaswa kuangalia kwa undani kile anachoahidi kwa muda unaotakiwa na amuache mke wa marehemu apumzike kwa kuwa ametokwa na mpendwa wake na bado hana nguvu,” alisema na kuongeza;