Habari zilizopatikana Mjini Dodoma jana na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge pamoja na Ikulu, Dar es Salaam zinasema atahutubia mchana.
Kutokana na ujio huo, Serikali imewaelekeza Mawaziri na Manaibu Waziri kutotoka nje ya Dodoma hadi hapo Rais atakapokuwa amehutubia Bunge.
Kadhalika safari zote za Kamati za Bunge ambazo zilikuwa katika mchakato wa kutekelezwa zimeahirishwa hadi baada ya kesho, ili kutoa fursa kwa wabunge wote kuwapo wakati wa hotuba hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana kuwa hata yeye amesikia taarifa kuwa Rais atazungumza bungeni lakini hajui atazungumza kitu gani... "Hata mimi nimesikia kuwa atazungumza lakini sijui atazungumza jambo gani kwa kuwa siyo miongoni mwa watu wanaomwandalia hotuba," alisema Balozi Sefue.
Kadhalika, Mkurugenzi wa Mawasiliano
Ikulu, Salva Rweyemamu alithibitisha kuwa Rais Kikwete atalihutubia
Bunge, Alhamisi... "Nathibitisha ni kweli, ila kwa taarifa nyingine
watafuteni watendaji wa Bunge, kama Katibu wa Bunge nadhani wana taarifa
zaidi."