MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf
Mehboob Manji amesema hakuna mgawanyiko ndani ya klabu hiyo na habari
kwamba Seif Ahmed 'Magari' ametengwa ni uzushi, lakini habari za ndani
kutoka kwenye klabu hiyo zinasema uongozi unaamini unahujumiwa na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kumekuwa na habari kwamba Seif Magari ameondolewa katika sehemu ya uongozi wa klabu na kwa sababu hiyo, hata swahiba wake, Abdallah Ahmed Bin Kleb ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, naye amejitoa pia.
"Hakuna mgawanyiko, hayo ni maneno tu, Seif yupo na Majjid (Suleiman) wote tupo nao. Na hatuna wasiwasi na ligi, Simba SC inaongoza inatuzidi pointi tano tu.
Tumefungwa na Azam FC kwa bahati
mbaya, sisi ndio tulicheza mpira mzuri na kila mtu ameona,"alisema Manji.