Baada ya Ney Wa Mitego kutoa Track ya Salam Zao, Kuna tetesi Kuwa
Muandaaji wa BSS Madam Rita anampango kumfungulia Kesi ya Madai Ney wa
Mitego kwa Kumchafua (Defamation)
kwani eti alisema Madam Rita huwa
hatoi zawad anazoziahidi kwa washindi wa shindano
lake la kusaka Vipaji, Je Kama ni kweli kuhusu Kesi hii Ney wa mitego
ataweza kulipa milioni 500? Tayari msanii huyo amesema yuko tayari
kwenda mahakamani na ataweka mwanasheria wa kumtetea.
Thursday, August 22, 2013
HII NDO KAULI KUTOKA KWA NDUGU WA AGNES MASOGANGE, KUHUSU NDUGU YAO KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli. “Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema ndugu huyo.
Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.
Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange mwenyewe miaka ya nyuma alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kupitia safu ya Ten Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:
TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, walokole, wao wanachukuliaje suala la wewe kuingia kwenye mambo ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?
WATUMISHI WA ZAHANATI WATUHUMIWA KUFANYA MAPENZI NA WAGONJWA.
WATUMISHI wawili katika zahanati ya Mwanhala wilayani Nzega, wamekumbwa na kashfa ya kufanya mapenzi na wagonjwa hospitalini.
Kutokana na kashfa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bitun Msangi, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa watumishi hao.
Agizo la mkuu huyo limetolewa hivi karibuni, baada ya Diwani wa kata ya Utwigu, Sawaka Shita kuwalalamikia watumishi hao mbele ya Baraza la Madiwani, kwa kukithiri kufanya mapenzi na wagonjwa nyakati za kazi, licha ya kuonywa kwa mara kadhaa.
Diwani huyo aliliambia baraza hilo kuwa vitendo hivyo vina hatarisha maisha ya watumishi hao na ya wananchi, hususani waliotembea nao na kutishia kuvunja ndoa za wananchi.
Alidai kuwa taarifa hizo za malalamiko, zilishafika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, tayari kwa utekelezaji, lakini wananchi wa kata hiyo walitaka kuifunga zahanati hiyo, baada ya kukithiri vitendo hivyo vya kufanya mapenzi katika wodi zilizopo.
MKE AFUMANIWA AKILIWA URODA CHOONI NA RAFIKI WA MUMEWE
Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Juma, mkazi wa Tegeta A, Dar amejikuta akikamuliwa faini ya Sh. laki tano kufuatia kufumwa ugoni na mke wa mtu.
Katika tukio hilo lililojiri Kimara-King’ong’o, Dar, Jumapili iliyopita, Juma alifumaniwa na mke wa mwanaume aitwaye Swai aliyetajwa kwa jina moja la Cesilia, mkazi wa maeneo hayo.
Ilidaiwa kuwa Cesilia alimwachia mumewe mtoto na kumuaga kuwa anakwenda harusini ambapo mumewe alimkubalia bila kujua kumbe anakwenda kuzini.
Ilisemekana kuwa muda mfupi baadaye, kuna vijana walimfuata Swai na kummwagia ‘upupu’ kuwa mkewe alikuwa akisaliti ndoa yao.
Ilifahamika kuwa vijana hao walimchukua Swai na kumpeleka hadi kwenye nyumba ambayo wenyewe hawajahamia iliyopo karibu na biashara yao ya duka ambapo baada ya mwenye mali kuingia, alimkuta Juma akiwa amevaa ‘singlendi’ na bukta ambapo alizidi kuangaza macho huku na kule ili amuone mkewe.
RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAKE.... !!!
Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:
- Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
- Joyce Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
RWANDA NA UGANDA WAJITOA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.
Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.
“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”
Wednesday, August 21, 2013
ALHAJ MWINYI NA MZEE MKAPA WAWASILI ZIMBABWE KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS MUGABE
Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan
Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na
Mama Anna Mkapa, wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere kuelekea Harare, Zimbabwe, kushiriki katika sherehe ya kuapishwa
kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho
Alhamisi Agosti 22, 2013
Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan
Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na
Mama Anna Mkapa, wakiwasili katioka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Harare, Zimbabwe, walikoalikwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa
Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho
Alhamisi Agosti 22, 2013.PICHA NA IKULU
MADIWANI BUKOBA: TUKO TAYARI KUHAMIA CHADEMA....!!!
MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofukuzwa katika Manispaa ya
Bukoba, wamesema wako tayari kujiunga na Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kama chama chao kitaendelea na msimamo wa
kuwafukuza. Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, mmoja wa madiwani
hao (jina na kata yake tumevihifadhi), alisema wako tayari kuhamia
Chadema muda wowote kama hawatarudishiwa uanachama wao.
Alisema, madiwani wote waliofukuzwa wana msimamo mmoja, ambapo wanasubiri vikao vya Kamati Kuu ya CC ili wajue hatima yao, lakini vikishindwa kuwarudisha kwenye chama, watahamia Chadema ili kuendeleza harakati zao walizozianzisha.
Alisema, wanachokifanya wao ni kutetea maslahi ya taifa na wananchi waliowapigia kura na si kulinda biashara za watu binafsi, hata kama wanaungwa mkono na uongozi wa juu wa CCM.
Msimamo huo wa madiwani umekuja siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kuwakaribisha madiwani hao katika chama chake na kusema wako tayari kuwafundisha siasa za mageuzi.
Alisema, madiwani wote waliofukuzwa wana msimamo mmoja, ambapo wanasubiri vikao vya Kamati Kuu ya CC ili wajue hatima yao, lakini vikishindwa kuwarudisha kwenye chama, watahamia Chadema ili kuendeleza harakati zao walizozianzisha.
Alisema, wanachokifanya wao ni kutetea maslahi ya taifa na wananchi waliowapigia kura na si kulinda biashara za watu binafsi, hata kama wanaungwa mkono na uongozi wa juu wa CCM.
Msimamo huo wa madiwani umekuja siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kuwakaribisha madiwani hao katika chama chake na kusema wako tayari kuwafundisha siasa za mageuzi.
GODBLESS LEMA AUGUA GHAFLA, KESI YAKE YAHAIRISHWA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha jana imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kutokana na mbunge huyo kuwa mgonjwa.
Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Hawa Mguruta, anayesikiliza shauri hilo kuwa Lema anaumwa na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya AICC tangu Agosti 14 hadi 19, mwaka huu aliporuhusiwa kutoka hospitali, hivyo ametakiwa apumzike kwa muda wa siku 10 kuanzia Agosti 19, mwaka huu.
Wakili Kimomogoro aliomba shauri hilo liahirishwe hadi siku nyingine, ombi lililokubaliwa na hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 1 na 2 mwaka huu, ambapo mashahidi tisa wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.
DIAMOND NAE ATAJWA SAKATA LA UNGA....!!!
*Utajiri, safari zake nje ya nchi vyatiliwa shaka
*Ahusishwa na mtandao hatari wa Masogange
KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’
Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.
Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.
Kama hiyo haitoshi, safari za nje ya nchi za mwanamuziki huyo unaohusisha ziara zake nchini Afrika Kusini na Uingereza, pia ni mambo ambayo yamechochea wingu la mashaka lililofikia hatua ya jina lake kuingizwa katika mtandao huo ambao katika siku za karibuni, umewagusa pia baadhi ya watu wenye majina makubwa katika jamii.
PONDA AIGHARIMU SERIKALI MILIONI 10...!!!
*Usafiri wa helikopta waitafuna dola mara 71 ya gharama ya gari
ULINZI wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiwa gerezani na anapopelekwa mahakamani, umeanza kuvitesa vyombo vya Dola. Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, zinaeleza kuwa serikali juzi ilitumia kiasi cha shilingi 10,682,031 kama gharama za usafiri wa helikopta za kumpeleka na kumrudisha kiongozi huyo mahakamani mkoani Morogoro.
MTANZANIA Jumatano kupitia vyanzo vyake vilivyoko ndani na nje ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 hadi saa moja ni dola za Marekani 3,000 hadi 3,300 ambazo ni sawa na shilingi 5,341,032.85 .
Hivyo gharama za kwenda na kurudi kwa saa jumla yake ni dola za Marekani 6,600 ambazo ni sawa na shilingi 10,682,031.
Akithibitisha hilo, Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, Antony Mwami alisema gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 ni dola 3,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni tano.
TSVANGIRAI ATUHUMIWA KUDHARA MAHAKAMA...!!!
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tvangirai anakabiliwa na makosa ya kudharau mahakama kufuatia matamshi aliyoyatoa kuhusiana na idara hiyo.
Jaji wa mahakama kuu Chinembiri Bhunu amesema waendesha mashtaka watafahamishwa kuhusu tuhuma hizo. Haya yanajiri wakati chama cha Tsvangirai cha Movement For Democratic Change kimepoteza kesi mbili kulalamikia uchaguzi mkuu wa Julai 31 mwaka huu.
P.T
Mahakama ya kikatiba ilitangaza kwamba Rais Robert Mugabe alishinda uchaguzi kwa njiya huru na haki. Mugabe alipata asili mia 61 ya kura dhidi ya asili mia 34 alizopata Bw. Tsvangirai.
Viongozi hao wamekuwa katika utawala wa kugawana madaraka ulioafikiwa mwaka 2009 kufuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata. Chama cha MDC kiliondoa kesi yake mbele ya mahakama ya kikatiba kikisema hakikua imani ya kupata haki.
Subscribe to:
Posts (Atom)