Thursday, August 01, 2013

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 1, 2013

DSC 0051 066d6
DSC 0052 9dfcf

JUMA KASEJA APATA DILI KUBWA KONGO...!!!

Mlinda mlango wa Taifa Stars Juma Kaseja
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Juma Kaseja amesema kwamba amefanya mazungumzo tu na wakala wa klabu ya St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini bado hajaingia Mkataba na klabu hiyo ya Lubumbashi.

Akizungumza jana mchana, Kaseja amesema kwamba mtu aliyejitambulisha kwake kama wakala wa Lupopo alimfuata wakafanya mazungumzo na kufikia makubalino juu ya dau la usajili, mshahara na mambo mengine ya msingi.

Hata hivyo, kipa huyo namba moja Tanzania amesema kwamba baada ya mazungumzo hayo na maafikiano, wakala huyo amepeleka majibu Lupopo ambao wakiafiki ndipo masuala ya Mkataba yatafuatia.

MUSWADA WA SUALA LA KODI YA SIM CARD KURUDISHWA BUNGENI AGOSTI

Waziri wa Fedha, , Dk. William Mgimwa amenukuliwa kwenye magazeti ya NIPASHE na HabariLeo matoleo ya leo akisema kuwa Serikali sasa imekubali kuwa kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na hivyo inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioazisha kodi hiyo wenye mkutano wa Bunge mwishoni mwa mwezi wa Agosti kwa mjadala zaidi na ufumbuzi kutoka kwa Wabunge.

Wiki iliyopita Rais Jakaya Kikwete alikutana na Wizara hiyo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wajumbe wa MOAT (Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Simu -  TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel)  Ikulu kusikia pamoja na mambo mengine, kuondolewa kwa kodi ya simu kutakavyokwaza maendeleao ya sekta ya mawasiliano na kuwataka MOAT kutoa mapendekezo ya jinsi serikali itapata kiasi cha Sh. bilioni 178 zilizopangwa kupatikana katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2013/14 kutokana na kodi ya simu.

VYAKULA VYA MAFUTA NI CHANZO CHA KUKUKOSESHA USINGIZI

baga

Tumekuwa tukipokea maoni toka kwa watu wengi juu ya matatizo ya kukosa usingizi, ingawa kuna sababu nyingi zinazoweza kukufanya ukose usingizi kama magonjwa nk, ila mlo nao ni moja ya sababu hizo.Na moja ya vyakula hivi ni vile vyenye mafuta (fat) mengi kama burger, chipsi nk. Tafiti zinaonesha kuwa, vyakula hivi sio tu hukufanya uongezeke uzito bali pia huabiri mfumo wa kulala.

Tafiti zinaendelea kuwa, vyakula hivi vizito huamsha mfumo wa usagaji vyakula (digestion system) na kuifanya ianze kufanya kazi, hii hukupelekea mwili wako kuwa hai na pia hukufanya mara nyingi kujisikia kwenda haja hivyo kukukosesha usingizi. 
Hivyo basi epuka kula mlo wenye wanga mwingi wakati wa usiku au angalau kwa masaa mawili kabla ya kwenda kulala.

Wednesday, July 31, 2013

MWANASHERIA KUISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU KRISTO...!!

dola
Maajabu mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee . Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo .
Mwanasheria huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Jesus-Christ-Wallpapers-3Mwanasheria huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia yoyote ya kustahili adhabu hiyo . 

Dola Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua Bwana Yesu .

FAHAMU KWANINI UNATAKIWA KUZIFANYA NDIZI KUWA SEHEMU YA MAISHA YAKO.


banana-amazing-fruit-and-cureNdizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku moja .

Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose , Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako .

Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika .
Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili lina faida nyingine ambayo ni kuusaidia mwili wako kupambana na kujikinga na maradhi  kadhaa.

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU MWAKA WA MASOMO 2013/2014 HAYA HAPA



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr Shukuru kawambwa. 
---
Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.

Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.
---

MAELEKEZO MUHIMU:

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 15/08/2013.

ZIDANE AWAFUNGUKIA SPURS, AWATAKA WAMPE NAFASI YA KUCHEZA REAL MADRID KUTIMIZA NDOTO ZAKE



 Touch down: Gareth Bale arrives at Heathrow Airport from Hong Kong in the early hours  
Gareth Bale alipokuwa akiwasili uwanja wa  Heathrow akitokea Hong Kong  baada ya kupata majeruhi
Nothing to smile about: Bale, who may be subject of a world record £85m bid from Real Madrid, clearly has a lot on his mind on his return to London 
Hakuna tabasamu: Bale, anaweza kuwa mchezaji ghali zaidi duniani akimzidi Ronaldo kama dili la usajili wake wa pauni milioni 85 litakamilika kwenda Real Madridi, lakini wakati akiwasili London alionekana kuwa na mawazo mengi kichwani mwake.
Zidane alisisitiza kuwa : “Kama mchezaji ameonesha nia ya kujiunga na Madrid, basi Tottenham wampe ruksa ya kuzungumza na sisi. Nafasi ya kuichezea Real Madrid huwa inatokea mara moja katika maisha ya mchezaji na inaeleweka kuwa Gareth Bale hataki kukosa nafasi hii muhimu”.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 31, 2013

DSC 0005 ea013
DSC 0006 f6d17

AFYA YA MANDELA YAZIDI KUIMARIKA

051 86464

RAIS mstaafu nchini Afrika Kusini , Nelson Mandela aliyelazwa hospitalini tangu tarehe nane mwezi Juni, anaonyesha dalili za afya yake kuimarika.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa serikali. Hata hivyo Mandela mwenye umri wa miaka 95 angali hali mahututi ambayo inadhibitiwa na madaktari.

Rais Jacob Zuma amewataka watu kuendelea kumuombea Mandela na kuwashukuru wale waliotenda mema kwa niaba ya Mandela. (HM)

Mandela ambaye ni rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia, anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa.

Alifungwa jela miaka 27 baada ya kuanzisha vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Anajulikana na ukoo wake kwa jina Madiba, na alichaguliwa kama rais wa Afrika Kusini mwaka 1994 baada ya wazungu kumaliza utawala wao na kisha akaondoka mamlakani baada ya miaka mitano ya kutawala nchi.

Katika taarifa yake, bwana Zuma alitoa wito kwa wafanyabiashara kuunga mkono mradi unaofadhiliwa na wakfu wa Mandela kujenga hospitali ya watoto.
"Madiba anapenda sana watoto, na anawatakia afya nzuri. Anatutaka tuhakikishe kuwa wanaishi maisha mazuri katika siku za baadaye,'' alisema Zuma.
Wakfu wa Mandela , ungependa kujenga hospitali yenye uwezo wa kuwashughulikia watoto 238 wa kulazwa pamoja na kuwatibu watoto kote nchini Afrika Kusini. Chanzo: bbcswahili

UN: VIFO VITOKANAVYO NA HIV VYAPUNGUA AFRIKA

hiv 8da7b

UMOJA wa Mataifa umetangaza kwamba Afrika imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Vifo vinavyotokana na maradhi ya Ukimwi Mashariki na Kusini mwa Afrika vimepungua kwa asili mia 40.

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi- UNAIDS umehusisha hatua za sasa na kutolewa kwa dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi. (HM)

Umoja wa Mataifa umesema mataifa ya Botswana, Ethiopia, Kenya, Zambia na Zimbabwe yamepunguza idadi ya watu wanaokufa kwa ukimwi kwa zaidi ya nusu.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa Maradhi nyemelezi ya kifua kikuu pia yamepungua sana tangu mwaka 2005. Chanzo: bbcswahili

Tuesday, July 30, 2013

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA URU LAKUMBWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA


HOFU kubwa imetawala Kanisa Katoliki Parokia ya Uru iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea kutokea katika kanisa hilo huku baadhi ya watu wakiyahusisha na imani za kishirikina. 

  Katekista wa parokia hiyo, Lucian Tesha, aliwaambia waamini waliokusanyika katika ibada ya misa ya kwanza kanisani hapo juzi Jumapili kuwa usalama katika kanisa hilo upo shakani na kuwataka kuwa macho.

Hali hiyo inatokana na kile alichodai kuwa kuna mtu mmoja (mwanaume) kwamba amekuwa akionekana eneo la kanisa akiweka vitu mbalimbali ambavyo havina nia njema na kanisa hilo la Moyo Mtakatifu wa Yesu.
 
“Mtu huyu ameonekana kanisani hapa kwa mara ya nne sasa, hatujui anataka nini, lakini amekuwa akiweka vitu mbalimbali katika sanamu ya Bikira Maria na karibu na sakristi ya mapadri…kwa kweli hali hii inatisha.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAWACHANA CHADEMA...!!!


 
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina ubavu wa kumkataa au kutomtambua John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasai, Rajab Baraka alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliyedai chama hicho hakimtambui John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa.

Katika madai yake Dk. Slaa alidai Tendwa anakipendelea CCM katika kutoa haki ya demokrasia na hatendi haki kama mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini.

Dk. Slaa alisema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kusisitiza hata katika barua zao za mawasiliano kwenda kwa ofisi ya msajili chama hicho hakitumii jina la John Tendwa.

MSHIRIKI WA BBA...... "NIMELALA NA WANAUME MATAJIRI KWASABABU YA PESA ZA KUHUDUMIA FAMILIA YANGU"

It seems Beverly Osu no longer remember that cameras and microphones are everywhere in the Big Brother Africa house and as such whatever she says or do will being captured and transmitted to viewers. That could only explain why she revealed her top secret to her in-house lover, Angelo, without thinking twice in one of their recent get together sessions. Talking about her "runs" life in Lagos, Beverly said:
"I’ve done all sorts. I’ve slept with men for money when I had to take care of my family." We observed that it was also in the Big Brother house that Beverly revealed the fact that she had once aborted a four-month old pregnancy she had for her estranged boyfriend.
Beverly also confirmed that she once dated singer 2shotz, but the newly married singer is denying her.

VIWANGO VIPYA VYA MISHAHARA YA WATUMISHI WA SERIKALI 2013.

TGOS A
TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS A 3. (Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A 6. (Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A 9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A 12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh 318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A 18(Sh335,200).
TGOS B
TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B 3 . (Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B 6. (Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9. (Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11 . (Sh442,000) na TGOS B 12. (Sh451,500).
TGOS C
TGOS C 1 . (Sh471,000), TGOS C 2 . (Sh482,000), TGOS C 3 . (Sh493,000), TGOS C 4. (Sh504,000), TGOS C 5. (Sh515,000), TGOS C 6. (Sh526,000), TGOS C 7. (Sh537,000), TGOS C 8. (Sh548,000), TGOS C 9. (Sh559,000), TGOS C 10. (Sh570,000), TGOS C 11. (Sh581,000) na TGOS C 12. (Sh592,000).

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...