SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh 1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika lakini pia inaangalia utaratibu wa kufanya makato hayo kwa njia ambayo haitamuumiza mtumiaji wa simu.
Akizungumza
jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa alisema
kuwa kupitia tozo hizo wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa mwaka.
“Kupitia
wawakilishi wenu na sisi serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na
ikaonekana kwamba kuna uwezekano wa kupata chanzo kingine cha mapato
kupitia kadi za simu”alisema.
Alisema
katika mapendekezo yaliyokuwa yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh
1,450 katika kila kadi ya simu lakini baada ya kukaa na kushauriana
serikali iliona ni vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila mwananchi aweze
kumudu gharama ambapo kwa mwaka kila mmiliki wa kadi ya simu atatozwa sh
12,000.