USHUHUDA WA SUGU
Ukweli
wa jinsi matajiri wauza unga wanavyowatumia wanamuziki wa Kitanzania
kama punda, unapewa nguvu na ushuhuda aliowahi kuutoa Mbunge wa Mbeya
Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Mbunge huyo ambaye anapewa
heshima kwamba ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva, alimweleza mwandishi
wetu kuwa kabla hajawa memba wa jumba hilo la kutunga sheria, aliwahi
kufuatwa na wauza unga kumshawishi awe anabeba mzigo kwenda nao nje ya
nchi.
“Jamaa waliniambia kwa sababu mimi nasafiri safiri sana, passport
(hati ya kusafiria) yangu itakuwa imeshagongwagongwa sana, kwa hiyo ni
rahisi kwenda nchi tofautitofauti kwa urahisi, kwa hiyo wakataka niwe
nabeba unga. “Kigezo cha pili waliona kwa sababu mimi ni mwanamuziki,
kwa
hiyo ni rahisi watu kuamini ziara zangu ni za kimuziki. Nilikataa,
niliwaambia siwezi kufanya biashara hiyo kabisa,” alisema Sugu.
Mwaka
2011, mbunge huyo aliwahi kugusia hilo, wakati akitoa hoja kuchangia
bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa serikali
ni lazima iwasaidie wanamuziki wa Kitanzania kwa sababu wanaibiwa sana,
hivyo kuwafanya vijana kuona kimbilio rahisi la kutajirika ni kuuza
madawa ya kulevya. “Mheshimiwa spika, serikali isifanye ili kijana wa
Kitanzania afanikiwe lazima auze unga, madawa ya kulevya,” alisema Sugu
na kueleza mfano huo wa jinsi alivyofuatwa kushawishiwa na matajiri wa
unga ili naye awe punda.