Sunday, June 02, 2013

DEREVA MWANAMKE WA BASI LA NDENJELA COACH AWA KIVUTIO KWA ABIRIA

DEREVA NUSURA MAGULUKO 28 AKIMWOMBA MUNGU KABLA YA KUANZA SAFARI
SASA HAPA YUPO KAZINI
BAADHI YA ABIRIA WAKIFURAHIA MWENDO MZURI WA DEREVA NUSURA MGULUKO

ABIRIA WAKIPATIWA HUDUMA YA VITAFUNWA NDANI YA BASI HILO LA NDENJELA

MISS SHINYANGA CENTRE APIGWA NA KUNYANG'ANYWA PESA NA MUANDAAJI WA SHINDANO HILO BAADA YA KUKATAA KUONDOKA NAE....!!!

 



Na Mwandishi wetu Steve Kanyeph
Mashindano ya kumtafuta mrembo Shinyanga yaani Miss Shinyanga Centre yamemalizika huku yakiingiwa dosari baada ya mshindi wa taji hilo SCOLASTIKA SITTA{19} kutoa malalamiko kuwa amedhalilishwa kwa kupigwa na kunywanganywa pesa kiasi cha shilingi laki 3 alizopewa ikiwa ni zawadi
mrembo huyo amesema tukio hilo limefanywa na muuandaaji wa mashindano ya miss Shinyanga ASELA MAGAKA baada ya mrembo huyo kukataa kuondoka kwenda Kahama usiku wa manane.

“Alitaka tuondoke baada ya kushuka jukwaani na twende Kahama kwaajiri ya kambi ya miss Shinynga usiku huo huo mimi nikakataa kwa sababu ilikuwa ni usiku sana na baada ya hapo akapanick akanipiga makofi na kuninyang'anya pesa zote shilingi laki 3”.Alisema mrembo huyo.




Mrembo huyo amesema kitendo hicho ni cha udhalilishaji na kimemkatisha tamaa ya kuendelea kushiriki mashindano kwa ngazi ya mkoa na amekwenda kutoa taarifa polisi na taratibu za kisheria zinaendelea.
Scolastica anatoa ushauri kwa waandaaji wa mashindano ya urembo kutowadhalilisha washiriki na kwamba warembo wanatakiwa kuwa imara na jasiri katika kudai haki zao na kupinga vitendo vya udhalilishaji kwani mashindano ya urembo yanakabiliwa na changamoto nyingi.

WANYARWANDA WANASWA WAKIJIUZA JIJINI DAR


POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanikiwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi...Kamatakamata hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo Kariakoo, jijini Dar ambalo machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa wateja.


Katika hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa na makahaba hao ilitimua mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria kusafisha eneo la Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.

Baadhi ya wanaume wakati wakitimua mbio walisikika wakisema kuwa wakukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola ni wanawake hao kwa vile wanavaa kimitego huku wakijua binadamu anapitiwa na shetani wakati wowote.


“Sisi kosa letu nini? Wakamateni haohao machangudoa, watavaaje kimitego mbele yetu sisi wanaume? Shetani naye atakuwa wapi wakati huo?” alisikika akisema mmoja wa wanaume hao huku akichanganya miguu kupita kawaida.
Awali kabla ya zoezi la kuwanasa makahaba hao halijaanza, afande mmoja alipowauliza wanachofanya hapo, kahaba mmoja aliuliza: Una maswali mengi kwani we ni polisi?

Mei 24, mwaka huu, makahaba hao walipandishwa kwenye Mahakama ya Jiji na kusomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka, John Kijumbe mbele ya Hakimu Timoth Lyoni.

Waliosomewa mashitaka ni Natasha Bahati, 30 (Mrundi), Asma Athuman, 23 (Mrundi), Niyonkuru  Evelinde, 29 (Mnyarwanda), Zaimana Hawa, 20 (Mrundi) na Wabongo 35.
Wote walikana mashitaka lakini walipelekwa Gereza la Segerea, jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

WAZIRI MKUU ACHARUKA KASI NDOGO YA UJENZI WA BARABARA RUKWA

20120913_164754
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 *Afanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya wajenzi wa Kichina
*Aahidi kumtuma Waziri Magufuli kufuatilia, ataka mkandarasi aongeze kasi, awe makini
*Amtaka RC Rukwa aunde timu ya kumpatia ripoti kila mwezi
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda jana jioni (Jumamosi, Juni Mosi, 2013) alilazimika kufanya ziara ya ghafla kwenye kambi ya wajenzi wa barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni ili kupata maelezo ni kwa nini kazi hiyo inasusua na haionyeshi kuendelea.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa akitoka Namanyere, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Rukwaalilazimika kusimama kwenye kambi hiyo ya wajenzi iliyopo Paramawe, wilayani Nkasi.

Wasemavyo wasanii kuhusiana na kifo cha Ngwea

Kutokana na kifo cha msanii Albert Mangwea ambaye amefariki nchini Afrika ya Kusini ambako alikwenda kufanya maonyesho, wasanii mbalimbali  wamezungumzia kifo chake.
Ni dhahiri, Albert Mangwea alikuwa katika kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya nchi na ndiyo uhai wake ulikopotea, Mwandishi wetu Kalunde Jamal aliongea na baadhi ya wasanii wenzake na maongezi yakawa kama ifuatavyo:
Joseph Haule a.k.a Profesa Jay
Anasema katika hili hakuna jinsi kwa kuwa kila binadamu atayaonja mauti.
“Inaniuma sana lakini sina cha kufanya kwa kuwa ni kazi ya Mungu na kazi yake haina makosa, kinachotakiwa ni kumuombea apumzike kwa amani  huko aendako.         
Selamani Msindi ‘Afande Sele’
Anasema anamtambua Ngwea siyo kama msanii bali ni mdogo wake wa karibu na ameshindwa kujizuia kutoa machozi kuhusiana na kifo hicho.
Anaongeza kuwa katika kuonyesha ni kwa jinsi gani kijana huyo alikuwa na mapenzi na watu kwani kwao ni Morogoro lakini alijulikana ni kijana wa Dodoma almaarufu East Zoo.
Ngwea kapambana na muziki ukiwa hauna mbele wala nyuma kapambana kuhakikisha unakuwa bora lakini kwa sasa ndiyo unatambulika baada ya kufanya jitihada za kila aina kuufanya uwe ulivyo.”
“Sidhani kama atanitoka kichwani kwangu, naona kama ametutoroka kwa kuwa hatuhitaji aondoke muda huu lakini hakuna jinsi tutakutana naye siku ya mwisho na nitamweleza machungu yangu na kwa jinsi gani kifo chake kimeniumiza,” anasema.
Snura Mushi ‘Snura’
Anasema anasikitika sana hasa kwa wao ambao ndiyo kwanza wameingia kwenye muziki na walitaka kujifunza mengi kutoka kwa wasanii wanaofanya vizuri kama Mangwea, lakini kwa bahati mbaya au nzuri Mungu amechukua kiumbe chake hakuna cha kufanya kupinga hilo kwani haliwezekani.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 2, 2013

4 aaa9f
1 802eb
2 2b5a3

Saturday, June 01, 2013

SERIKALI YAOMBELEZA KIFO CHA MANGWEA

untitled25 a7fc8
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA
BW. ALBERT MANGWEA, (Man Ngwair)
1/06/2013.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne tarehe 28 Mei, 2013.Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya "Free Style" alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi.
Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.
Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.
Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
"Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangwea mahala pema peponi."
Imetolewa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara

ALICHOKISEMA DIAMOND KUPITIA MTANDAO WAKE WA INSTAGRAM KUHUSU MAREHEMU ALBERT MANGWAIR

Hali ya huzuni ikiwa imetanda juu ya nyuso za mamilioni ya
watanzania baada ya msiba mzito
uliotufikia Ghafla kwenye Tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya......
Tumesikia Producers,wanamuziki mbalimbali na watu mbalimbali
wakifunguka na kuongea lolote
juu ya marehemu Albert Mangweha....
Kupitia Mtandao wake wa Instagram bado
Mwanamuziki Diamond Platnumz
akiwa kwenye hali ya kutokuamini
kilichotokea muda mchache uliopita aliweza kufunguka
juu ya matarajio yake ya kufanya kazi za uhakika
na marehemu Albert Mangweha.......
Muda mchache uliopita alitupia kupitia mtandao wake wa
Instagram Picha hii chini akiwa ameiandikia
maneno haya''Kinachoniuma zaidi ni jinsi tulivyokua
tukijaribu kutengeneza HIT bila Mafanikio... si kwa
nyimbo niliyokushirikisha wala uliyonishirikisha, zote
Hazikufikia Malengo yetu na Kuplan kufanya Ngoma Mpya
 Ukirudi toka South Africa.... bt pia kwa Mipango ya
Mwenyez Mungu Haijawezekana... RIP Brother, i will
 always miss and Respect you....''

Ayo ndio maneno aliyoandika Msanii Diamond Platnumz....
R.I.P ALBERT MANGWEHA....

HILI NDILO TAMKO RASMI LA PUSH MOBILE NA BONGO RECORDS KUHUSU MAUZO YA NYIMBO ZA MANGWEAR KWENYE SIMU

Hili ndilo Tamko Rasmi la Push Mobile na Bongo Records Kuhusu Mauzo ya Nyimbo za Mangwear Kwenye Simu

DAKTARI AKIRI NGWEA KAFA KWA KUNYWESHWA SUMU, ADAI KUWA ALITOKWA NA DAMU NYINGI SANA PUANI WAKATI AKIKATA ROHO..!!

KIFO cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika.
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo) alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa kwenye Mochwari ya Hillbrow.

M2 The P akiwa amelazwa Hospitali
Mbongo huyo alisema alifanikiwa kuutazama mwili wa marehemu Ngwea ambapo ulionesha kuwa wakati wa kukata roho damu nyingi zilimtoka kupitia puani na mdomoni kiasi cha kuwashangaza wauguzi.
 

NI SUMU
Alisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimtibu mshirika wa marehemu, Mgaza Pembe a.k.a M2 The P aliyenusurika, alimwambia wawili hao walionekana kuingiwa na kitu cha hatari na kibaya sana mwilini jambo lililowashtua hata madaktari wenyewe.


Alisema muuguzi huyo alimweleza kuwa kitu walichokula au kulishwa kiliwadhuru sana ndani ya miili yao na kusababisha mishipa ya damu kwa Mangwea kupasuka hovyo kwa kuwa moyo ulizidiwa na presha ya msukumo wa damu.
Mtanzania huyo alidai kuwa hata kama kweli wawili hao walichanganya vileo kama watu wanavyodai, basi ule mchanganyiko ndiyo uliotengeneza sumu mwilini akisisitiza kuwa hilo halina shaka kwa mujibu wa muuguzi huyo.
“Unajua kuna watu wanapenda kuchanganya pombe kali kwa hiyo kuna wanaodai wawili hao walichanganya ‘unga’, bangi na pombe kali.

HAWA NDO WANAFUNZI BORA KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA MTIHANI WA CSEE 2012
NECTA'S LOGO

 1. Watahiniwa Kumi (10) bora Kitaifa:
NAFASI
NAMBA
JINA
JINSI
JINA LA SHULE NA MKOA
1
S0189-0063
SAID JUMA IRANDO
M
FEZA BOYS'   S  S  (DAR ES SALAAM)
2
S4459-0028
ALEX  ELIFAS
M
JUDE MOSHONO   S   S  (ARUSHA)
3
S0189-0039
JASPER GEOPHREY KAJIRU
M
FEZA BOYS'   S  S   (DAR ES SALAAM)
4
S2549-0086
MOSES J BOSCO
M
ALPHA SECONDARY    S  S (DAR ES SALAAM)
5
S4213-0074
YOHANA L MAYENGA
M
MARIAN BOYS' S   S  (PWANI)
6
S0239-0072
NGUSE  NGULUMBI
F
ST. FRANCIS GIRLS   S   S  (MBEYA)
7
S4213-0044
JOSHUA Z AZZA
M
MARIAN BOYS'  S    S  (PWANI)
8
S0189-0062
SAID ATWAYA NCHIMBI
M
FEZA BOYS'   S  S   (DAR ES SALAAM)
9
S0867-0134
LUPYANA L KINYAMAGOHA
M
PANDAHILL   S   S  (MBEYA)
10
S0101-0350
PETER SEREKA KICHOGO
M
AZANIA    S   S  (DAR ES SALAAM)

2.    Wasichana Kumi (10) bora Kitaifa
NAFASI
NAMBA
JINA
JINA LA SHULE NA MKOA
1
S0239-0072
NGUSE  NGULUMBI
ST. FRANCIS GIRLS   S  S   (MBEYA)
2
S0239-0078
SAMMOTA  CHUNGU
ST. FRANCIS GIRLS   S   S  (MBEYA)
3
S0239-0075
RAHMA  MKWATA
ST. FRANCIS GIRLS   S    S (MBEYA)
4
S0239-0018
DIANA  MGAYA
ST. FRANCIS GIRLS  S  S  (MBEYA)
5
S1060-0066
REBECCA J MWAMBEGELE
ST.MARY'S   S   S (DAR ES SALAAM)
6
S0239-0010
BELDA  THOMAS
ST. FRANCIS GIRLS  S   S  (MBEYA)
7
S0239-0002
AGNES  NTAPARA
ST. FRANCIS GIRLS   S  S  (MBEYA)
8
S0248-0045
JOANGELINE J BAMWENZAKI
MARIAN GIRLS   S  S   (PWANI)
9
S0298-0011
FATMA M MOSHI
FEZA GIRLS' S  S   (DAR ES SALAAM)
10
S0239-0045
JESCA  CHENGULA
ST. FRANCIS GIRLS   S  S  (MBEYA)

  1. Wavulana Kumi (10) bora Kitaifa
NAFASI
NAMBA
JINA
JINA LA SHULE NA MKOA
1
S0189-0063
SAID JUMA IRANDO
FEZA BOYS'   S    S  (DAR ES SALAAM)
2
S4459-0028
ALEX  ELIFAS
JUDE MOSHONO   S  S   (ARUSHA)
3
S0189-0039
JASPER GEOPHREY KAJIRU
FEZA BOYS'S   S   S   (DAR ES SALAAM)
4
S2549-0086
MOSES J BOSCO
ALPHA   S   S    (DAR ES SALAAM)
5
S4213-0074
YOHANA L MAYENGA
MARIAN BOYS'   S  S   (PWANI)
6
S4213-0044
JOSHUA Z AZZA
MARIAN BOYS'   S   S   (PWANI)
7
S0189-0062
SAID ATWAYA NCHIMBI
FEZA BOYS'   S  S  (DAR ES SALAAM)
8
S0867-0134
LUPYANA L KINYAMAGOHA
PANDAHILL   S   S   (MBEYA)
9
S0101-0350
PETER SEREKA KICHOGO
AZANIA     S   S   (DAR ES SALAAM)
10
S0692-0065
NORBERT S KIMARYO
ROSMINI    S   S   (TANGA)

TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) ULIOFANYIKA FEBRUARI 2013 KWA UFUPI.

Taarifa hii imeidhinishwa na Baraza la mitihani la Tanzania katika kikao chake cha 94 kilichofanyika Mei 30.
Idadi ya watahiniwa wa shule waliofanya mtihani: 42,952
Idadi ya watahiniwa wa shule waliofaulu: 40,242 sawa na 93.92%
Mfumo wa kusahihisha mtihani huu ulitumia Fixed Grade Range na Standardization.
Mchanganuo wa madaraja kwa asilimia:
- Division I - 0.76%
- Division II - 12.54%
- Division III - 70.45%
- Division IV - 10.18%
- Division 0 - 6.08%

Shule kumi bora zenye watahiniwa zaidi ya 30.
1. Marian Girls (Pwani
2. Mzumbe (Morogoro)
3. Feza Boys (Dar-es-salaam)
4. Ilboru (Arusha)
5. Kisimiri (Arusha)
6. St. Mary's Mazinde Juu (Tanga)
7. Tabora Girls (Tabora)
8. Igowole (Iringa)
9. Kibaha (Pwani)
10. Kifungilo Girls (Tanga)

Shule kumi za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 30.
1. Pemba Islamic College (Pemba)
2. Mazizini (Unguja)
3. Bariadi (Simiyu)
4. Hamamni (Unguja)
5. Dunga (Unguja)
6. Lumumba (Unguja)
7. Oswald Mang'ombe (Mara)
8. Green Acres (Dar-es-salaam)
9. High View International (Unguja)
10. Mwanakwerekwe "C" (Unguja)

Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) 2012 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...