Tuesday, May 07, 2013

FBI WAFIKA ARUSHA KUCHUNGUZA TUKIO LA KIGAIDI LA KANISA KUPIGWA BOMU



MAJASUSI wa shirikisho la ujasusi la nchini Marekani wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini Tanzania katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa Vatican nchini siku ya jumapili.
Magesa alitoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipozuru eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali na kuwapa pole.

Wakati maafisa hao wakifika jijini humo tayari vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao wakiwemo watu wanne kutoka Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja kabla ya tukio.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa watu hao walikamatwa muda mfupi wakiondokanchini kupitia mpaka wa Namanga kuelekea nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi zitatolewa kadri muda na wakati utakavyoruhusu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 7, 2013

DSC 0007 83e8a

DSC 0006 a102d

FAHAMU KUHUSU DIAMOND PLATNUM KUBORONGA HUKO LONDON...... ADAM NDITI ANAYECHEZEA CHELSEA AMBWATUKA


Mtanzania ambaye kwa sasa ni raia wa Uingereza na anayechezea klabu ya Chelsea, Adam Nditi ameiponda show ya Diamond mjini Reading nchini humo na kudai ilikuwa ni aibu tupu.

adam na diamond 
“Diamond jana manyago aibu tupu waswahili lazima tubadilike it’s embarrassing,” ametweet.
  
“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa very unprofessional kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1 asubuhi.”
 
“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni alikuwa haimbi.”

Kwa sasa Diamond yupo ziarani nchini Uingereza.

Rais Jakaya Kikwete Afanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji na Kuwateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwa wakurugenzi wa majiji



Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia

--
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji.

Aidha amewateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwawakurugenzi wa majiji.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mabadiliko ya uongozi yamefanyika katika halmashauri za majiji yaArusha, Mwanza, Dar-es- Salaam na Mbeya.

Alisema wakurugenzi walioteuliwa na kuhamishwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa yaTabora, Sipora Liana kuwa Mkurugezni wa Jiji la Arusha na Mkurugenzi wa mji wa Njombe, Hassan Hida kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza.

Ghasia alisema wakurugenzi waliohamishwa ni wa Jiji la Dar es Salaam, Musa Zungiza kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Wilson Kabwe, kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam.

KAULI YA BUNGE KUHUSU MLIPUKO WA BOMU HUKO ARUSHA

KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA KATIKA KANISA KATOLIKI LA YOSEFU MFANYAKAZI PAROKIA TEULE YA OLASITI, ARUSHA MJINI, TAREHE 5 MEI, 2013.


Mheshimiwa Spika,

kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko uliotokea katika Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.

Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhikulitokea mlipuko katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada yakuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzialikuwa ni Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, AskofuFransisco Mantecillo Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake AskofuJosephati Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huoinakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmiakiwa ametoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara yauzinduzi mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo baada ya kutua kulitokeakishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo ulisababisha taharuki miongonimwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.

BARAZA KUU LA WAISLAMU LALAANI VIKALI MLIPUKO WA BOMU NDANI YA KANISA KATOLIKI

TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.


Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini. 
Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu sote, Wakristo na Watanzania wote.

Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.

Wabillahi Tawfiiq.

SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.

Monday, May 06, 2013

SIRI NZITO YAFICHUKA NA YA YULE MFANYA BIASHARA ALIYE JIRUSHA GHOROFANI KARIAKOO!

NYUMA ya habari ya mfanyabiashara tajiri wa Kariakoo jijini, Costa Shirima (47), anayedaiwa kujirusha kutoka ghorofa ya tisa katika Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Mtaa wa Mchikichini, Dar es Salaam na kufariki dunia, kuna siri ambayo Ijumaa Wikienda limeelezwa.
Wananchi wakiwa eneo alipodondoka marehemu Costa Shirima.

Habari za kina kutoka hotelini hapo zilieleza kuwa Shirima alikuwa asafiri kwa ndege ya saa 10:00 jioni, Ijumaa iliyopita kuelekea nchini China kufuata bidhaa za maduka yake.

ALIMILIKI MADUKA KADHAA
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ulibaini kwamba Shirima ambaye alithibitishwa kufariki dunia baada ya kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar, alikuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na hoteli hiyo ya Concord.
Taarifa zaidi zilidai kuwa marehemu mara kwa mara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya hoteli hiyo kupunga upepo.
Ilidaiwa kuwa jamaa zake walipomhoji kulikoni kwenda kupunga upepo mchana wote huo, Shirima alisema kuwa alihisi hewa nzito mahali alipokuwa.

Mwili wa Costa Shirima baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya tisa katika Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Mtaa wa Mchikichini, jijini Dar.

MHUDUMU AFICHUA MANENO YA MWISHO
Madai zaidi yalishushwa na mhudumu mmoja wa hoteli hiyo aliyeomba hifadhi ya jina kuwa jamaa huyo alipoingia mahali hapo, alitaka kupatiwa chumba cha kupumzika lakini alipopelekwa kwenye vyumba vya ghorofa ya kwanza alikataa hadi alipofika ya tisa na kuanza kupunga upepo.

Mhudumu huyo alidai kuwa alikuwa akimsikia Shirima akiongea peke yake akisema “Haiwezekani… haiwezekani kabisa…” na baadaye alipokea simu ya kiganjani ambayo alisikika akibishana na mtu wa upande wa pili.

CHID BENZ AMBATIZA JINA JIPYA NEY WA MITEGO.... ASEMA SASA ATAITWA "NEEMA WA MITEGO"...!!

 
Ugomvi  wa  chini chini kati   ya Chid benz  na  Ney wa  mitego  sasa  umefikia  pabaya.....
Juzi  Ney wa mitego  alionja  kichapo  toka  kwa  mashabiki  katika  show  yake  mbagala....Inadaiwa  kwamba Varangati hilo   lilitokana  na  madai  yake  kwamba   Chid  benz  ni  shoga  na  ametoboa  pua  kama  dem.... 
Mapema mchana huu Chidi Benz amefunguka kupitia ukurasa wake ya Facebook   na  kumtaka  NEEMA  WA  MITEGO(Neema ni jina la  kike aache  kumtukana  wala  kumwandika  message  zozote.....Vinginevyo  ataendelea  kuambulia  kichapo
Hii ni post yake

JANUARY MAKAMBA NAYE AWAPONDA CLOUDS FM KWA KUGOMA KUPIGA "BONGO FLEVA " LEO....!


Huenda mjadala kuhusu uamuzi wa kituo cha radio cha Clouds FM, leo kutopiga Bongo Flava siku nzima haujalikuna sikio la naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Kupitia Twitter, Makamba ameandika kuwa Tanzania ina matatizo matatizo mengi ya kujadili kuliko nyimbo za kuchagua kucheza redioni. “We’ve got much bigger problems than radio playlists, ” ametweet.

Katika mahojiano maalum leo kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alidai kuwa ametoa amri leo kituo chake kisicheze Bongo Flava.

Uamuzi huo leo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Rais Kikwete akatiza ziara nchini Kuwait kurejea nyumbani kuwafariji waathirika wa mlipuko wa Bomu Arusha.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amelazimika kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika  eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Mei, 2013

RAY ‘ASINGIZIWA’ MTOTO WA BATULI.


 
KATIKA hali ya kushangaza, mashabiki wameibuka na kumsingizia mtoto wa mwigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ kuwa ni wa Vincent Kigosi ‘Ray’.
 
 
Vincent Kigosi ‘Ray’.
Ishu hiyo imetokea juzikati katika mtandao wa Facebook ambapo awali, Batuli aliposti picha inayomuonesha akiwa na mwanaye, ndipo shabiki mmoja alipozua mada kuwa mtoto ni wa Ray.
“Manga Msabaha nitake radhi mwanangu anafanana na Vincent Kigosi jamani? Hunitakii mema wewe…jamani sijazaa na Vincent Kigosi pls wadau huyo siyo mtoto wa Ray mshindwe,” aliandika Batuli.
Chanzo ni Global Publishers

MSANII MWINGINE AMUUNGA MKONO LADY JAYDEE KWENYE SAKATA LAKE LA RUGE NA KUSAGA

 
Mkali wa miondoko ya bongo fleva anatamba na ngoma yake kali aliyomshirikisha OMMY DIMPOZI  chukua tyme SUMA MNAZALETI ameyasema maneno hayo leo kwa njia ya masseji Alisema'' ebana nadhani unajua nini kinaendelea kuhusu lady jaydee! nachukua nafasi hii we kaka yangu ambaye umenisaidia sana kwa mda mrefu kukujulisha kuwa mdogo wako,Nitakuwa msanii miongoni mwa wasanii wanao support maneno ya lady jay dee Nakwambia haya kwasababu najua umenisaidia sana,but kama baada ya haya utaamua kuona sifai  sio tatizo pia! no interview 4 NOW  Nilikuwa nakupa habari  kama ndugu yangu wa karibu. lakini kama hili unaliunga mkono sio mbaya ukinijulisha kwamba hakuna tatizo na unaendelea kusaport kazi zangu. alimaliza kwakuandika jina lake suma mnazaleti.

Mwandishi wetu alinyanyua simu kutaka kujua zaidi juu ya sakata hili

mzazi kwanini umeamua kuchukua maamuzi hayo mazito?

Suma alisema ana sababu nyingi sana ambazo zimemfanya amuunge mkono lady jaydee kwenye mambo yake yanayomsibu sasa hivi na kubwa zaidi pia alizungumzia jinsi watu walivyomkatili kwenye tuzo za kili ambako kwenye academi alionekana kupata nafasi zaidi ya 3 kuwa nominies ikiwemo ya wimbo bora wakushirikiana lakini mwisho wa siku hakuingia hata sehemu moja, pili alilalamika kwakutopata airtime ya nyimbo zake kabisa katika kituo ambacho lady jaydee anarushiana nacho maneno na mengine mengi suma mnazaleti alifunguka.

LADY JAYDEE ASEMA''ILE ILIKUWA TRAILER MOVIE NDIO LINAANZA SASA"" TAREHE 15 AU 17 ATAFUNGUKA YA MOYONI

https://sphotos-a.xx.fbcdn.net/hphotos-prn1/p206x206/557919_10151342477575025_1251237535_n.jpg


CUF: SPIKA MAKINDA HAIFAI.

WADAI ANA UWEZO MDOGO WA KUONGOZA.
Mwenyekiti wa TAIFA wa Chama Cha Wananchi –CUF Profesa Ibrahim Lipumba.
Spika wa Bunge,Anne Makinda.

MWENYEKITI wa taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema Spika wa Bunge, Anna Makinda, ameshindwa kukiongoza chombo hicho kwa maslahi ya taifa, badala yake amegeuka kuwa kinara wa upendeleo kwa chama na serikali ya CCM.

Profesa Lipumba amemtaka Makinda atafakari na apime uwezo wake wa kiuongozi katika Bunge na afanye maamuzi magumu ya kubadilika kifikra kwa kuacha upendeleo anaoufanya kwa sasa.


Kauli hiyo aliitoa juzi jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujadili na kuchangia mawazo juu ya maendeleo kwa wote mkoa wa Mwanza, uliofanyika katika Hoteli ya JB Belmont.


Alisema Spika amejionyesha uwezo wake mdogo wa kuongoza Bunge na akubali kushau

riwa au kubadilika kifikra ili alinusuru Bunge lisiendelee kudharaulika ndani na nje ya nchi.

JACQUILINE WOLPER ATUPIWA VIRAGO VYAKE NJE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA.....!!

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kutupiwa nje na baadaye kuzuiliwa vyombo vyake kwenye ile nyumba ya kifahari ya kupanga aliyokuwa akiishi Mbezi Beach, Dar es salaam.

Madai hayo yalitua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu hiyo ilijiri maeneo hayo baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa kulipa kodi ya pango ya mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh. milioni 2.4 za madafu).
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyekuwepo eneo la tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake kwenda kuchukua vyombo hivyo lakini walipofika mama mwenye nyumba (jina tunalo), aliwazuia na kumpigia simu staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa kulipa fedha kabla ya kuchukua vitu vyake.



 

“Wolper alipopigiwa simu alikuja juu na kumwambia mama mwenye nyumba kuwa kama anamfuatilia eti atamfunga kama mume wa mama huyo alivyofungwa na kumwambia kuwa atampelekea polisi wakamkamate,” alidai mtu huyo.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kuona soo limekuwa la kutishana, mama huyo alikwenda kumfuata mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina moja la Musa na kumueleza kisha kumuomba asimamie zoezi hilo.
Baada ya kujazwa data hizo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumsaka Wolper na alipopatikana alisema kuwa hajawahi kudaiwa na huyo mama na anayesema hivyo huenda alimuona wakati anahamisha vitu vyake kwani kwa sasa amehama kwenye nyumba hiyo.
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja la Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba suala hilo lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya kufanya usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia.
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Musa alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia sakata hilo alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper.
Alisema kuwa msanii huyo alikuwa hajamaliza kulipa fedha, akawatuma ndugu zake wakachukue vitu vyake lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba aliwazuia mpaka alipwe chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu vyake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...