Tuesday, April 30, 2013
MH. KOMBANI: WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUKUZA UCHUMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani amewataka watumishi wa Umma kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kukuza uchumi wa nchi.
Waziri Kombani amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaohusu majukumu ya watumishi wa Umma katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano.
Alisema ubora au udhaifu wa utendaji wa serikali yoyote unahusishwa na ubora wa watumishi wa Umma.
“Uchumi hauwezi kukua bila watumishi wa umma kufanya kazi vizuri, katika kukuza uchumi tunategemea,kukua kwa uchumi pia kunategemea watumishi wa umma,” alisema Waziri Kombani.
Waziri Kombani alisema kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo, ingawa inakabiliwa na changamoto mbali mbali.
Pamoja na changamoto hizo, Waziri Kombani amesema Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbali mbali ikiwemo, kupitia na kutafakari jinsi ya kufikia malengo ya maendeleo yake kwa haraka zaidi
Alisema changomoto zilizopo katika utumishi huo ni kuwa huduma zinawafikia wananchi kwa polepole, zisizo na ubora mfano kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaondikishwa katika shule ya msingi na sekondari, lakini kuna tatizo la ubora wa elimu.
“Tunapo sema uchumi wa nchi inatakiwa kumwangalia mtu wa ngazi za chini. Hivyo mkutano huu utakuwa unajadili changamoto zilizopo na nini kifanyike,” alisema.
Aidha aliongeza kuwa wakati mwingine wananchi wanalalamikia kuwepo kwa vitendo vya rushwa.
Hata hivyo Waziri Kombani ametoa wito kwa viongozi kutafuta majibu ya changamoto zilizopo, ikiwemo ongozeko la idadi ya watu, matumizi ya rasilimali na matumizi bora ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Mkutano huo wa siku mbili, unawashirikisha manaibu makatibu wakuu kutoka wizara mbalimbali, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa taasisi za elimu ya juu , sekta binafsi na wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Monday, April 29, 2013
ASKARI MWANAUME ABAKWA NA WANAWAKE WANNE BAADA YA KUTEKWA
Askari mmoja mwanaume anadaiwa kutekwa kisha
kudhalilishwa kijinsia na wanawake wanne kwa karibu wiki moja kabla ya
kupigwa mawe na kutupwa katikati ya milima.
Mateso ya muathirika huyo mwenye miaka 25 yalianza pale alipopata lifti ya gari kuelekea mji wa Mutare nchini Zimbabwe.
Wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa
kwenye gari, Mercedes Benz, na, baada ya kuendesha kwa takribani saa
moja kuelekea mji huo, dereva wa gari hilo akabadili mwelekeo wa safari
hiyo.
Ndipo muathirika
huyo akalalamika, alitishiwa kwa kisu.
Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula.
Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula.
"Askari huyo alitaka kushushwa, lakini
dereva huyo akatoa kisu na kumtishia nacho. Mmoja wa abiria wanawake
akamfunga kwa kitambaa cheusi machoni mtuhumiwa huyo."
Kwa mujibu wa Nuzondiwa,watesi hao
walimpeleka mlalamikaji kwenye nyumba isiyojulikana ambako walimvua
nguo zote na kumpora simu yake na Dola za marekani 35.
Watuhumiwa walimwamuru mtu huyo kulala na
mmoja wa wanawake hao katika matukio kadhaa na alishikiliwa kati ya
Aprili 19-23.
Kisha akafungwa tena kitambaa machoni na kushushwa kwenye
Milima ya Dangamvura ambako, kwa mujibu wa polisi, alipigwa mawe katika
mguu wake wa kushoto, na kumsababishia majeraha makubwa.
Watuhumiwa hao kisha wakawasha gari lao na
kutokomea kusikojulikana.Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha
Sakubva
Mbowe amtwisha mzigo mzito Zitto
Tabora. Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe
kuhakikisha chama kinapata ushindi katika majimbo mengi kwenye uchaguzi
mkuu ujao.
Mbowe alisema chama chake
kitahakikisha kinachukua majimbo ya Samwel Sitta, (Urambo Mashariki),
Ismail Aden Rage (Tabora mjini) na Jimbo la Kaliua la Profesa Juma
Kapuya, katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe alimwagiza mbunge
huyo wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kwamba majimbo hayo yanachukuliwa
na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Alimtaka kufanya kampeni za mtaa kwa
mtaa, nyumba kwa
hadi nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.
hadi nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Town School mjini Tabora, pamoja na mambo mengine alisema anazindua
kampeni hiyo kwa ajili ya mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi ambapo Zito
Kbwe alikabidhiwa jukumu la kuisimamia kanda hiyo.
Aliwageukia polisi na kuwataka kukiunga mkono chama hicho ili
kikifanikiwa kuingia madarakani kiweze kuwaboreshea mishahara yao kuliko
ilivyo sasa akidai wanalipwa mishahara kiduchu ikilinganishwa na ugumu
wa kazi yao.
“Nyie makamanda nanyi mmepigika kama
sisi, sasa ninachowaomba tuungeni mkono kupambana na hawa CCM ili
tuwakomboe wanyonge,” alisema Mbowe.
Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alisema Kanda
ya Magharibi ina historia katika nchi kwa Mkoa wa Tabora kuwa kitovu cha
mapambano ya uhuru wa nchi na Kigoma kuwa kitovu cha mapambano ya
mageuzi.
Mwananchi
SHILOLE ALONGA BAADA YA KUNASWA AKILA BATA COCO BEACH NA BARNABA
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka
kuwa hakuna kinachoweza kumtenganisha na msanii wa muziki wa kizazi
kipya, Elius Barnabas ‘Barnaba’ kwani walikotoka ni mbali.
Shilole na Barnaba hivi karibuni walinaswa maeneo ya Coco Beach wakila bata lakini baada ya kuwaona mapaparazi wakizunguka kutafuta matukio, Barnaba alitimua mbio na kumuacha Shilole ambaye bila hiyana alitiririka:
“Jamani mimi na Barnaba hakuna cha kututenganisha japokuwa watu wanachonga sana hata kuandikwa kwenye magazeti lakini bado tunaendelea tu, hivyo najua hakuna mtu anayeweza kututenganisha.”
PADRI AFUMANIWA NA MKE WA MTU! STORY NA PICHA KAMILI HIZI HAPA
KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya
padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa
kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina
sakata zima.
MSHANGAO: Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
MSAMAHA: Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe (jina tunalo) alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani."
MSHANGAO: Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
MSAMAHA: Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe (jina tunalo) alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani."
MIAKA 13 YA LADY JAY DEE KWENYE MUZIKI KUDONDOSHA BONGE LA PARTY
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika
mwaka huu 2013,
Inatimia miaka13 tangu nianze kazi ya muziki.
Nashukuru
MUNGU
tukopamojanapia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea ku support
muziki wa
Tanzania nakunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru
vyombo vyotevya
habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania
bila kujali
maslahi binafsi.
Tumeandaa
sherehe kubwa
na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki. Na mdhamini mkuu kwa
upande
wa media ni East Africa TV. Shereheyamiaka 13 ya Lady Jay Dee katika
muziki itaambatana
na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT
THE TRUT
ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika
sherehe hizo pia
kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za Jay Dee nikishirikiana na baadhi
ya wasanii
wenzangu hapa nchini.
Sherehe
zitafanyika Ijumaa
tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha
wote tufurahi
pamoja
Na
Mungu awabariki
AY Kuachia "JIPE SHAVU" Jumatano Hii ..
!!! YEEESAYAAH !!!
Mwanamuziki kutoka Tanzania, Ambwene Yessayah a.k.a AY au
pia unawweza kumuita "Zee La Commercial" anataraji
kuachia ngoma yake nyingine hivi karibuni ...
AY ambae
bado machoni mwako anafanya vizuri na video SPEAK WITH YA BODY,
PARTY ZONE na MONEY zinazopigwa katika
televisheni kubwa duniani kama Channel O na TRACE
TV ya Ufaransa soon anaachia JIWE hilo
litakalofahamika kama JIPE SHAVU ...
JIPE
SHAVU is the next single from AY akiwa
amemshirikisha mshkaji wake wa karibu akijulikana Fid Q [that
Illest Hip-Hop dude from MWANZA City] ...
Hapa "Zee La
Commercial" na hapa pembeni ni "Zee La Hardcore" ...
JIPE SHAVU ...
Dundo hilo according
to AY, limefanywa na Producer Q ikiwa
ni katika studio za MPO AFRICA zilizopo maeneo ya
mikocheni ...
AY anasema ngoma hiyo
itaachiwa rasmi jumatano hii katika sehemu tofauti ... As to fans wakae
tayari kupokea kazi nyingine bora kabisa kutoka kwake ...
AY na
rapper Fid Q waliwahi kufanya ngoma mbali mbali nzuri
za pamoja ikiwemo USIJARIBU yenye video yake pia ...
Let's wait for JIPE
SHAVU afu tuone ...
"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER
Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa
mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo.
Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.
Source: Mwananchi
Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.
Source: Mwananchi
Sunday, April 28, 2013
GARI JIPYALA MILIONI 35 ALILONUNUA NEY WA MITEGO PAMOJA NA BASTOLA HAPA
Mwaka 2013 ni mzuri kwa rapper Nay wa Mitego.
Licha ya kuwa na hit single hewani, Muziki Gani aliyomshirikisha
Diamond, rapper huyo amenunua ndinga mpya aina ya Mark X yenye thamani
ya shilingi milioni 35. Kama hiyo haitoshi, hitmaker wa Nasema Nao,
amejihami pia kwa kununua bastola.
Nay ameshare picha hizo kwenye Instagram na Facebook ambapo miongini mwa
picha za gari lake ameandika, ‘My new car. Mark X, Zic z wat I nid.”
Mwaka huu Nay ametumiwa kwenye show nyingi za Airtel na Vodacom ambazo
huenda zimemwingizia mkwanja wa kutosha.
Nay akiwa na bastola yake
MBUNGE LEMA AZUILIWA KUPIGA MSWAKI WALA KUNYWA CHAI AKIWA MAHABUSU...... !!
Lema ambaye bado anaendelea kusota rumande siku ya tatu baada ya kunyimwa dhamana, ameanza kufanyiwa vituko na Jeshi la Polisi baada ya jana asubuhi mkewe kuzuiliwa asimpe mswaki wala chai.
Mbunge huyo alikamatwa kutokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliyedai kuwa aliwachochea wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kumzomea kiongozi huyo na kupopoa gari lake kwa mawe.
Hata hivyo, siku moja kabla ya kukamatwa Lema aliwaonesha waandishi wa habari ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani aliyotumiwa na Mulongo akimtishia kuwa atamfungulia kesi yoyote anayoitaka.
“Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.
MSANII SIZE NANE ALILIA BIKRA YAKE HADHARANI...!!
Mwanamuziki aliyeitikisa vilivyo Kenya kabla ya kuokoka na
kuachana na muziki wa kidunia, mwanadada Size 8 sasa ameanza
kufunguka katika interview kwenye vituo mbali mbali vya redio na Tv kuhusiana na maisha mapya ya kidini.
Kati ya mambo yote ambayo Size 8
amekuwa akiyaongelea, ni moja tu ambalo amekuwa akilitilia mkazo kwa
kumaanisha kuwa linamsikitisha zaidi .....Jambo hilo ni lile la kupoteza
BIKRA YAKE.....
Size 8 ameziambia media kuwa "Najutia
sana kupoteza bikra yangu. Ninaamini kuwa kijana anatakiwa kujilinda
na kujizuia kufanya ngono katika ujana wake wote mpaka atakapo pata
kibali toka kwa Mungu."
KIONGOZI WA KANISA AZIKWA AKIWA HAI
Msaidizi
wa zamani wa Padri (Katekisita) katika Kigango cha Kanisa Katoliki
Kijiji cha Mkwajuni, Florian Mwamosi (70) amekufa baada ya kuzikwa akiwa
hai katika kaburi moja na mtu anayedaiwa kumuua kwa njia ya
kishirikina.
Tukio hilo limetokea katika Kitongoji
cha Maweni kijijini hapo wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alikiri kutokea kwa tukio hilo
akieleza kuwa lilitokea saa 9:00 mchana katika kijiji hicho cha Maweni
Mkwajuni wilayani Chunya.
"Marehemu
aliuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na mawe kwa tuhuma za
kuhusika na uchawi na kusababisha kifo cha Peter Robert," alisema.
Kamanda Athumani alisema kuwa
uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea na kwamba wahusika wote wa
tukio hilo wamekimbia na kuzihama nyumba zao, hivyo polisi wanaendelea
na msako wa kuwatia mbaroni watuhumiwa na kwamba tayari kaburi hilo
limefukuliwa jana kutenganisha maiti hizo.
Subscribe to:
Posts (Atom)