HUKUMU ya kesi iliyokuwa
inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe
imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela
miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda
jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Monday, March 25, 2013
ISHA MASHAUZI NAYE BINGWA WA MADAWA YA KULEVYA AKILI MWENYEWE.......!!!
STAA wa muziki wa taarab na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ ameibua gumzo na kushangaza mashabiki baada ya kukiri kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe kali na madawa ya kulevya aina ya mirungi
Ishu hiyo ilijiri Alhamisi ya wiki iliyopita wakati akihojiwa na mtangazaji wa Redio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ kupitia kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani ambapo alisema mirungi na pombe kali ndiyo starehe yake kwani inampa stimu kabla hajapanda jukwaani na katika maisha yake ya kawaida nje ya usanii.
Mashauzi alifunguka hayo baada ya Dida kumtaka atoe ufafanuzi juu ya skendo ya kuvuta bangi inayomkabili ambapo alisema siyo kweli kwamba anavuta bangi ila akakiri kuwa anakula sana mirungi na kugida ulabu. Aliongeza kwamba kwa kuwa hana mume, mtoto wala hataki kuwa na familia, mirungi na pombe ndiyo vitu vinavyompa furaha maishani mwake.
UKWELI KUHUSU ELIMU YA NAIBU WAZIRI WA MH. MLUGO HUU HAPA
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.
Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.
Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.
Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.
“Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na kuongeza:
“Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona.”
Waliomfundisha
Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.
Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.
Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.
Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.
Chanzo: Mwananchi
CHID BENZ AANZA UGOMVI TENA AMPIGA NGWEA CLUB
Chid Benz
Rapper Chid Benz, amempiga Cow Bama
a,k,a Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku
wa kuamkia leo.ugomvi huo ulitokea baada ya Chid
kumzingua Dully alipokua akiingia, ambapo
mwisho wake aliamua kuondoka. Alipoondoka Dully Ngwea akamuuliza
inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chid alipopaniki na kuanza kutoa
lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana Ngwea
aliamua kukaa kimya lakini Chid aliendelea kungea kwa hasira na kusema
"ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia NgweaMADARAJA MAPYA YA KUFAULU KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE
Serikali kwa kupitia wizara ya elimu
imefanya mabadiliko kwenye madaraja ya alama za mitihani ya kidato cha
nne. Hapo awali, madaraja yalikuwa ni kama ifuatavyo:
A = 81%-100%
B = 61%-80%
C = 41%-60%
D = 21%-40%
F = 0%-20%
Mabadiliko mapya yamefanywa na
sasa madaraja MAPYA ni kama ifuatavyo:
A = 80%-100%
B = 65%-79%
C = 50%-64%
D = 35%-49%
F = 0%-34%
Taarifa imetolewa mapema ili
wanafunzi kwa kidato cha nne waanze kujiandaa vyema na mitihani ijayo
MJUE MWANAMUZIKI ALIYEMTOA KAFARA RAFIKI YAKE ILI APATE UMAARUFU
Baada ya kuvuta bangi, mwanamuziki
mmoja nchini marekani (RAPER) anayefahamika kwa jila EL-ARMIN amtoa
kafara rafiki yake ili kupata umaarufu, raper huyo aliamini akimuua
rafiki yake atapata umaarufu nchini marekani na kupaa kama wasanii
maarufu nchini humo. vyombo vya habari nchini marekani
vimeripoti kwamba El-armin aliamini kwamba kutoa kafara ni ishara ya
mafanikio,
Kabla ya kumuua rafiki yake huyo aliwekea risasi kichwani kwa rafiki yake na kusema "wewe ni kafara yangu" rafiki yake huyo alizuia pisto na alijua ni utani. baada ya dakika chache El-armin alimshoot rafiki yake tumboni na rafiki huyo kufa papohapo.
Ndoto zake hatimaye zimepote na amefungwa kifungo cha muda mrefu, masupastaa wakubwa kama 50cent, beyonce, lady gaga,kanye west je huwa wanafanya hivyo?
Mbatia aitaka serikali kuacha kutoa maamuzi ya kibabe na badala yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari.
Na.Mo
Blog Team.
Serikali
nchini imetakiwa kuacha kufanya mambo bila kutaka ushauri katika
masuala ya kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitalii na badala
yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kupata muafaka
wa kweli na ikibidi ivipe ruzuku ili kuhakikisha uendeshaji wa vituo
hivyo katika mfumo huo mpya unafanikiwa.
Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (pichani), ameitaka
Serikali ikubali kwa nia njema kabisa angalau kwa muda wa miezi sita
ijayo au hata mwaka mzima ujao kwa mikoa mitatu, kutumia mfumo wa
analojia kwa kuwa ndio walikuwa wamejiandaa nao na ndio walikuwa
wamesajili nao vyombo hivi ili kujiandaa kuingia kwenye digitali.
Hata
hivyo serikali yenyewe imeshatoa tamko kwamba haitorudia nyuma kwenye
mfumo wa analojia na badala yake itaendelea kusonga mbele katika mfumo
wa digitali kwani tayari mfumo huo ni mfumo wa kiulimwengu.
Suala
hilo limeleta changamoto kubwa na wadau mbalimbali wa masuala haya ya
habari ambao wametaka kuwepo na mazungumzo ili kuweza kufikia muafaka
mzuri katika uendeshaji wa vyombo hivi vya habari kwa kuwa wenyewe
wanaona ni mzigo mkubwa kwa sasa kuingia katika mfumo huo wa digitali.
Rais Xi Jinping wa China awasili nchini kwa ziara ya siku mbili apokewa na Rais Jakaya Kikwete
Rais
wa China, Mhe. Xi Jinping na mke wake wakiteremka kwenye ndege mara
baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili hapa nchini.
Mhe.
Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiwa katika Jukwaa Maalum
wakati nyimbo za mataifa yao zilipokuwa zikipigwa sambamba na mizinga
21 kwa heshima ya Mhe. Rais Xi Jinping.
Mhe.
Rais Xi Jinping akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa kwa heshima
yake.
Mhe.
Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwasalimia baadhi ya kina mama wa
Dar es Salaam waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi.
Mhe.
Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na wake
zao wakifurahia burudan iliyokuwa ikitolewa na moja ya viku ndi vya
burudani vilivyokuwa uwanjani hapo mara baada ya Rais Xi Jinping
kuwasili nchini.
Mhe.
Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiondoka uwanjani hapo mara
baada ya mapokezi.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa
Sunday, March 24, 2013
MBEYA WABAINI CHANZO CHA WANAFUNZI KUFELI
OFISA Elimu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda ametangaza kiama kwa watu wanaomiliki vituo vya kufundishia watoto masomo ya awali baada ya kubaini kuwa ndiyo chanzo cha kuwa na wanafunzi wanaongia darasa la kwanza bila kujua kusoma na kuandika.
Kaponda aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkapa jijini hapa na kuwahusisha watendaji kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kujadili changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi.
Akitoa ufafanuzi, ofisa huyo aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa baada ya kubaini hiyo ni moja ya sababu ya kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani hapa, ofisi yake imejipanga kuvikagua vituo vyote vya masomo ya awali.
Alisema vituo vingi vya chekechea ndiyo chimbuko la maandalizi mabovu ya wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza ambao licha kusoma miaka miwili, wengi wao wamekuwa hawajui kusoma na kuandika hivyo kukosa sifa ya kujiunga darasa la kwanza.
Kaponda alisema hali hiyo imechangia hata wanafunzi wanaojiunga na elimu ya kidato cha kwanza pia baadhi yao kuwa na uwezo mdogo kutokana na msingi mbovu, hivyo kushindwa kusoma na kuandika.
Aidha, ofisa elimu huyo amewatupia lawama wasimamizi wa mitihani kwa kujihusisha na rushwa na kwamba ofisi yake inaendelea kujipanga kukabiliana na changamoto hiyo.
Dk. Michaeli Kadeghe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, alisema suala la kufeli kwa wanafunzi na baadhi yao kutojua kusoma na kuandika, ni aibu ingawa tayari taarifa zao zinaonesha kuwa wamefaulu mitihani.
Alisema mfumo wa mitaala ya elimu hapa nchini ndilo chimbuko la ubovu huu kwa kuwa haiwezekani wanafunzi wakaendelea kuwa na mfumo wa kuchagua majibu, hivyo ni mambo yanayopaswa kusitishwa haraka.
Mkuu huyo alisema kwa mfumo wa mitaala hiyo, ndiyo inawafanya hata wasiojua kusoma na kuandika kufaulu kwa staili ya kubahatisha katika mitihani yao, hivyo ni wakati mwafaka wa kufanya mabadiliko katika jambo hilo kwa wanafunzi kupimwa uelewa.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na watendaji wa serikali kutoka katika wilaya zote za mkoani hapa pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na makundi mengine ya kijamii, kilikuwa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Normani Sigala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Abasi Kandoro.
Chanzo;Tanzania daima
JACK CHUZI WA BONGO MOVIE AOLEWA BAADA YA KUKUBALI KUBADILI DINI....!!!
Katika Hali ya Kushtusha na
Kufuraisha....Staa wa Bongo Movie Jack Pentezel amewashtusha wengi baada
ya Kuamua kubadili dini kuwa Muislamu kisha kuolewa na Mpenzi wake wa
Muda Gadner Dibibi....
wadau wengi na wapenzi wa Bongo
Movie wamekuwa wakihoji juu ya Ndoa Hiyo iliofungwa kisiri sana na kwa
haraka,Je Ndoa Hiyo Itadumu? Je ni kweli wamehamua kukaa kwenye Maadili
ya Ndoa..? au Ni kama Mchezo wa Mjini kubadilishana Dini na kuoana
mwishowe ni kuachana....Tusubiri Tuone.....
Mpekuzi inapenda kumtakia Jack
Pentezel na Mumewe Gadner Dibibi Baraka Tele,Amani na Upendo utawale
kwenye Maisha yao ya Ndoa..
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NYUMBANI KWAKE
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia
hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013
baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi
karibuni alipougua ghafla. Picha na OMRMakamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia
hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013
baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi
karibuni alipougua ghafla. Kulia ni Mke wa Mzee Kingunge. Picha na OMRMakamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia
hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013
baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi
karibuni alipougua ghafla. Picha na OMR
WASICHANA WADOGO NAO WAINGIA KATIKA BIASHARA YA NGONO KWA SH. 5000
Ni usiku wa saa 4 nipo katika eneo maarufu la
Buguruni lililopo jijini Dar es Salaam nikiwa nimekaa napata kinywaji
kwenye baa moja.
Katika eneo hilo ambalo lipo
pembezoni mwa Barabara ya Mandela si tulivu sana kutokana na pilika
pilika za magari na watu wanaopita karibu kwa shughuli mbalimbali.
Huku nikiendelea kupata kinywaji
mara naona wasichana wadogo wenye umri wa miaka 14 hadi 16 wakizunguka
zunguka katika eneo hili la baa.
Awali nilifikiri walikuwa
wakitafuta msaada au wakipita kuelekea nyumbani kwao, kwani umri wao
haukunipa picha kwamba walikuwa kazini wakati huo wa usiku wa kiza
kinene.
Kilichonifanya niwaangalie kwa
udadisi zaidi ni kuona jinsi walivyovaa nguo ambazo zilionyesha nusu ya
sehemu zao za mapaja, huku kifuani wakiwa wamevaa blauzi zilizobana
zikionyesha matiti yao madogo ambayo yanaanza kuchipua.
Hawa ni sehemu ndogo tu ya wasichana wadogo ambao hukesha usiku kucha katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam wakitafuta wateja ili wapate fedha za kujikimu.
Mwandishi analazimika kuwadadisi
wasichana hawa ili kujua nini kilichosababisha waingie katika biashara
hii.
Inavyokuwa
Mwandishi ana mwita mmoja wa
wasichana hawa Neema Mashiri (16) (sio jina lake halisi) na kuongea naye
katika sehemu tulivu katika baa hiyo huku wakitumia vinywaji kunogesha
mazungumzo.
Neema akiwa mwenye kujiamini na
kazi yake bila ya kutetereka anasema kazi hiyo aliianza zaidi ya miezi
sita nyuma huku akiwa tayari amekutana na idadi ya wanaume ambayo
haikumbuki kutokana na wingi wake.
“Kwa siku moja nakutana na wanaume
katiya watano hadi saba na hii hutegemea siku na siku, kwani kuna siku
huwa na biashara ya kutosha na tunapata fedha za kutosha,”anasema Neema.
Neema akieleza ujira ambao hulipwa
anasema ni Sh3,000 hadi Sh5,000 kwa muda usiozidi dakika 30 kwa
mwanamume mmoja huku wakati kwa yule anayetaka kulala naye hadi asubuhi
hutakiwa kulipa Sh10,000 hadi Sh15,000.
“Baadhi ya wanaume wamekuwa
wakitufanyia vitendo vya kikatili kwa kutuingilia kinyume cha maumbile,
lakini kutokana na hali ngumu ya maisha hukubali kwani dau huwa kubwa
Sh10,000 hadi Sh12,000, lakini wengine hutumia ubabe tu na kututumia
bila kutulipa,” anasema
Neema na kuongeza;
WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WAJIPIGA PICHA CHAFU WAKATI WAKIFANYA ZINAA....!!
Wanafunzi watatu wa chuo maarufu
nchini wametia aibu ya mwaka baada ya kunaswa wakivunja amri ya
sita huku wakijipiga picha chafu za tukio hilo..... Kwa mujibu wa ripota wetu, tukio hilo la aibu linahusisha wanaume wawili na msichana mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Fetty..... Kuvuja kwa picha: Picha hizi zinadaiwa kusambaa na kumfikia mpekuzi wetu baada ya wanafunzi hao kutofautina na hivyo kuamua KUTUBU DHAMBI HII kwa staili ya KUUMBUANA |
BINTI ABAKWA KIKATILI NA VIJANA WAWILI....
Daily post imepokea video moja
ya kusikitisha sana ikimuonesha msichana mmoja akibakwa na
wavulana watatu.....
Katika
video hiyo, binti anaoneka kulia kwa huzuni akiomba msaada.Bahati
mbaya, shetani hao wawili hawakuwa na tone la huruma kwa binti
huyo.....
Watu hao ni wakenya na wanaongea
kiyoruba.
Ifuatayo ni sehemu fupi ya video
hiyo:
Video inafunguka kikatili
ikimuonesha ikimuonesha binti akiwa amekabwa na anapumua kwa
shida...
Binti:
Nisaiidiee..( huku nalia)
Mbakaji:
Jitahidi usioneshe sura yangu..( alikuwa anamweleza mwenzie aliyekuwa
anarekodi)
Anayerekodi:
Usijali, siichukui sura yako
Binti:
Nimewakosea nini...nakufaaa...!!!
Mbakaji aliendelea kusisitiza
kuwa sura yake ifichwe na binti aliendelea kuomba msaada bila
mafanikio....
Hiyo
ni picha ya mbakaji kama kuna mtu atafanikiwa kumtambua....
Credit: Dailpost-kenya
|
SHY - ROSE 'AMVUA NGUO' WAZIRI SITTA
SHY - ROSE |
MBUNGE wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji
amemtaka Waziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC),
Samuel Sitta kuacha ubabaishaji kwa kutoa kauli za uongo kwa Watanzania
na badala yake aongeze kasi ya uwajibikaji.
Shy-Rose alisema hayo jana akijibu
kauli ya Waziri Sitta kwamba baadhi ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EALA), akiwemo yeye hawahudhurii vikao vinavyoitishwa na
wizara hiyo na kwamba wamekuwa wakidai posho.
Akijibu kauli hiyo kwa maneno makali,
Shy-Rose alimtaka Waziri Sitta na naibu wake kutoa vielelezo dhidi ya
madai yao.
“Kama nilivyosema kwenye kikao cha
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wizara
imejitenga sana katika kutoa mwongozo na vile vile katika kuwafikia
Watanzania walio wengi kwa kigezo kwamba haina fedha.
“Nimekuwa nikiwasiliana moja kwa moja
na Naibu Waziri Abdullah Juma Sadallah kuhusu masuala mengi kwa maana
ya kushirikiana na kupeana mwongozo, lakini majibu ya Naibu Waziri daima
yamekuwa ni ya ubabaishaji na ya kukatisha tamaa, akisema kwamba
wabunge wa EALA hawako chini ya wizara,” alisema Shy-Rose.
Mbunge huyo amemtaka Waziri Sitta kukaa na
viongozi wa wizara yake ili apate ukweli wa mambo kuliko kurukia kujibu
hoja kwa ubabaishaji kwani nia ni kuweka maslahi ya nchi mbele na si
binafsi kama alivyofanya juzi yeye na naibu wake kwenye kikao cha
kamati.
“Kwa vile amenitaja mimi moja kwa
moja kuwa ni kinara wa kutoa udhuru… nasema si kweli hata kidogo…
ninamheshimu Waziri Sitta kama kiongozi na kama mzazi wangu, lakini
kauli yake imenisikitisha sana sana kwani amenifedhehesha kwenye jamii
kwa kutoa kauli za kunichafulia jina langu kwa vile nimesema ukweli.
“Ni Waziri Sitta huyo huyo kwenye
kikao cha bajeti mwaka jana bungeni Dodoma nilikuwa miongoni mwa wabunge
aliowapongeza kwa kazi nzuri. Leo iweje abadili kauli yake? Au ni kwa
vile nimesema ukweli?” anahoji Shy-Rose na kuongeza kuwa penye ukweli
hatasita kuwaumbua viongozi ambao hawawajibiki.
Kuhusu suala la posho, alisema
walialikwa mara moja tu bungeni lakini waliambiwa kila mtu ajigharamie
malazi na usafiri.
“Hivi inaingia akilini kweli ualikwe
kwenda safari halafu unaambiwa ujigharamie? Yeye Sitta na Naibu Waziri
kwa vile wanatumia magari ya wizara na kuwekewa mafuta na kupewa posho
kufika bungeni ndiyo maana inamwia rahisi kuongea kiubabaishaji.
“Licha ya wizara kukataa
kutugharimia, lakini nilikuwa miongoni mwa wabunge waliohudhuria kikao
cha bajeti ya wizara huko Dodoma… hiki ni kielelezo tosha kabisa suala
la posho ni agenda ya uongo ili wizara kujisafisha kwenye kamati na
Watanzania kwa ujumla.
“Hivi inaingia akilini kweli eti
tunadai posho kuhudhuria vikao vya kupewa mwongozo tena hapa Dar?”
anahoji Shy-Rose na kuongeza kuwa suala la posho kwake binafsi
halijawahi kuwa agenda kuu hata siku moja.
“Hii hoja ya posho si ya kweli hata
kidogo, kilichoongelewa ni vipi tunafika Dodoma iwapo hatujui tutalala
wapi na tutakula nini. Sijaomba gharama hizi kama Shy-Rose bali kama
Katibu wa Wabunge wa EALA,” aliongeza.
Shy-Rose alisema ni jambo la
kusikitisha kwamba Watanzania walio wengi hawaifahamu Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa upana wake, hivyo juhudi za ziada zinahitajika kwa wizara
kushirikiana na wabunge wa EALA ili kuwafikia Watanzania wengi kufahamu
mtengamano huu.
Mbunge huyo alisema semina pekee
iliyowahi kufanyika kwa wabunge wa EALA ilikuwa mara baada ya
kuchaguliwa takriban miezi kumi iliyopita.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa na
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na wizara, waliambiwa wizara itakuwa
inatoa mwongozo kabla ya vikao vya Bunge kuanza ili kuweka maslahi ya
taifa mbele na baada ya hapo hawajawahi kuitwa tena na wizara hiyo.
Kwa mujibu wa Shy-Rose, kikao pekee
kilichoitishwa na wizara ni Januari mwaka huu jijini Bujumbura wakati
ambapo mbunge huyo alikuwa nchini India kwa matibabu.
Juzi wakati Waziri Sitta akitoa
ufafanuzi katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Sitta alisema madai ya wabunge wa
jumuiya hiyo kwamba hawashirikishwi katika vikao vya wizara yake sio ya
kweli kwani wengi ni mabingwa wa kutoa udhuru na wanataka posho.
TANZANIA DAIMA
Subscribe to:
Posts (Atom)